Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga amesema Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Agosti 8, 2019 ,anatarajiwa
kuzindua kanzi data ya usajili wa wakulima kupitia mazao nane ya kimkakati, itakayosaidia
kujua idadi ya wakulima sambamba na wakulima kujua takwimu za mazao na
upatikanaji wa masoko kwa urahisi kupitia njia ya mtandao .
Mhe. Hasunga ameyasema hayo Julai 30, 2019 wkati akikagua
maendeleo ya maandalizi ya maonesho ya Nanenane Kitaifa Mkoani Simiyu, ambapo
amesema pamoja na kuzindua kanzi data ya wakulima Mhe. Rais Magufuli
anatarajiwa pia kuzindua mfumo wa kielectroniki utakaosaidia kujua idadi ya
wakulima, mahali walipo,mazao wanayolima na ukubwa wa maeneo wanayolima.
“Tunataka kili Mtanzania popote alipo akitaka takwimu sahihi awe
anaweza kuingia kwenye mfumo na akaziona,
ukitaka wakulima wa pamba wa pamba waonekane, tukakitaka wakulima wa
mkonge waonekane, tunataka tuwe na uwezo wa kuwaona wakulima wakubwa, wa kati
na wadogo na mahali walipo” alisema Mhe. Hasunga.
Pamoja na hayo ameongeza kuwa tarehe hiyo pia Rais Dkt
Magufuli atafungua soko la bidhaa ambalo litawawezesha wakulima kuuza
mazao yao nje ya nchi ambayo itasaidia kupata uhakika wa bei na kuepuka
madalali na kuleta uwazi ili kila mkulima /mdau yoyote aweze kuona na
kujua bei sambamba na kufahamiana .
Waziri Hasunga amesema kwa upande wa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan , wakati akizindua
maonesho ya nane nane Agosti Mosi, 2019, anatarajiwa kuzungumzia masuala
ya mazinigira ambapo atazindua mkakati wa kuthibiti upotevu wa mazao
utakao wezesha kujua hasara anazozipata mkulima hatua itakayopelekea
kukabiliana nazo kwa wakati.
Aidha waziri Hasunga ameongeza kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa atazindua bima ya mazao ambayo
itasaidia kukabiliana na vihatarishi vya mazao mfano ukame na mafuriko sambamba
na kuona maendeleo ya ushirika nchini na nafasi ya ushirika na namna ambavyo
unawaunganisha wakulima ,wafugaji na wavuvi.
Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amemtembelea mmoja wa wajasiriamali
kutoka wilaya ya Meatu Deke Ndabuli Maige anayetengeneza mashine za kupukuchua
mahindi ambapo mjasiriamali hiyo amesema kuwa alianza kutengeneza mashine hizo
tangu mwaka 2014 na hadi sasa ameshatengeneza mashine 10 na tayari
ameshauza mashine 7.
Pamoja na hayo ameongeza kuwa mashine hizo zinauwezo wa
kupukuchua magunia 150 kwa siku huku akitumia lita saba za mafuta ya kuendeshea
mashine hiyo kwa siku.
MWISHO
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akipokea
maelezo juu ya teknolojia rahisi ya upandaji wa mazao ya mbogamboga katika
Vipando vya Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, wakati wa ziara yake ya kujionea
maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda
ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akipokea
maelezo juu matumizi ya zana za kisasa za kilimo katika Banda la Jeshi la
kujenga Taifa(JKT), wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya
Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja
vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(kushoto), kuhusu jengo la
Maonesho la Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa
Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga (aliyeyoosha mkono)akiangalia mbegu
ya ulezi, wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho
ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya
Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga (mbele)akiangalia vipando vya
nyanya vya Jeshi la kujenga Taifa(JKT), wakati wa ziara yake ya kujionea
maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda
ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph
Chilongani(kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(mwenye
suti) juu ya mashine iliyotengnezwa na mjasiriamali Deke Ndabuli Maige kutoka Meatu(wa pili
kushoto)yenye uwezo wa kupukuchua gunia 150 kwa siku.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha
akimuonesha jambo Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga (wa pili kushoto) wakati
wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa
yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu.
Baadhi ya wananchi wakipewa elimu juu ya namna
ya kutambua noti bandia katika banda la Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ikiwa ni
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa
yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu.
Moja ya zana za kisasa zinazopaswa kutumiwa na
wakulima ili kuongeza tija ya uzalishaji zilizopo katika Banda la Jeshi la
kujenga Taifa(JKT), litakalooneshwa katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa
yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu..
Viatu vya ngozi vilivyotenegenezwa na Shirika
la Uzalishaji Mali la SUMA JKT, ambavyo vitapatikana Maonesho ya Nanenane Kitaifa
yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu
Mtaalam wa JKT (kulia) akitoa maelezo juu ya
namna ya kufuga asmaki kwenye matanki kwa Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga
(wa nne kulia) katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda
ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu
Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga
akiangalia asali inayotoka mkoani Mra,
mara baada ya kutembelea mabanda ya mkoa wa Mara, wakati wa ziara yake ya kujionea
maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda
ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Baadhi ya mabanda ya maonesho yakiwa
yamekamilika ikiwa ni hatua za mwisho za maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa
yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu.
Kitalu nyumba cha Halmashauri ya Manispaa ya
Musoma
Baadhi ya bidhaa za JKT zinazouzwa kwenye
banda lao katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa
Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga akipewa maelezo kuhusu mbegu za zao
la mtama, wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho
ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya
Nyakabindi mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Japhet Hasunga akiangalia
zao la mbogamboga aina ya kabichi katika vipando cya jeshi la Magereza, wakati
wa ziara yake ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa
yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu.