Thursday, November 25, 2021

HALMASHAURI ZOTE IGENI MKOA WA SIMIYU-NAIBU WAZIRI (AFYA) TAMISEMI

Wito huo umetolewa leo na Mhe.Dkt.Festo Dungage NaibuWaziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serilkali za Mitaa (TAMISEMI-AFYA), mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19 Mkoa wa Simiyu.

Mhe.Dugange,amepongeza Sekretarieti ya Mkoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na viongozi wote wa Mkoa wa Simiyu,kwa kazi nzuri wanayofanya.

"Hongera kwa kazi nzuri sana mnayofanya mkoa wa Simiyu. Hatua ya  ujenzi wa madarasa kufikia 85%, hiyo ni hatua kubwa sana. Lengo la Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha kwamba watoto wetu wanaoingia kidato cha kwanza 2022, wote wanaingia darasani kwa pamoja , hivyo hakutakuwa na uchaguzi wa kuingia kidato cha kwanza kwa mara ya pili yaani (second Selection).

Serikali ya Awamu ya sita imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 15000 kati ya hayo  madarsa 12000 ni kwa ajili ya shule za sekondari na  madarasa 3000  kwa ajili ya shule za msigi.Mkoa wa Simiyu umepatiwa shule 380.

Kuhusa sekta ya afya pongezi kwako Mkuu wa Mkoa, RHMT na RMO, kwani sekta hii ilikuwa na changamoto sana, mikataba ambayo inatoa viwango vya upimaji  utendaji kazi (Key Performance Indicator - KPI) na vikao vya kila robo mwaka ni ubunifu wa hali ya juu kwani inaleta uwajibikaji Kabla ya kuwa Naibu Waziri nilikuwa Mwanasimiyu/mganga Mkuu na hivyo namba yangu simu yangu ilitumika kupokea malamiko mbalimbali ya wanasimiyu.Kipindi cha nyuma kulikuwa na malalamiko  mengi sana ila ndani ya miezi 6 sijapata malalamiko yeyote.

"Asilimia 95 ya huduma za afya hutolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambzo zipo chini ya TAMISEMI. Niwapongeze sana Mkoa wa Simiyu kwani  kwa kipindi cha miezi sita  mlianza matumizi ya mfumo wa GoThomis, na   65% ya vituo vyenu vya afya vinatumia mfumo huo  kwa  ajili ya kukusanya mapato. Kama aliyoeleza mkuu wa Mkoa  mfumo huo umewasaidia kuongeza mapato kutoka Tsh.200mln–600mln. Makusanyo haya yanasaidia sana kuacha utegemezi toka Serikali kuu au wafadhili. Hivyo ni vyema Halmashauri zote ziige mkoa wa Simiyu" amesema Mhe. Dugange .


Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amemshukuru Mhe. Dugange kwa kutembelea mkoa wa Simiyu,na kumhakikishia kuwa ujenzi wa madarasa ambao umefikia  85% utamalizika kwa wakati. Kwa upande wa sekta ya afya Mhe. Kafulia amemfahamisha Naibu Waziri Tamisemi /afya kuwa mafanikio katika sekta ya afya yametokana na utendaji kazi mzuri wa Mganga mkuu wa mkoa pamoja na timu yake RMO,kwani kwa kipindi cha miezi sita mapato yameongezeka kwa asilimia 300. "Nimesaini mkataba wa utendaji kazi kati yangu na  Wakuu wa wilaya .Niwapongeze  wakuu wa Wilaya kuwa sasa tunasomana" amesema Kafulila.

 

Akiwasilisha taarifa ya hali ya utekelezaji mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 mkoa wa Simiyu,Kaimu Katibu Tawala M,Injinia Mashaka Luhamba alieleza kuwa Mkoa wa Simiyu umetengewa jumla ya Tshs 20,476,951,633.30 kwa ajili ya kutekeleza miradi inayolenga kuimarisha miundombinu ya Sekta za Elimu na Afya na mapambano dhidi ya UVIKO 19. Fedha hizo zimetolewa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Shule za Sekondari,Shule Shikizi,Hospitali za Wilaya katika ngazi za Halmashauri za Wilaya, Miji ,Manispaa na Majiji. Aidha, fedha zingine zimepelekwa kutekeleza miradi ya kipaumbele katika Hospitali ya Rufaa za Mkoa na Mamlaka za maji.

