Tuesday, September 26, 2017

TCRA YATOA ELIMU KUHUSU HUDUMA YA KUHAMA MTANDAO MMOJA WA SIMU KWENDA MWINGINE BILA KUBADILI NAMBA

Mamlaka ya Mawasiliano hapa nchini (TCRA) imetoa elimu kuhusu huduma ya kuhama kutoka Mtandao mmoja wa Simu kwenda Mtandao mwingine bila kubadili Namba ya Simu(Mobile Number Portability- MNP) mkoani Simiyu.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mjini Bariadi Mhandisi Mwandamizi wa Mawasiliano Mwesigwa Felician kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA), amesema huduma hii ni ya hiari  na inampa uhuru na kumwezesha mtumiaji wa huduma ya mawasiliano kuhamia mtandao wowote anaoutaka na kuendelea kupata mawasiliano bila kulazimika kubadili namba yake ya simu.

“Namba ya simu ya Mteja itabaki ile ile na itakuwa ni kitambulisho chake, yaani (NAMBA YAKO KITAMBULISHO CHAKO) kokote atakapohamia watu watampata, hakuna haja ya kuwataarifu marafiki,familia,  wafanyakazi wenzake au washirika wenzake katika shughuli zake kama ilivyo sasa. Tunatoa elimu hii kwenu waandishi wa habari ili na ninyi muifikishe kwa wananchi kupitia kazi zenu” amesema Mhandisi Mwesigwa.

Amesema huduma hii inamwezesha mtumiaji wa huduma za mawasiliano kuchagua mtoa huduma mwenye huduma bora zaidi(quality of service), huduma nzuri kwa wateja(customer care services), ubunifu katika kutoa huduma zake hivyo kuongeza ushindani kwenye sekta ya mawasiliano na kuchochea utoaji huduma bora na zenye gharama nafuu.

Ameongeza kuwa huduma hii inatolewa kwa wateja wa malipo ya kabla(pre paid) na malipo baada ya huduma(post paid) kupitia vituo vya mauzo au wakala anayetambuliwa mtoa huduma (Makampuni ya Mawasiliano/Simu), ambapo watumiaji wa mawasiliano watakaohitaji huduma hiyo watatembelea maeneo hayo ili kupewa utaratibu wa kuhama.

“Mtu anayetaka kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadiliha namba yake anapaswa kufika katika Vituo vya mauzo au wakala wa mtandao anaotaka kuhamia, kupata utaratibu na akiona ipo haja ya kuhama tena itamlazimu akae kwa mtoa huduma huyo mpya kwa muda usiopungua siku 30 kabla ya kurudi kwa yule awali au kuhamia kwa mwingine” amesisitiza Mhandisi Mwesigwa.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Watumiaji wa Bidhaa za Mawasiliano, kutoka Mamlaka ya Mamlaka ya Mawasiliano, Thadayo Ringo amesema huduma hii hapa nchini imeanza Machi Mosi mwaka huu na mpaka kufikia mwezi Juni 2017 takribani wananchi 15,000 walikuwa wameshaitumia huduma hii.

Aidha, Ringo ameongeza kuwa Tanzania ni nchi ya Tisa Barani Afrika kutoa huduma hii katika mawasiliano, ambapo amebainisha nchi nyigine zinazotoa huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila kubadili namba (MNP) kuwa ni Kenya, Rwanda, Botswana, Afrika ya Kusini, Ghana, Senegal, Namibia na Misri.


