Sunday, July 7, 2019

MREMBO DIANA ANTHONY ATANGAZWA MISS SIMIYU 2019


Mrembo Diana Anthony  kutoka wilaya ya Meatu jana ameibuka mshindi wa kwanza kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka  Miss Simiyu mwaka 2019 lilioshirikisha jumla ya warembo 15 hivyo kupeperusha bendera ya ulimbwende mkoa wa Simiyu na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.

Shindano la kumtafuta mlimbwende yamefanyika Julai 6, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, huku Mgeni rasmi akiwa naibu spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.Tulia Ackson  yakisindikizwa na burudani ya kutoka kwa mwanamuziki anayetamba ndani na nje ya nchi Nasibu  Abdul  almaarufu  Diamond Platnumz

Shindano hili limeamuliwa na Majaji wanne ambapo mionggoni mwao wamewahi kuwa Miss Tanzania katika nyakati mbaimbali  Saida Kessy (1997), Hoyce Temu aliyeshinda taji la miss Tanzania mwaka 1999, mtaalamu wa kuibua vipaji nchini Rita Paulsen  maarufu madam Rita na Anitha Kagemulo.

Washindi wengine wanne wa shindano la Miss Simiyu 2019  wanaotengeneza tano bora ni   Rebeca Manoti, Miriam Palangyo, Neema Ismail na Angel Mathew.

 Akizungumza kabla ya kuwatangaza washindi watano wa Shindano la Miss Simiyu 2019, Jaji Mkuu wa Shindano hilo, Hoyce Temu (Miss Tanzania 1999) alisema warembo walioshiriki katika shindano hilo wanavigezo vyote vya kufikia Miss Tanzania.

“Kwa mara ya kwanza Simiyu imefanya maajabu sijawahi kuona warembo wa namna hii na kama hawatafika Miss Tanzania hawa basi mimi nidaiwe na majaji wenzangu” alisema Hoyce Temu.

Akikabidhi zawadi ya  Miss Simiyu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson aliwataka washiriki wote wa Taji la Miss Simiyu kufanya mambo mazuri ili wawe mfano mzuri wa kuigwa.

Aidha   kampuni ya halotel Tanzania pia ilitoa zawadi kwa ya simu za mkononi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tano .

Wadhamini wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na  Simiyu Talent  Company kwa kushirikiana na Grace Entertainmen .ni Jambo Food products Company, Friedkin Conservation Fund, Busega Mazao, Halotel Tanzania na Diamond rock.
MWISHO

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi zawadi Mshindi wa kwanza katika Shindano la Miss Simiyu 2019 , Dayana Anthony, shindano lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.   

Hawa ni Majaji wa Shindano la Miss Simiyu mwaka 2019, Kutoka kushoto ni Saida Kessy (Miss Tanzania 1997), Rita Paulsen , Hoyce Temu(Miss Tanzania 1999)  na  Anitha Kagemulo wakiangalia jambo kabla ya kuanza shindano hilo, lililofanyika Julai 06, 2019.

Hawa ndiyo washindi watano(Top Five) wa Shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakiongozwa na Miss Simiyu 2019 Dayana Anthony(aliyekaa).
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnum akitoa burudani katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi  mara baada ya kumalizika kwa Shindano la Miss Simiyu 2019,  lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.   
Washindi watano(Top Five) wa Shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakiongozwa na Miss Simiyu 2019 Dayana Anthony(aliyekaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson na baadhi ya wadhamini wa shindano hilo, Mkurugenzi wa Jambo Food Products, Salum Khamis(wa nne kulia) na Mwakilishi wa Friedkin  Conservation Fund(kulia)
Hawa ndiyo washindi kumi(Top Ten) wa Shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Washiriki 15 wa Shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadhi ya wananchi wa Simiyu na Majaji wa Shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi wakifuatilia washiriki wa shindano hilo wakionesha mavazi mbalimbali(hawapo pichani).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) na  Mkurugenzi wa Jambo Food Products, Salum Khamis wakicheza muziki katika Shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiwatambulisha baadhi ya viongozi katika Shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Washindi watano(Top Five) wa Shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakiongozwa na Miss Simiyu 2019 Dayana Anthony(aliyekaa) wakiwa katika picha ya pamoja waandaaji wa Shindano hilo Simiyu Talent Company Ltd na Grace Entertainment.
Mkurugenzi wa Simiyu Talent Company Ltd , Zena Mchujuko akitoa neno  la shukrani mara baada ya kumalizika kwa shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Jaji Mkuu wa Shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Hoyce Temu akitangaza washindi watano wa shindano hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson wakifurahia jambo wakati wa  shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mmoja wa waandaji wa Shindano la Miss Simiyu kutoka Grace Entertainment akitoa neno la shukrani mara baada ya kumalizika kwa shindano la Miss Simiyu 2019 , lililofanyika jana Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi.




0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!