Kuhusu miradi ya ujenzi wa shule mkoani Simiyu,Injinia Luhamba amesema, hadi sasa miradi iliyoanza kutekelezwa ni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 380 vya shule za Sekondari na vyumba vya madarasa 69 vya Shule Shikizi. Mpaka sasa ujenzi huo umefikia  85% ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.Injinia Luhamba ameeleza kuwa pamoja na mafanikio haya katika ujenzi wa Madarasa Mkoa umekuwa ukikabiliwa na  changamoto mbalimbali hususani katika Wilaya ya Maswa na Itilima ambapo changamoto kubwa imekuwa upatikanaji wa vifaa. Vifaa vya viwandani kama vile bati na saruji kuchelewa kufika katika maeneo husika hasa kwa Halmashauri ambazo zilitumia mfumo wa manunuzi ya pamoja. Bei ya vifaa kupanda ghafla mara tu miradi ilipoanza na hivyo kusababisha gharama ya mradi kuongezeka.Shule ambazo ziliomba kibali cha kuhamisha fedha kwenda katika maeneo mengine kwa ajili ya ujenzi zilichelewa kupata kibali na hivyo kusababisha kuchelewa kuanza kwa mradi.

Kuhusu sekta ya afya,mganga Mkuu Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniface Marwa, ameeleza kuwa kwa kipindi cha miezi tisa kumekuwa na mafanikio makubwa sana katika sekta ya afya Mkoani Simiyu.Awali kulikuwa na vituo vya afya 218 lakini sasa kuna vituo vya afya 221.Aidha upatikanaji wa dawa nao umeongezeka kufikia asilimia 91.

 Dkt. Marwa amesema mafanikio yote haya yamepatikana kutokana ushirikiano uliopo baina ya wafanyakazi wa Sekta ya Afya, uongozi bora toka kwa mkuu wa mkoa na menejimenti yake. DKt Marwa amemfahamisha Naibu Waziri kuwa moja ya siri kubwa ya mafanikio haya ni usainishaji wa mikataba ya ya utendaji kazi katika sekta ya afya kati ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya ambao nao walisainishana na maafisa tarafa, Katibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri zote ambao nao wamesainishana na waganga wakuu wa halmashauri.

"Lengo la kusaini mikataba hii ni kuhakikisha utendaji kazi katika sekta ya afya unafanyika kwa weledi zaidi. Aidha ripoti za utendaji kazi zimekuwa zikitolewa kila robo mwaka na kwa kweli kumekuwa na mafaniko makubwa sana.Lengo letu ni kutaka kuwe na usimamizi na utendaji wa pamoja katika mkoa"amesema.Dkt Marwa.

 

Akijibu hoja kuhusu changamoto ya uhaba wa watumishi sekya ya afya Mhe. Dugange amekiri kuwa mkoa wa Simiyu ni mmoja kati ya mikoa inayokabiliwa na changamoto  kubwa ya uhaba wa Watumishi wa  sekta ya afya.Serikali imeliona hilo na  inafanyia kazi kwa  kuendesha zoezi la kujua daktari na N esi ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wanaopaswa kuhudumiwa na dakkati /nesi mmoja ( Doctor/Nurse Patient ratio).Lengo la Serkali ni kuhakikisha kuwa kila mkoa uwe na watumishi angalau si chini ya  60% ya mahitaji yao .Akizungumzia 40% ya mapato ya ndani baada ya kutoa mapato lindwa, Mhe. Dugange amesema kuwa lazima fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo.

 Mhe. Festo Dugange yupo ziara Mkoani Simiyu kwa lengo la kupitia miradi ya ujenzi wa madarasa ya Uviko na vituo vya afya,ili kuona shughuli zinazoendelea na Changamoto mbalimbali wanazokalibiana nazo katika utekelezaji wa shughuli hizo. Mwisho


NAIBU WAZIRI TAMISEMI (AFYA) MHE. DKT. FESTO DUGANGE AKISALIMIANA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MKOA WA SIMIYU MARA BAADA YA KUWASILI MKOANI HAPO

KAIMU RAS , INJINIA MASHAKA LUHAMBA AKISOMA TAARIFA YA MKOA

MGANGA MKUU OFISI YA MKUU WA MKOA SIMIYU DKT. BONIOFACE MARWA AKISOMA TAARIYA YA SEKYA YA AFYA

KULIA, ANAYEONGEA NI NAIBU WAZIRI TAMISEMI(AFYA),MHE,DKT.FESTO DUGANGE AKIZUNGUMZA, KUSHOTO ANAYESIKILIZA KWA MAKINI MKUU WA MKOA WA SIMIYU MHE. DAVID KAFULILA
WASHIRIKI KUANZIA KUSHOTO KUTOKA SEKTA YA AFYA, AAS-ELIMU,ASS-LGA, NA SEKTA YA AFYA WAKISIKILIZA KWA MAKINI






