Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu kuwa sehemu ya Halmashauri hiyo katika ukusanyaji wa mapato ili Halmashauri hiyo iweze kupanda katika ukusanyaji mapato na kupata uwezo wa kujiendesha.
Mmbaga
ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa tarafa ya Kinang’weli
wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasiliza na kuzungumza
na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.
‘Halmashauri
yetu haifanyi vizuri katika ukusanyaji wa mapato, kutokana na hali hii ya
ukusanyaji baadi ya masuala yenu muhimu kama watumishi mnaweza msiyapate kwa
wakati hivyo kila mtumishi ajulikane kama afisa mapato wa halmashauri, hili si
jukumu la Mkurugenzi na Mtunza Hazina wa Halmashauri pekee, wote mshirikiane kukusanaya
mapato kwa uadilifu,” alisema Mmbaga.
Aidha,
Mmbaga amewataka watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima kuwa waangalifu
katika matumizi ya mapato yanayokusanywa kwa kuhakikisha wanawekeza katika
maeneo yenye tija na matokeo.
Sambamba
na hilo Mmbaga amewataka watumishi hao kuziba mianya yote ya ubadhilifu na
kumwataka viongozi kuwachukulia hatua watumishi watakaothibitika pasipo shaka
kuwa wamefanya ubadhilifu wa mali za umma na katu wasiwafumbie macho.
Kwa
upande wao watumishi wa lioshiriki katika kikao hicho walipata fursa fursa ya
kuwasilisha changamoto zao ikiwa ni pamoja na kuomba Katibu Tawala wa Mkoa kama
Mkuu wa Utumishi wa Umma ndani ya Mkoa aweze kuzipatia ufumbuzi ambazo ni kulipwa
stahiki zao ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara, madai ya fedha za
kujikimu na nauli kwa watumishi wapya, upandishwaji wa madaraja na suala la
uhamisho.
Katika
kuyapatia ufumbuzi masuala haya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam
Mmbaga amesema ni vema wakuu wa taasisi wapewe taarifa sahihi juu ya
upandishwaji wa madaraja na uhamisho wa watumishi ili waweze kuwaelimisha na
kuwapa taarifa sahihi za masuala hayo watumishi walio chini yao.
Aidha,
Mmbaga amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya itilima kuweka mpango
mkakati wa kulipa madai mbalimbali ya watumishi ikiwa ni pamoja na nauli na
fedha za kujikimu ili waweze kulipwa kulingana na halmashauri itakavyopata
fedha.
Naye
Afisa Utumishi wa Halmashauri amesema suala la kupandishwa madaraja kwa
watumishi walioajiriwa kuanzia mwaka 2014 halijafanyika kwa nchi nzima si kwa
Itilima peke yake hivyo amewasihi watumishi hao kuendelea kuwa watulivu mpaka
yatakapotolewa maelekezo na Ofisi ya Rais Utumishi juu ya upandishaji wa vyeo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya
Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo amewataka wakuu wa shule na wakuu wa Vituo vya
kutolea huduma za afya wilayani humo kuyawekea mipaka asili maeneo yaliyo chini
yao ili kuepusha maeneo hayo kuvamiwa na wananchi ambapo uvamizi huo unaweza
kuleta migogoro katika jamii inayozunguka taasisi hizo.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi ya watumishi wa tarafa ya
Kinang’weli wilayani Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasiliza na
kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.
Baadhi ya watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akiwa katika kikao pamoja nao wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo akifafanua jambo katika
kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya
watumishi wa tarafa ya Kinang’weli wilayani
Itilima wakati wa ziara yake yenye lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na
watumishi iliyofanyika jana Februari 26, 2021.
Mmoja wa watumishi wa
tarafa ya Kinang’weli wilayani Itilima akichangia hoja katika kikao cha Katibu
Tawala wa Mkoa Bi. Miriam Mmbaga na watumishi hao, wakati wa ziara yake yenye
lengo la kuwasikiliza na kuzungumza na watumishi iliyofanyika jana Februari 26,
2021.

Afisa Utumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Upendo Haule akifafanua jambo katika katika