Huduma hii ya kuhama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani, inatolewa kwa watumiaji ambao namba zao zinatumika yaani hazijafungiwa au kusimamishwa kwa muda.
Mhandisi Mwandamizi wa Mawasiliano Mwesigwa Felician kutoka TCRA akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) Mjini Bariadi mkoani Simiyu wakati wa kikao kilicholenga kutoa Elimu kuhusu huduma ya kuhama kutoka Mtandao mmoja wa Simu kwenda Mtandao mwingine bila kubadili Namba ya Simu(Mobile Number Portability- MNP).
Baadhi ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Simiyu wakisikiliza Mhandisi Mwandamizi wa Mawasiliano Mwesigwa Felician kutoka TCRA(hayupo pichani) wakati wa kikao cha kutoa elimu kuhusu huduma ya kuhama kutoka Mtandao mmoja wa Simu kwenda Mtandao mwingine bila kubadili Namba ya Simu(Mobile Number Portability- MNP).
Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Watumiaji wa Bidhaa za Mawasiliano, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Thadayo Ringo akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bariadi mkoani Simiyu wakati wa kikao kilicholenga kutoa Elimu kuhusu huduma ya kuhama kutoka Mtandao mmoja wa Simu kwenda Mtandao mwingine bila kubadili Namba ya Simu(Mobile Number Portability- MNP).
Baadhi ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Simiyu wakisikiliza Mhandisi Mwandamizi wa Mawasiliano Mwesigwa Felician kutoka TCRA wakati wa kikao cha kutoa elimu kuhusu huduma ya kuhama kutoka Mtandao mmoja wa Simu kwenda Mtandao mwingine bila kubadili Namba ya Simu(Mobile Number Portability- MNP).Wednesday, September 20, 2017

WAKURUGENZI WA MIFUKO, MASHIRIKA WATEMBELEA MAENEO YA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA BIDHAA ZA HOSPITALI, MAJI TIBA SIMIYU

Baadhi ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika ya Serikali hapa nchini wametembelea na kukagua maeneo yanayokusudiwa kutumika  katika ujenzi wa kiwanda kikubwa  cha kutengeneza  bidhaa zinazotumika hospitalini zitokanazo na  zao la pamba na kiwanda cha maji tiba(drip) mkoani SIMIYU.

Maeneo yaliyotembelewa ni kijiji cha Nyamikoma  Halmashauri ya Wilaya Busega ,kijiji cha Isenga Halmashauri ya Wilaya Bariadi  na  Mtaa wa  Katenga Halmashauri ya  Mji wa Bariadi.

Akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania(TIRDO), Profesa Mkumbukwa Mtambo amesema kuanzishwa kwa viwanda hivyo kutasaidia kuokao fedha takribani shilingi bilioni 19 zinazotumika kununua maji tiba na shilingi bilioni 29 kununua bidhaa za hospitali zitokanazo na pamba kwa mwaka, ambavyo vyote kwa sasa vinanunuliwa nje ya nchi.

Profesa Mtambo ameongeza kuwa pamoja na kuokoa fedha viwanda hivyo vitatoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania 1600 na ajira nyingine 5000 hivyo vitachangia katika kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla.

Aidha, amefafanua kuwa upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivi vyote viwili utkaofanywa na TIRDO unatarajia kuanza wiki sita kuanzia sasa, hivyo akawaeleza viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuwa mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo watawasilisha taarifa itakayosaidia pia kuwaandaa wakulima kuzalisha pamba itakayohitajika kwa ajili kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa(MSD), Laurean Rugambwa amesema jumla ya lita 1,500,000 za maji tiba(drip) hutumika hapa nchini kwa mwaka, ambayo huagizwa nje ya nchi hivyo ameuhakikishia uongozi wa Mkoa kuwa bidhaa zitakazozalishwa katika viwanda hivyo zitapata soko la uhakika kwa kuwa zitanunuliwa na Bohari hiyo kwa ajili ya matumizi ya vituo mbalimbali vya kutolea huduma za Afya hapa nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Bernard Kaonga amesema wanaunga mkono ujenzi wa viwanda hivyo na wamekubali kuingia kwenye ubia na TIRDO pamoja na wadau wengine kama wadau wakubwa wa afya, kwa kuwa viwanda hivyo vitasaidia kupunguza gharama ya kuagiza  bidhaa hizo nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema ni vizuri Mkoa ukapata mapema taarifa ya Upembuzi yakinifu wa kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba ili kuendana na maandalizi ya msimu wa kilimo cha pamba, ambapo amesisitiza kuwa mkoa huo umejipanga kuongeza uzalishaji kutoka kilo milioni 70 mpaka kilo milioni 130 kwa mwaka 2018.  

Ameongeza kuwa viwanda hivi vitakuwa na manufaa makubwa kwa wanachi wa mkoa huo ikiwepo suala la ajira  kwa watu zaidi ya 6500 wanatarajiwa kuajiriwa katika kiwanda kitakachozalisha bidhaa za hospitali zitokanazo na zao la pamba.

“Kwa watu wa Simiyu kupata mradi utakaoajiri watu 1500 moja kwa moja, ajira nyingine 5000 pamoja na ajira za kwenye (ginneries) viwanda vyetu vya kuchambua pamba tutakuwa tumefanya kitu; ni lazima tutengeneze kura mpya za Mhe.Rais mwaka 2020, maana wapiga kura wengi wa mwaka 2020 watakuwa wapya ambao hitaji lao kubwa ni ajira na katika umri wetu huu ni lazima tujibu” amesema Mtaka.

Naye Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amesema Wakurugenzi wa Halmashauri, Madiwani, Viongozi wa Serikali za Vijiji na Mitaa na wananchi maeneo yote yaliyotembelewa wamekubali kutoa maeneo hayo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda, hivyo ni vema maamuzi ya mahali viwanda hivyo viwili vitakapojengwa yakatolewa mapema na wawekezaji hao ili  yaweze kuandaliwa  hati miliki.


Wabia wakuu katika Ujenzi wa Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha kutengeneza maji tiba(maji ya drip) Mkoani Simiyu ni pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF),Bohari ya Dawa(MSD),Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Shirika la Viwango nchini(TBS), Benki ya Maendeleo(TIB),Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF), NEMC,TEMDO na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania(TIRDO) ambao ndiyo wasimamizi wa Miradi hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa nne kushoto) akiwaongoza baadhi ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika pamoja na viongozi wa Mkoa huo katika ziara ya kutembelea na kuona maeneo yanayokusudiwa kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba pamoja na maji tiba Mkoani Simiyu.
Afisa Mipango Miji wa Halmasahuri ya Wilaya ya Busega. Yoram Salum (kushoto) akitoa taarifa ya eneo lililotengwa kwa ajili ya viwanda katika kijiji cha Nyashimo  wakati wa ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu waliyofanya  kwa lengo la kuona maeneo kinapoweza kujengwa kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha maji tiba Mkoani Simiyu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Ndg.Melkizedeck Humbe akitoa maelezo juu ya eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda  Mtaa wa Katenga  wakati wa ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la  kuona maeneo kinapoweza kujengwa kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Ndg.Abdallah Malela akitoa maelezo juu ya eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda katika Kijiji cha Isenge wakati wa ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanyakwa lengo la   kuona maeneo kinapoweza kujengwa kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika(baadhi hawapo pichani) katika majumuisho ya Ziara iliyofanyika katika Halmashauri ya Mji Bariadi, Halmashauri ya Wilaya Bariadi na Busega iliyofanyika kwa lengo la kuona maeneo ya kujenga  kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini  akizungumza na Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika na katika majumuisho ya Ziara iliyofanyika katika Halmashauri ya Mji Bariadi, Halmashauri ya Wilaya Bariadi na Busega iliyofanyika kwa lengo la kuona maeneo ya kujenga  kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda, Prof.Mkumbukwa Mtambo akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika majumuisho ya Ziara iliyofanyika katika Halmashauri ya Mji Bariadi, Halmashauri ya Wilaya Bariadi na Busega iliyofanyika kwa lengo la kuona maeneo ya kujenga  kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba mkoani Simiyu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Bernard Konga akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika majumuisho ya Ziara iliyofanyika katika Halmashauri ya Mji Bariadi, Halmashauri ya Wilaya Bariadi na Busega iliyofanyika kwa lengo la kuona maeneo ya kujenga  kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu walipotembelea kiwanda cha kuchakata pamba cha Alliance Ginneries kilichopo Kasoli wilayani Bariadi wakati wa ziara yao iliyofanyika kwa lengo la kuona maeneo ya kujenga  kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akitoa maelezo juu ya eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda katika Mtaa waKatengawakati wa ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa ya Taifa(MSD), Ndg Laurean Rugambwa akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi( WCF) Ndg .Masha Mshomba akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika pamoja na Viongozi wa mkoa wa Simiyu  wakipokea maelezo ya namna wanavyozalisha Mbegu za pamba kitaalam kutoka Mtaalam wa Kampuni ya Alliance Ginneries wakati walipotembelea kiwanda hicho baada ya kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akiwaonesha mbegu za pamba zilizoandaliwa kitaalam  na kiwanda  cha Alliance Ginneries Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika pamoja na Viongozi wa mkoa wa Simiyu (hawapo pichani) walipotembelea kiwanda hicho baada ya kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Mwakilishi kutoka Benki ya Maendeleo(TIB), Egata Makanja akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto), Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalishaji, Dkt. Gamitwe Mahaza(katikati)na Mkurugenzi Mkuu waTIRDO wakifurahia jambo wakati wa ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji Mkoani Simiyu.
Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika pamoja na Viongozi wa mkoa wa Simiyu  wakipokea maelezo ya namna wanavyozalisha dawa kutoka katika mti wa muorobaini inayotumika katika katika pamba hai (organic cotton) kutoka Mtaalam wa Kampuni ya Alliance Ginneries wakati walipotembelea kiwanda hicho baada ya kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Mwakilishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Moses Mbambe akichangia hoja katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Mwakilishi wa Shirika la Viwango nchini(TBS) akichangia hoja katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Msaidizi wa Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji katika Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Dkt.Gamitwe Mahaza(kushto) akichangia hoja katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu  wakifuatilia mjadala katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Mdau wa zao la pamba na mfanyabiasha Emmanuel Gungu Silanga akichangia hoja  kikao cha majumuisho ya ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu
Mwenyekiti wa Halmashauriya Mji Bariadi, Mhe.Robert Mgata akichangia hoja katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.
Diwani wa Kata ya Dutwa, Mhe.Mapolu Nunde Mkingwa kikao cha majumuisho ya ziara ya Wakurugenzi wa Mifuko na Mashirika waliyofanya kwa lengo la   kuona maeneo ya kujenga kiwanda cha bidhaa za Hospitali zitokanazo na pamba na kiwanda cha  maji tiba Mkoani Simiyu.