 


Wednesday, November 24, 2021

Wilaya ya Bariadi, Yapongezwa kwa Kupata Leseni ya Kuchimba Madini

Washiriki wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wakati wa kikao

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila akizungumza na Washiriki wa kikao cha kuwapongeza Wanabariadi kwa kupata leseni ya Kuchimba Madini

Washiriki wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amempongeza Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mhe.Lupakisyo Kapange na Wakurugenzi Bw.Khalid Mwalami na Adrian Jungu kwa kazi kubwa ambayo wameendelea kuifanya katika sekta ya madini. 

Rc.Kafulila ametoa pongezi hizo kwenye kikao cha kukabidhi leseni ya kuchimba Madini kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Bariadi mji na Bariadi vijijini, hafla iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya Bariadi.

 " Nakupongeza Mkuu wa Wilaya, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bariadi mji na Bariadi vijijini , kwani Halmashauri ya Bariaji Vijijini ilikuwa dhoofu sana katika makusanyo kiasi cha kufikiria kuifuta. Lakini ndani ya miezi 6 imetoka nafasi za mkiani mpaka nafasi ya 15 kati ya halmashauri185 huku halmashauri ya mji ikishika nafasi ya 13".Amesema Kafulila.

RC. Kafulila - Ampongeza Mmiliki wa Kiwanda cha Kuchambua na Kusafisha dhahabu - ELIFRA INVESTMENT LIMITED.

Mhe.Kafulila,amempongeza mjasiliamali Frank Malima, ambaye ndiye mmiliki wa kiwanda cha kuchambua na kusafisha dhahabu cha ELIFRA INVESTMENT LIMITED.

Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akiwa ameambatana na Viongozi wengine wa Mkoa mara alipotembelea kiwanda cha kuchambua na kusafisha dhahabu cha ELIFRA INVESTMENT LIMITED kilichopo Mkoani Simiyu, hivi karibuni.

Akizungumzia Bw.Frank Malima, Mhe. Kafulila alieleza kuwa Bw. Malima  ni mubobezi wa masuala ya madini, maarifa ambayo ameyapata  nje ya nchi ikiwemo Afrika ya Kusini.

Akimshukuru, Mkuu wa Mkoa, Bw.Malima ameahidi kuwapatia kinamama mashine aina ya BALL MILL,mashine ambayo itaongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 5 kwa mwezi mpaka tani 100 kwa mwezi, hii ikiwa ni matumizi ya mashine moja.

Kiwanda cha kuchambua na kusafisha dhahabu cha ELIFRA INVESTMENT LIMITED kina uwezo wa kusafisha kilo 15-20 za dhahabu kwa siku. 




Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kafulila pamoja na viongozi wengine katika kiwanda cha kuchambua na kusafisha  dhahabu cha ELIFRA INVESTMENT LIMITED- Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila wa kwanza Kulia, akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Lupakisyo Kapange pamoja na Viongozi wengine wakipata maelezo wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda cha Kuchambua dhahabu cha ELIFRA INVESTMENT LIMITED kilichopo Bariadi.

Tuesday, November 23, 2021

RC. Kafulila Aridhishwa na Ujenzi wa Madarasa ya Uviko-19 - Wilayani Bariadi

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.David Kafulila amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Lupakisyo Kapange, Mkurugenzi wa Bariadi  Bw.Khalid Mwalami na timu yake pamoja na viongozi wa shule alizozikagua kwa usimamizi mahiri. 

Mhe Kafulila alitoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ambapo zaidi ya asilimia 90 ya majengo yake yamefikia hatua ya kupauliwa.

Akiwa ameridhishwa na kazi hiyo,Mhe. Kafulila amepongeza kasi ya Ujenzi wa madarasa katika Wilaya ya hiyo na kusema, Wilaya hiyo ni mfano wa kuigwa na wilaya zingine zote. 

Aidha Mkuu wa Mkoa amempongeza na kumtolea mfano Mkuu wa shule ya sekondari Mbiti, Bi. Salome Bulenge, ambaye pamoja na changamoto zingine, shule yake ndio ya kwanza kufikia hatua ya upauaji.

