Tuesday, June 25, 2019

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 30 KUSHINDANIWA SIMIYU JAMBO FESTIVAL 2019


Tamasha kubwa la michezo ambalo hufanyika kila mwaka Mkoani Simiyu (Simiyu Jambo Festival) linatarajiwa kufanyika Juni 30, mwaka huu katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi huku takribani shilingi milioni 32 zikishindaniwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 25, Mratibu wa tamasha hilo Bi. Zena Mchujuko amesema Mgeni rasmi katika Tamasha hili anatarajiwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.

Amesema katika Tamasha hilo kutafanyika mashindano ya mbio za baiskeli wanaume na wanawake, mbio fupi kilometa tano wanaume na wanawake na mashindano ya mdahalo kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

“Jumla ya shilingi milioni 32 zitashindaniwa kwa michezo yote,  mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kwa wanaume atapata 1,000,000, Wanawake  700, 000, walemavu 500, 000 na tutatoa zawadi mpaka kwa mshindi wa 25;  ngoma za asili mshindi atapata 1,000,000” alisema Bi. Zena

Aidha, amesema fomu za ushiriki zinapatikana kataika ofisi ya Chama cha Baiskeli Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi na katika Tovuti: www.simiyutalent.co.tz kwa gharama za shilingi elfu tano(5000) kwa mashindano ya baiskeli na shilingi elfu mbili (2000) kwa ajili ya mashindano ya mbio fupi.

Katika hatua nyingine Bi. Mchujuko amesema kupitia Tamasha la Simiyu Jambo Festival jamii ya watu wa Simiyu itapata ujumbe wa kupinga mimba za utotoni jambo litakalopelekea watoto wa kike waweze kutimiza ndoto zao kupitia Kauli Mbiu ya Tamasha ambayo ni :-WEZESHA MTOTO WA KIKE ATIMIZE NDOTO ZAKE, INAWEZEKANA KUZUIA MIMBA KATIKA UMRI MDOGO”

Mratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu Duniani(UNFPA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Amir Batenga amesema shirika hilo limekuwa likishirikiana na Serikali katika jitihada za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, ambapo waathirika wakubwa ni wasichana wenye umri mdogo, hivyo anaamini kupitia Tamasha hilo wananchi watapata ujumbe mahususi wa kukabiliana na mimba katika umri mdogo.

Naye Katibu wa Chama cha Mbio za Baiskeli Mkoa wa Simiyu, Bw, Samwel Richard washiriki takribani 260 kutoka mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mara, Mwanza, Geita na Kagera wanatarajia kushirikia mashindano ya baiskeli, huku akiwahakikishia wananchi kuwa wachezaji wao wamejiandaa vizuri na wamekuwa kambi kwa takribani wiki mbili.

Kwa upande wake Kiongozi wa Ngoma za Asili Mkoa wa Simiyu, Bw. Buhimila Shala amesema kupitia ngoma za wagika na wagalu watatoa ujumbe uliobebwa na Kauli mbiu ya Tamasha kwa lengo la kuwaokoa wasichana kupata mimba katika umri mdogo.

Tamasha la Simiyu Festival mwaka 2019 limedhaminiwa na Jambo Food Products Company, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani-UNFPA, NGM Gold Mine Limited, NGS Petroleum, Alliance Ginneries Limited, Busega Mazao Limited, Maswa Standard Chalk, Ms Hotel na Vetreces Company Limited.
MWISHO
Mratibu wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival Bi. Zena Mchujuko(kulia) akizungumza na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu Duniani(UNFPA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Amir Batenga(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya namna Shirika hilo liakavyotumia Tamasha la Simiyu Jambo Festival kupeleka ujumbe wa Kupinga mimba za utotoni  tamasha ambalo linatarajiwa kufanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Kiongozi wa Ngoma za Asili, Bw. Buhimila Shala (kushoto) akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari   na kueleza namna ngoma za asili zitakavyopamba Tamasha la Simyu Jambo Festival ambalo linatarajiwa kufanyika Juni 30, 2019.
Katibu wa Chama cha Baiskeli Mkoa wa Simiyu, Bw. Samwel Richard(kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya namna chama hicho kilivyojiandaa na mashindano ya baiskeli katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival, linalotarajiwa kufanyika Juni 30, 2019

Monday, June 24, 2019

RC MTAKA AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI SIMIYU KUISAIDIA, KUILEA SEKTA BINAFSI


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi wa Serikali mkoani Simiyu kuisaidia na kuilea Sekta Binafsi ili iendelee kukua na wahakikishe kuwa maamuzi wanayofanya hayawi vikwazo  katika mazingira ya biashara na uwekezaji.


