Waziri wa
nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman
Jafo ametoa agizo kuwa ifikapo Julai 30, 2019 hospitali zote za wilaya zinazojengwa nchini
ziwe zimekamilika .
Jafo
ameyasema hayo akiwa kwenye ziara ya siku moja mkoani Simiyu
ambapo alitembelea miradi mbalimbali ukiwemo wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Itilima,. ujenzi wa
barabara ,ujenzi wa kiwanda cha chaki na ujenzi wa kituo cha
mabasi(stendi) cha kisasa, huku akipongeza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya
Itilima kwa kizingatia viwango, mahitaji na ubora katika ujenzi.
Aidha
amesema kuwa hakuna sababu za fedha kuongezwa kiasi kilichotolewa awali kwa ajili
ya ujenzi wa majengo saba ya awali kinatosha kukamilisha huku akitolea mifano
ya hospitali ambazo zimeshakamilika kwa kiasi hicho kilichotolewa awali.
Akiwa
wilaya za Meatu na Maswa waziri Jafo amekagua na kuridhishwa na ujenzi wa
barabara zilizojengwa na mkandarasi CHICO kwa kiwango cha lami ikiwa ni utekelezaji
wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe
Magufuli aliyoitoa akiwa ziarani mkoani hapo zenye urefu wa kilometa tatu(
kilometa moja na nusu kwa kila wilaya)
“Nikupongeze
sana mratibu wa TARURA Mhandisi Dkt Philimon Msomba kwa kazi hii nzuri
kikubwa wananchi muutunze mradi huu
,kwanza nimefarijika sana kukuta hadi taa za barabarani zipo hongereni sana
”alisema waziri Jafo.
Kwa upande
wake Mbunge wa Maswa Mashariki ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe.Stanslaus
Nyongo amemuomba Waziri Jafo kabla mkandarasi hajaondoa vifaa vyake eneo la
ujenzi wa barabara ni bora ukafanyika mchakato wa kuongeza kiasi kingine cha
pesa kwa ajili ya kilometa 1.5 zilizobaki.
Katika
hatua nyingine akiwa Mjini Bariadi Waziri Jafo ameridhishwa na ujenzi wa kituo
cha mabasi kinajengwa Mjini hapo na kumtaka mkandarasi Kampuni ya Halem and
Kings Builders Co Ltd kutoka Dar es salaam kukamilisha ujenzi ifikapo Septemba 2, 2019 ambapo kwa sasa
umefikia asilimia 87 na mpaka kukamilika kwake ujenzi utagharimu kiasi
cha shilingi bilioni 7.2
Pamoja na
hayo waziri Jafo alitembelea ujenzi wa kiwanda cha chaki na kiwanda cha
vifungashio unaoendelea wilayani Maswa na kupata taarifa ya ujenzi huo ambao
ulipaswa kukamilika Augost 7 lakini mkandarasi SUMA JKT kaomba kuongezewa
muda hadi sept 22 ,2019 kwa kile alichodai awali walipata changamoto
zilizopelekea kuchelewa kuanza .
“kwenye
taarifa yenu ujenzi huu ulipaswa kukamilika lakini hapa mnasema muongezewe muda
,mradi una lengo maalum na mkakati kiwanda kikamilike kianze kutoa products(bidhaa),
mimi niwahakikishie ntakuja hapa tarehe 22 au 23 kujihakikishia kama kweli
ujenzi huo umekamilika ” alisema waziri Jafo
MWISHO
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza na viongozi wa wilaya ya Itilima
baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo, Julai 13,
2019.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Itilima wakati
alipotembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo, Julai 13, 2019.
Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Itilima ambayo
ujenzi wake umemridhisha Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo wkati alipoyakagua jana Julai 13,
2019.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Chilongani(mwenye suti
ya kijivu) akimongoza Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo katika ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya
kilometa moja na nusu ambao ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli aliyoitoa akiwa ziarani
mkoani Simiyu, Septemba 2018.
Mratibu wa TARURA katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
mhandisi. Mathias Mugolozi (aliyenyosha mkono) akitoa maelezo kwa Waziri wa
nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani
Jafo kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi(stendi) Mjini Bariadi wakati
alipotembelea na kukagua mradi huo Julai 13, 2019.
Mratibu wa TARURA katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
mhandisi. Mathias Mugolozi (aliyenyosha mkono) akitoa maelezo kwa Waziri wa
nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani
Jafo kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi(stendi) Mjini Bariadi wakati
alipotembelea na kukagua mradi huo Julai 13, 2019.
Sehemu ya jengo la
abiria lililopo katika kituo
cha mabasi(stendi) Mjini Bariadi ambacho kinaendelea kujengwa na kinatarajia
kukamilika Septemba 02, 2019.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa maelekezo kuhusu ujenzi wa kituo cha
mabasi(stendi) Mjini Bariadi mara baada ya kuitembelea na kukagua mradi huo
Julai 13, 2019.
Sehemu ya barabara ya lami kilometa 1.5 inayojengwa wilayani
Maswa ambayo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli aliyoitoa akiwa ziarani mkoani Simiyu,
Septemba 2018.
Sehemu ya barabara ya lami kilometa 1.5 inayojengwa wilayani
Meatu. ambayo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli aliyoitoa akiwa ziarani mkoani Simiyu,
Septemba 2018.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo(kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa
Simiyu alipomtembelea ofisini kwake wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi
mkoani Simiyu jana Julai 13, 2019.
Waziri wa nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo(kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa
Simiyu alipomtembelea ofisini kwake wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi
mkoani Simiyu jana Julai 13, 2019.
Sehemu ya eneo la Kituo cha Mabasi(stendi) cha mjini
Bariadi.
0 comments:
Post a Comment