Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa
Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yatakayofanyika Kanda ya Ziwa
Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi Mjini Bariadi kuanzia tarehe 29/07/2019
hadi 08/08/2019.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalum wa kutoa taarifa kwa
Umma uliofanyika Mjini Bariadi, Julai
24, 2019.
Mtaka amesema Mhe Makamu wa Rais atafungua rasmi maonesho
hayo Agosti Mosi, 2019 na waoneshaji mbalimbali zikiwemo Taasisi, Mashirika
mbalimbali na wajasiriamali wataanza kuonesha teknolojia, huduma na bidhaa zao
Julai 29, 2019 ikiwa ni maandalizi ya ufunguzi rasmi utakaofanywa na Mhe.
Makamu wa Rais.
“Shughuli ya ufunguzi itafanywa tarehe 01/08/2019 na
Mhe. Makamu wa Rai, haya ni maonesho ambayo yatakaribisha viongozi wa Kitaifa,
Agosti 03, 2019 tutakuwa na Mhe. Waziri Mkuu, Agosti 06, 2019 tutakuwa na
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na Kilele tunatarajia kuwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli” alisema.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba amesema ameridhishwa
na maandalizi ya Maonesho ya nanenane yanayoendelea mkoani Simiyu na kutoa wito
kwa wakulima na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
maonesho haya ili kuja kujionea teknolojia mbalimbali zitakazojibu changamoto
za wakulima, wafugaji na wavuvi.
Aidha, Mhe. Mgumba ametoa wito kwa waoneshaji kuwa
wabunifu katika teknolojia, huduma na bidhaa watakazoonesha ili maonesho haya
yawe chachu ya kuwasaidia wakulima,
wavuvi na wafugaji kuongeza tija katika
uzalishaji
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima amesema matarajio ya mikoa ya Simiyu,
Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Ziwa Mashariki ni kuwa na maonesho ya
tofauti na mwaka jana, lengo likiwa ni kuifanya kanda hiyo kuwa ni mahali pa
kudumu pa wakulima, wafugaji na wavuvi kuwa na maonesho ya kilimo biashara.
Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanafanyika kwa mara ya
pili sasa mkoani Simiyu tangu Kanda ya Ziwa ilipogawanywa katika kanda mbili
yaani, Kanda ya Ziwa Mashariki(Simiyu, Mara na Shinyanga) na Kanda ya Ziwa
Magharibi(Mwanza, Geita na Kagera) ambapo mwaka huu yanaadhimishwa chini ya
kauli Mbiu:-“KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KATIKA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI”
MWISHO
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba (kulia) akikagua moja ya kitalu nyumba wakati wa ziara ya
kukagua maandalizi ya Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019
Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mtaalam kutoka JKT
(kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (katikati)
wakati akikagua moja ya tanki la ufugaji wa samaki wakati wa ziara ya kukagua
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya
Nyakabindi Bariadi.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba (kulia) akikagua baadhi ya vipando wakati wa ziara ya kukagua
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya
Nyakabindi Bariadi.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba (kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Afisa wa JKT akikagua
baadhi ya vipando wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika
kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya
Nyakabindi Bariadi.
Baadhi ya vipando vilivyo
katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane
Kanda ya Ziwa Mashariki vilivyopandwa kwa ajili ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 .
Mtaalam kutoka JKT
(kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (katikati)
wakati akikagua moja ya Bwawa la ufugaji wa samaki wakati wa ziara ya kukagua
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya
Nyakabindi Bariadi.
Mtaalam kutoka JKT
(kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba wakati
akikagua moja ya tanki la ufugaji wa samaki wakati wa ziara ya kukagua
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya
Nyakabindi Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Mhe. Adam Kighoma Malima(kulia) akizungumza katika kikao cha Kamati ya
maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki,
kilichofanyika Julai 23, 2019 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi, (kushoto)
ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Moja
ya vipando vya mazao ya kilimo katika
viwanja vya Nanenane Nyakabindi
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba (kushoto) akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Mkoa wa
Simiyu na Wizara ya Kilimo wakati akikagua ujenzi wa majego ya kudumu katika
VIwanja wa Nananenane Nyakabindi Bariadi
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba akikagua vipando vya mazao ya iilimo katika viwanja vya
Nanenane Nyakabindi, Julai 25, 2019.
Naibu Waziri wa Kilimo,
Mhe. Omary Mgumba akikagua vipando vya mazao ya iilimo katika viwanja vya
Nanenane Nyakabindi, Julai 25, 2019.
0 comments:
Post a Comment