Mtaka ameyasema hayo wakati akifungua Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu ambayo imefanyika mjini Bariadi.

Amesema viongozi wa Serikali mkoani humo wanapofanya maamuzi katika biashara za watu ni lazima wawe na nia ya dhati ya kuona sekta binafsi inakuwa, ili maamuzi ya viongozi hao yasiwe vikwazo kwa ukuaji wa Sekta binafsi na mazingira ya biashara na uwekezaji.

“Sekta binafsi ni lazima ilelewe anaeilea ni Serikali, Sekta binafsi ni lazima ilindwe anayeilinda ni Serikali,Sekta binafsi ni lazima isimamiwe anayeisimamia ni Serikali na Serikali inaisimamia kwa maana ya kuilea ili ifanye vizuri” alisema Mtaka.

Aidha, ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya mkoani Simiyu kuendeleza utaratibu wa kukutana na wafanyabishara ili kupata nafasi ya kujadiliana juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji na namna ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, huku akisisitiza pia kuendelea kufanyika kwa mabaraza ya biashara ya wilaya.

Katibu wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA) Mkoa wa Simiyu, Bi. Christina Matulanya amesema ili kuboresha mazingira ya biashara Serikali inapaswa kuendelea kuvutia wawekezaji  na kusimamia sheria, sera na kanuni zisipindishwe, huku akiupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuandaa mwongozo wa uwekezaji.

Katika hatua nyingine Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Charles Mkumbwa  ametoa wito kwa wafanyabiashara kuwa wazalendo, kutoa risiti ipasavyo, kufuata sheria za kodi na akaahidi kuwapa ushirikiano wafanyabiashara kila wanapohitaji.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule ya biashara,  Khalidi Swabiri ambaye alikuwa mwezeshaji wa warsha hii amesema ni vema mabaraza ya biashara ya wilaya yakafanyika ili wafanyabiashara wapate muda wa kukutana na viongozi wa Serikali, sekta binafsi kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika mazingira ya biashara na uwekezaji na ufumbuzi wake.

Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA), Dkt. Meshack Kulwa  amesema pamoja na kuomba mabaraza ya biashara ya wilaya yafanye kazi, ameomba  TCCIA mkoani Simiyu itafute viongozi watakaofanya kazi kwa kujituma ili TCCIA Simiyu iweze kuwa imara.
MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na watendaji wa Serikali na Sekta binafsi katika Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu ambayo imefanyika mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Bodi ya Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA), Dkt. Meshack Kulwa akifafanua jambo katika Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali na sekta binafsi wakifuatilia Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali na sekta binafsi wakifuatilia Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Bariadi.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule ya biashara, Khalidi Swabiri (mwezeshaji)  akitoa  mada  katika Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu, iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mjini Bariadi.


Meneja wa Mamlaka ya Mapato(TRA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Charles Mkumbwa  akifafanua jambo katika Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Bariadi.
 Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi akichangia hoja katika Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Bariadi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule ya biashara,  Khalidi Swabiri (mwezeshaji)  akitoa  mada  katika Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu, iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali na sekta binafsi wakifuatilia Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Bariadi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule ya biashara,  Khalidi Swabiri (mwezeshaji)  akitoa  mada  katika Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu, iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mjini Bariadi.


Baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali na sekta binafsi Mkoani Simiyu wakifuatilia Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali na sekta binafsi wakifuatilia Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali na sekta binafsi wakifuatilia Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Bariadi.

Friday, June 21, 2019

TFDA YAFUNGUA OFISI YA KANDA MPYA YA ZIWA MASHARIKI SIMIYU


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imefungua rasmi Ofisi ya Kanda mpya ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambapo makao makuu ya kanda hiyo yatakuwa Mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama amesema mamlaka hiyo imeanzisha Kanda Mpya ya Ziwa Mashariki inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ili kusogeza huduma kwa wananchi na kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Amesema ofisi hii itajishughulisha na usajili wa maeneo yanayo jihusisha na uzalishaji na uuzaji wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba, kupokea maombi ya usajili wa bidhaa za vyakula vinavyofungashwa, kufanya ukaguzi wa bidhaa za vyakula katika soko kuwalinda walaji na  kudhibiti usindikaji wa chakula dawa na vipodozi.