Thursday, September 14, 2017

BAADA YA KIWANDA CHA CHAKI SIMIYU YAJIPANGA TENA UPANUZI KIWANDA CHA MAZIWA, UJENZI WA KIWANDA CHA NYANYA NA PILIPILI

Baada ya mikakati ya upanuzi wa kiwanda cha kutengeneza chaki Wilayani Maswa, Mkoa wa Simiyu umejipanga tena kufanya upanuzi wa Kiwanda cha kusindika Maziwa kilichopo Wilayani Meatu na Ujenzi wa kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili wilayani Busega.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia zoezi la upembuzi yakinifu kwa viwanda hivyo lililofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa Ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP), kukamilika na taarifa yake kuwasilishwa kwa Viongozi na wadau wa Maendeleo Mkoani Simiyu katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.

Akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Wilayani Meatu, Profesa Lusato Kurwijila kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) amesema Tanzania inazalisha maziwa lita bilioni 2.1 kwa mwaka, lakini yanayopelekwa viwandani kusindikwa ni asilimia tatu ya maziwa yote, kutokana na ukosefu wa miundombinu ya kukusanyia maziwa.

Amesema upanuzi wa kiwanda cha Maziwa Meatu ni mradi unaotekelezeka hivyo ni vema ukafanyika uwekezaji katika ufugaji wa kisasa ili kupata maziwa ya kutosha, miundombinu ya  kukusanyia na kupozea maziwa,  kuwahamasisha wafugaji kuunda vyama vya ushirika ambavyo vitamiliki na kuendesha vituo vya kukusanyia maziwa na kutoa ajira kwa wananchi hususani vijana na wanawake.

Akizungumzia uanzishwaji wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, Mtaalam  wa Bustani  na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) Profesa Theodosy  Msogoya amesema, mradi huo unaweza kutekelezwa kwa mafanikio, hivyo ametoa wito kwa Serikali kuajiri watalaam wa Bustani na kuwahamasisha wakulima kujiunga katika vikundi ili waweze kukopesheka.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) Profesa Jeremia Makindara amesema, uwepo wa fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na utashi wa kisiasa,upatikanaji wa malighafi, nguvu kazi, maji, kiwanda kujengwa katika njia kuu ya usafirishaji (barabara ya Mwanza-Musoma), upatikanaji wa soko la uhakika kutasaidia kukiletea kiwanda hicho faida.

