Mkuu wa
wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amewaomba wadau wa afya waliopo mkoani
Simiyu kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma
za afya kwa kutenga bajeti kwa ajili ya kuchangia
ununuzi wa vitendea kazi na kujenga
miundombinu ya afya.
Kiswaga amevitaja
vitendea kazi hivyo kuwa ni pamoja na magari ya kubebea wagonjwa (ambulance),
vifaa vya kwenye vituo vya afya ,zahanati na hospitali ili huduma ziendelee
kutolewa kwa ufanisi mkubwa.
Ameyasema
hayo katika kikao cha wadau wa afya kilichofanyika Mjini Bariadi wakati
akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwenye kikao cha wadau
wa afya kilichofanyika Julai 11 na Julai 12, 2019 kwenye ukumbi wa kanisa
Katoliki mjini Bariadi.
Aidha
ameongeza kuwa kuna kila sababu ya mashirika hayo kuongeza majengo na magari ili
huduma za afya zizidi kuimarika mkoani hapo.
Pamoja na
hayo amesema kuwa kama mkoa watahakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa
wadau wa afya mkoani hapo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
"kila
shirika lililopo mkoani hapa linafanya kazi nzuri endeleeni kuzidisha juhudi
hizo bado tuna upungufu wa vitendea
kazi , tunaomba muendelee kutafuta fedha huko ili kuhakikisha kwamba
vitendea kazi kama magari, magari ya kubebea wagonjwa lakini pia majengo bado
ni changamoto pamoja na kazi kubwa nzuri ambazo mmezifanya tunaombeni muendelee
kuweka bajeti hizo "alisema Kiswaga na kuongeza kuwa:
“kama
mkoa tutahakikisha mashirika haya yanatekeleza majukumu yake bila
wasiwasi wowote , watendaji kuanzia ngazi za chini sitegemei kusikia shirika
limeshindwa kutekeleza shughuli zake eti kisa mtendaji kakwamisha , watendaji
kuanzia ngazi ya chini hakikisheni mnatoa ushirikiano wa kutosha ili mashirika
haya yatekeleze majukumu yake”aliongeza Kiswaga
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa wadau wa afya mkoani hapa Dkt Amiri Batenga ambaye ni mwakilishi
wa shirika la umoja wa kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani UNFPA mkoa
wa Simiyu amesema kuwa wameendelea kuboresha vituo vya kutolea huduma za afya
lengo likiwa kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga.
Aidha,
Dkt. Batenga ameongeza kuwa wameshatumia kiasi cha bilioni tano na nusu kwa ajili
ya ujenzi na ukarabati wa majengo ,vifaa pamoja na magari mkoani Simiyu huku
akiomba Serikali kuendele kusimamia na kuhakikisha vituo na vifaa hivyo
vinafanya kazi iliyokusudiwa na wananchi waone haja ya kutumia vituo hivyo
maana vimejwngwa kwa ajili yao.
“kujenga
vituo vya afya ,kuweka vifaa na kufundisha watumishi ni jambo jingine vituo hivi
vinatakiwa vitumike kina mama wajawazito wasipotumia hivi vituo yale malengo
hayawezi fikiwa …pale tumejenga vituo 38 nasasa hivi tumeongeza vingine
viwili ili kufikia malengo lazima mama aje pale tukiunganisha nguvu ya
pamoja kina mama wakafika kwenye vituo vya afya vifo vitaisha
kabisa” alisema Batenga
Mkoa wa
Simiyu una zaidi ya mashirika 17 yanayofanya kazi bega kwa bega na mkoa yakiwa
na lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo
afya na elimu.
MWISHO
Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na
wadau wa afya mkoani Simiyu wakati akifungua kikao cha wadau hao, kwa niaba ya
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI
11 na 12, 2019.
Mratibu
wa Shughuli za Kudhiti na kupambana na UKIMWI, Dkt. Khamis Kulemba akiwasilisha
mada katika kikao cha wadau wa afya, kilichofanyika kilichofanyika Mjini
Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Mwakilishi wa Shirika la DOCTOR WITH AFRICA akiwasilisha
mada katika kikao cha wadau wa afya, kilichofanyika kilichofanyika Mjini
Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Baadhi ya viongozi na
wadau wa afya mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga, katika kikao
cha wadau hao, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Afisa
Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige akiwasilisha mada kuhusu hali ya
lishe katika mkoa, kwenye kikao cha wadau wa afya, kilichofanyika kilichofanyika
Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Baadhi ya viongozi na
wadau wa afya mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga, katika kikao
cha wadau hao, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akizungumza
kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kufungua
kikao cha wadau wa afya mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony
Mtaka kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Mwakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la AMREF zlinaloanya
kazi zake mkoani SImiyu, akiwasilisha mada katika kikao cha wadau wa afya,
kilichofanyika kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Mwakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la CUAMM zlinaloanya
kazi zake mkoani SImiyu, akiwasilisha mada katika kikao cha wadau wa afya,
kilichofanyika kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Mwakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la AMREF zlinaloanya
kazi zake mkoani SImiyu, akiwasilisha mada katika kikao cha wadau wa afya,
kilichofanyika kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Baadhi ya viongozi na
wadau wa afya mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga, katika kikao
cha wadau hao, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Baadhi ya viongozi na
wadau wa afya mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga, katika kikao
cha wadau hao, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Mwenyekiti wa wadau wa afya mkoani Simiyu, Dkt Amiri Batenga
ambaye ni mwakilishi wa shirika la umoja wa kimataifa linaloshughulikia
idadi ya watu duniani (UNFPA)mkoa wa Simiyu, akiwasilisha mada katika kikao cha
wadau wa afya, kilichofanyika kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12,
2019.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Bariadi, Dkt. Mike
Mabimbi akichangia hoja katika kikao cha wadau wa afya, kilichofanyika kilichofanyika
Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Baadhi ya viongozi na
wadau wa afya mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga, katika kikao
cha wadau hao, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI 11 na 12, 2019.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na
wadau wa afya mkoani Simiyu wakati akifunga kikao cha wadau hao, kwa niaba ya
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kilichofanyika Mjini Bariadi JulaI
11 na 12, 2019.
0 comments:
Post a Comment