Kazi nyingine zitakazofanywa na kanda hii ni kutoa vibali vya uingizaji nchini na usafirishaji wa chakula nje ya nchi, kufanya ufuatiliaji wa bidhaa za vyakula katika soko, kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa, vipodozi na vifaa tiba pamoja na kuelimisha na kutoa taarifa kwa wadau na wananchi kwa ujumla kuhusu bidhaa zinazothibitiwa na mamlaka.

Aidha, Mwasulama amesema Ofisi ya kanda hii itatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ambapo wataalam waliopo kwenye wilaya, manispaa, miji na majiji watasimamia sheria ya chakula na dawa kwa mujibu wa kanuni ya kukasimu baadhi ya majukumu na madaraka ya TFDA katika  Halmashauri.

Akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa wa Simiyu na TFDA katika ufunguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema Taasisi nyingine zinazohitajika katika uwekezaji wa viwanda na maeneo mengine ya uwekezaji zikaiga mfano wa TFDA  kwa kusogeza huduma karibu na wananchi ili waweze kupata huduma kwa wakati.

“Hiki kilichofanywa na TFDA ni vizuri taasisi nyingine nazo ziige, kama leo TFDA ipo Simiyu kama Kanda ya Ziwa Mashariki ningetamani kuwaona TBS, NEMC, OSHA wako Simiyu kama Kanda ya Ziwa Mashariki na Taasisi zote ambazo kwenye uwekezaji wa viwanda na maeneo mengine ya uwekezaji zinakuwa karibu na maeneo ya kutolea huduma” alisisitiza Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaotekeleza majukumu waliyokasimiwa na TFDA kufanya majukumu hayo kwa mujibu sheria huku akiwaasa  kuacha tabia ya kufungia biashara za wananchi bila kuwaelimisha badala yake wawasaidie kuwapa elimu ili wazalishe bidhaa bora kwa walaji.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Dkt. Mike Mabimbi akizungumza kwa niaba ya waganga wakuu wa wilaya ambao ni Makatibu wa kamati za ukaguzi wa chakula na dawa amesema watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa majukumu wanayokasimiwa  na TFDA na akashukuru TFDA kusogeza huduma karibu na wananchi.
MWISHO


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa huo Mamlaka ya Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.


Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama akitoa taarifa fupi ya uanzishwaji wa  Kanda hiyo itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, katika uzinduzi waa kanda hiyo  uliofanyika  Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.


Baadhi ya wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) wakifuatilia masuala mbalimbali ambayo yaliyokuwa yanaendelea katika Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.


Baadhi ya viongozi,  wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) wakifuatilia masuala mbalimbali ambayo yaliyokuwa yanaendelea katika Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimueleza jambo Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama mara baada ya kuzindua rasmi Kanda ya Ziwa Mashariki ya  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga, Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.

Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa, Dkt. Mugune Maeka akitoa neno la shukrani  mra baada ya kuhitishwa kwa uzinduzi wa Kanda ya Ziwa Mashariki ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga, Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati mbele) akiwa katika picha ya pamoja  na baadhi ya viongozi,  wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) mara baada ya  Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa huo Mamlaka ya Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa huo Mamlaka ya Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama akitoa taarifa fupi ya uanzishwaji wa  Kanda hiyo itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, katika uzinduzi waa kanda hiyo  uliofanyika  Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.

Wednesday, June 19, 2019

UKAGUZI WA KINGA, TAHADHARI YA MOTO UFANYIKE KWENYE SHULE ZA BWENI KUEPUSHA MAJANGA: KAMISHNA JENERALI ANDENGENYE

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kuendelea kufanya ukaguzi wa kinga na  tahadhari  ya moto kwa  shule zote za mabweni nchini kujiridhisha ikiwa zimezingatia ushauri wa kitaalam katika ujenzi wa majengo, kwa lengo la kuepusha majanga ya moto yanayogharimu maisha ya watu na mali.

Andengenye ametoa maagizo hayo Juni 19, 2019 Mkoani Simiyu wakati akizungumza  na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi katika shule ya sekondari Simiyu, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Akizungumza na wanafunzi Kamishina Jenerali Thobias Andengenye amesema kumekuwa na matukio ya moto katika shule kadhaa za bweni ambayo yameleta athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo kwa wanafunzi, kuteketea kwa  mali, hivyo jeshi la zimamoto na uokoaji linaendelea kuweka mikakati ya kukabiliana na majanga hayo.