Kwa upande wao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya na Mkurugenzi wa Wilaya ya Meatu, Ndg. Fabian Manoza wamesema, viwanda hivyo vitakuwa vyanzo vipya vya mapato kwa Halmashauri zao na kuwasaidia wananchi kupata ajira na kukukuza uchumi wao.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa UNDP hapa nchini Ndg, Amoni Manyama ametoa wito kwa Serikali Mkoani Simiyu kuona namna ya kuwashirikisha wanufaika wa TASAF katika maendeleo ya viwanda na kuhakikisha kuwa makundi yote hususani wanawake yanashirikishwa na kunufaika na uanzishwaji wa viwanda hivyo.

 Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema watayafanyia kazi yote yaliyoanishwa katika Tafiti zilizofanywa na Watalaam hao kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA)na upembuzi yakinifu huo na kuyaweka katika matendo.

“Tumekuwa ni mkoa ambao tunawashirikisha wataalam kutoka katika vyuo vyetu, dhamira yetu ni kuona matokeo na position(Nafasi) yetu kama Mkoa ni kujipanga  kimkakati na mpango kazi wetu, dira ya mkoa na tunasema  kwenye miaka mitatu tutatekeleza” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema Serikali Mkoani humo iko tayari kushirikiana na sekta binafsi katika uwekezaji, hivyo ametoa wito kwa Watanzania walio tayari kuwekeza Mkoani humo kwa kushirikiana na Halmashauri ambazo zimeanzisha miradi hiyo ya viwanda.

Sambamba na hilo amezishukuru Taasisi za Fedha zilizo tayari kufanya kazi na Mkoa wa Simiyu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwepo mradi wa kilimo cha Umwagiliaji wilayani Busega hususani Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) ambayo imesema iko tayari kufanya kazi na Mkoa huo, katika miradi mbalimbali ya Kilimo.

Upembuzi yakinifu wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyanya na pilipili wilayani Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu uliofanywa na Wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii(ESRF) ulianza kufanyika Mwezi Julai mwaka huu na kukamilika mapema mwezi Septemba.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akizungumza na Viongozi na wadau wa maendeleo mkoani humo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini Ndg.Amoni Manyama (kushoto) akizungumza na Viongozi na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) uliofadhili na shirika hilo.
Mtaalam wa Maziwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA), Profesa Lusato Kurwijila akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Mtaalam wa Uchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Mutahyoba Baisi akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Mtaalam  wa Kilimo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) Profesa Theodosy T. Msogoya akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Mhandisi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) Profesa  Benard  Chove akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi wa Vipind na uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba(kulia) akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mhe.Festo Kiswaga.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA), Dkt. Jeremia Makindara akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu , Mhe.Dkt.Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndg.Fabian Manoza akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkuu wa Wilaya ya Busega  Mhe.Tano Mwera akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi wa FURSA, Suma Mwaitenda akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buseg, Ndg.Anderson  Njiginya akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya yaItilima, Ndg.Mariano Mwanyigu akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Baadhi ya viongozi na wadau wa maendeleo Mkoani Simiyu wakifuatilia taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), iliyowasilishwa katika kikao maalum Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wadau wa maendeleo Mkoani Simiyu wakifuatilia taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), iliyowasilishwa katika kikao maalum Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wadau wa maendeleo Mkoani Simiyu wakifuatilia taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), iliyowasilishwa katika kikao maalum Mjini Bariadi.
 Meneja wa Kitengo cha Kukuza Biashara kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB)  akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilishwa kwa  taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Wataalam  kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) wakifuatilia mjadala wa viongozi na wadau wa maendeleo Mkoani Simiyu, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi baada ya kuwasilishwa kwa  taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nickson Simon kutoka FURSA akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Daktari wa Mifugo wa Halmashuri ya Wilaya ya Itilima Faustine Musoke akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Ndg.Hassan Ngoma kutoka FURSA akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!