Amesema mikakati hiyo ni pamoja na kusogeza huduma za zimamoto karibu na wananchi kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya moto katika majengo, kusoma ramani za majengo na kuanzisha klabu za zimamoto katika shule, ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujua vitu vya kufanya na vya kuepuka na uwezo wa kukabili moto katika hatua za awali na kuuzima.

Katika hatua nyingine Andengenye amewataka wamiliki wa shule kuzingatia ushauri wa kitaalam unaotolewa na wataalam wakati wa ukaguzi juu ya namna ya kufanya mabweni , madarasa na ofisi ziwe salama kwa kuwasilisha michoro ya majengo  hayo katika Ofisi za Zimamoto ili  ushauri wa kitaalam uweze kutolewa.

“Niwaombe wanaomiliki shule wazingatie ushauri wa kitaalam unaotolewa, wazingatie ujenzi unaofuata ushauri wa kitaalaam  kwa kuwasilisha michoro kama wanataka kujenga mabweni, kuongeza madarasa au kuongeza vyumba vya ofisi basi wazingatie ushauri ili majengo yanayojengwa yawe salama zaidi” alisema.

Aidha, amewaasa wananchi kuacha kuweka mitungi ya gesi ndani na kutikisa mitungi ya gesi kama njia ya kufahamu kiasi cha gesi kilichopo; kwa kuwa kunaweza kusababisha moto na kushauri kuwa njia sahihi ya kupima kiasi cha gesi katika mtungi ni kuweka mtungi katika maji, ambapo baada ya kuutoa sehemu isiyo na gesi itaonekana kuwa kavu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa watu kutumia gesi, hivyo ameshauri Jeshi la Zimamoto na uokoaji kuendelea kutoa elimu katika mikusanyiko ya watu na kupitia vyombo vya habari kuhusu dhana ya matumizi sahihi ya gesi ili kuepusha majanga  ya moto.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amelishukuru Jeshi la Zimamoto na uokoaji kutoa elimu kwa wanafunzi na akawataka wanafunzi wote waliopata elimu hiyo kuwa mabalozi katika maeneo yao wanayoishi.

Magreth Sonda mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Simiyu ameshukuru kupata elimu ya tahadhari na kinga dhidi ya moto na kuahidi kuwa yeye pamoja wanafunzi wenzake watakuwa mabalozi wa kueneza elimu hiyo kwa jamii inayowazunguka ili kuepusha majanga ya moto ambayo yana athari nyingi ikiwemo vifo na kuteketea kwa mali.
MWISHO

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye akiweka kizimia moto katika moja ya vyumba vya madarasa katika shule inayotarajiwa kuwa shule ya wanafunzi wenye vipaji vya michezo Simiyu Sekondari, wakati wa ziara yake Mjini Bariadi Mkoani Simiyu, Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akimtambulisha Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi kabla ya kuzungumza nao juu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Juni 19, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiwasha moto kwa ajili ya kuwaonesha wananchi namna ya kuzima moto pindi moto unapotokea, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Juni 19, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye kukagua moja ya mabweni yanayojengwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu, wakati alipotembelea shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye kukagua moja ya mabweni yanayojengwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu, wakati alipotembelea shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Askari wa jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu, akimuelekeza mmoja wa wanafunzi namna ya kuzima moto wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye katika shule ya Sekondari Simiyu, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani hapa Juni 19, 2019.
Askari wa jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu, akimuelekeza mmoja wa wanafunzi namna ya kuzima moto wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye katika shule ya Sekondari Simiyu, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye tai) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye madarasa kuona namna yalivyojengwa na namna vizimia moto vinayoweza kuwekwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu, wakati alipotembelea shule hiyo akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu, Maulo Kigahe wakishangilia mara baada  Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye kufunga kizimia moto kilichopo kushoto, katika moja ya madarasa katika Shule ya Sekondari Simiyu, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye tai) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye madarasa kuona namna yalivyojengwa na namna vizimia moto vinayoweza kuwekwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu, wakati alipotembelea shule hiyo akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, wakati alipofika mkoani hapa kufanya ziara Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye, alipotembelea shule ya sekondari Simiyu, akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye, alipotembelea shule ya sekondari Simiyu, akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye, alipotembelea shule ya sekondari Simiyu, akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.


TUZO YA SERENGETI HIFADHI BORA AFRIKA YATAMBULISHWA KWA WANANCHI SIMIYU NA MARA


Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika imetambulishwa rasmi kwa wananchi wa mikoa ya Simiyu na Mara kutoka katika maeneo yanayoizunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Akiitambulisha tuzo hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla Juni 18, 2019 katika Kijiji cha Robanda wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, amesema tuzo hii iwe chachu kwa wahifadhi, viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kuimarisha shughuli za uhifadhi hapa nchini.

“Tuzo tuliyoipata ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika iwe chachu ya kutufanya tuendelee kuitangaza zaidi Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili tuweze kushinda tuzo ya Kimataifa; Tuzo hii iwe chachu kwetu wahifadhi, viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kuimarisha shughuli za uhifadhi hapa nchini” alisema Kigwangalla.

Ameongeza kuwa Sekta ya uhifadhi ina faida kubwa zaidi ya utalii ambazo ni pamoja na kutoa hewa ya oksjeni kutoka kwenye misitu, kukamilisha mzunguko wa mvua, kutoa mahali pa wanyamapori kuishi na kusaidia zoezi la uchavushaji kwa mimea unaopelekea kuwepo chakula, hivyo shughuli za uhifadhi ziimarishwe zaidi kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA kwa kazi kubwa ya uhifadhi wanayoifanya jambo ambalo limeifanya Mamlaka hiyo kutoa msaada kwa jamii, ambapo alibainisha kuwa TANAPA imechangia jumla ya shilingi milioni 100 katika ujenzi wa shule ya sekondari Simiyu maalum kwa ajili ya michezo.

Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu ni wadau wakubwa wa uhifadhi na unaunga mkono juhuda zote za uhifadhi zinazofanywa na wizara na wadau mbalimbali wa uhifadhi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima amepongeza Kamati za Ulinzi na Usalama ya Mikoa ya Simiyu na Mara kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha kuwa zinapambana na uharibifu wowote katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti hali iliyochangia hifadhi hii kuonekana bora zaidi katika Bara la Afrika.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye pia ni mhifadhi amesema tuzo hiyo I matunda ya juhudi za Serikali na wananchi katika kukomesha ujangili na uwindaji haramu na kupitia tuzo hii itachochea watalii wengi kuingia nchini.

Naye Shawezi Silas mkazi wa Kata ya Ikoma wilaya ya Serengeti amesema tuzo hiyo wananchi wameipokea kwa furaha kubwa sana  na imewasaidia kuilewa maana ya uhifadhi na umuhimu wa kuzilinda rasilimali za Taifa ikiwemo wanyamapori.
 MWISHO
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katiakati), Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka(wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adama Malima wakiwaonesha wananchi Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika, katika halfa ya kuitambulisha tuzo hiyo, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
 Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adama Malima, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka, Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Bi. Karoline Mthapula na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (aliyesimiama mwenye miwani), wakiangalia tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika, mara baada ya kuhitishwa kwa hafla ya kuitambulisha tuzo hiyo kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adama Malima, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka, wakiteta jambo mara baada hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika, , iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za mkoa wakati wa hafla ya kuitambulisha kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akitoa salamu za mkoa wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.

Baadhi ya viongozi akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakicheza ngoma na kikundi cha burudani kutoka mkoani Mara, wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Mtaalamu kutoka TANAPA akitoa taarifa ya namna tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika ilivyopatikana, wakati wa hafla ya kuitambulisha tuzo hiyo kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe, Pius Machungwa akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wenzake wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simyu, Bw. Adili Elinipenda, mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Robanda kwa ajili ya Kuongoza Hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa mara baada ya kuwasilisha salamu wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kushoto) wakifurahi mara baada ya kupokea zawadi ya Ng’ombe dume ambayo imetolewa na wananchi wa Robanda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha rasilimali za nchi zinasimamiwa na kulindwa, wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019


Baadhi ya wananchi wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019

Baadhi ya viongozi akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakicheza ngoma na kikundi cha burudani kutoka mkoani Mara, wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi  wakati wa hafla ya kuitambulisha kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!