Ikiwa ishara ya kuonyesha kwamba ujenzi umefikia hatua ya kupaua, wakiwa katika shule ya Sekondari Mwamlapa ,Mhe.Kafulila akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Kapange walinyanyua bati na kumkabidhi fundi ujenzi .


Mhe. David Kafulila akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi. Mhe. Lupakisyo Kapange wakijadili jambo





Rc. Kafulika akiwa na Dc. Kapange wakinyanyua bati ikiwa ni ishara ya kuonyesha ujenzi umefikia hatua ya Upauaji



Sunday, November 21, 2021

"Bodi Ya Pamba, AMCOS, SIMCU Saidieni Wakulima Wa Pamba"-RC- Kafulila

Taasisi nyingi ambazo zimekuwa zikipata fedha kupitia ushuru wa Pamba, zimeshindwa kuwasadia wakulima na badala yake wanaonufaika ni viongozi kupitia fedha zinazotokana na Pamba ya wakulima. Hali hii imepelekea wakulima wengi nchini wakiwemo wanaozalisha Pamba, kuchukia ushirika licha ya kulazimishwa kupeleka mazao yao Amcos kwa ajili ya kuuzwa.

Mhe. Kafulila amesema hayo, wakati wa kikao na viongozi wa vikozi kazi vya zao la Pamba alipotembelea  Tarafa ya Mwamapala Wilaya ya Itilima.Mhe. Kafulila amesema Bodi ya Pamba, Vyama vya msingi vya Ushirika (Amcos), SIMCU ni vyombo ambavyo vinatakiwa kusimamia zao la Pamba na kuwasaidia wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija. Vyombo hivyo vimekuwa vikikusanya ushuru unaotokana na zao la Pamba ambalo ni jasho la mkulima, lakini wameshindwa kuwasaidia wakulima.

“Kwa mkoa wa Simiyu, msimu uliopita Amcos walipata zaidi ya Bilioni 4, Chama kikuu cha ushirika (SIMCU) walipata zaidi ya Milioni 800, Bodi ya Pamba nayo ilipata fedha nyingi, lakini fedha hizo hazijarudi kwa wakulima kuwasaidia,”amesema Kafulila. 

Msingi wa kuanzishwa kwa vyombo hivyo,ulikuwa kukusanya ushuru na baada ya msimu kuisha kuwasaidia wakulima wakati wa maandalizi ya msimu mpya ili kuweza kuzalisha kwa tija. 

“ Kama mkoa tumeanza kupambana na hii mifumo kwa kuifanyia marekebisho, tumeanza na hii ya mkulima kuwa mwanachama, tunataka kila mkulima awe mwanachama kwa sharti la kumiliki shamba la pamba,”amesema Kafulila.

Tumepeleka mapendekezo Wizara ya Kilimo,kubadilishwa kwa masharti ambapo mkulima kigezo cha kujiunga na Amcos kitakuwa shamba lake na siyo vigezo vingine vilivyopo kwa sasa ikiwemo pesa.Hali hii itafanya wakulima kuongezeka kwenye Amcos na maamuzi kufanywa na wengi,lakini pia kuweza kupata viongozi sahihi na siyo kama ilivyo sasa ambapo wanachama ni wachache na wanafanya maamuzi ya wakulima wote.

Hata hivyo Kafulila ameeleza kuwa mbali na hilo kama mkoa watapitia mifumo yote na kuhakikisha inabadilishwa ndani ya mkoa, ambao umejiwekea lengo la kuzalisha tani laki tano katika msimu ujao wa Pamba 2021/22.

 Mwisho.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na Viongozi wa Vikosi kazi vya Pamba Wilayani Itilima 

Viongozi wa vikosi kazi vya Pamba Wilayani Itilima wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa

Wa Kwanza kushoto Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Fauzia Suleiman, Akiwa amefuatiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo Wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mhe. Kafulila



Mhe. Kafulila akiwa ameongozana na Viongozi wa Halmashauri ya Itilima wakifanya ukaguzi wa miradi mbalimbali 



Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima akizungumza na Viongozi wa Vikosi kazi vya Pamba Wilayani Itilima 


Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa 




Saturday, November 20, 2021

"Tokeni Maofisini Nendeni Site Mkaangalie Hali ya Ujenzi" - RC. KAFULILA


Mkuu wa Mkoa Wa Simiyu Mhe. David Kafulila akitembelea Miradi ya Ujenzi wa Shule za Miradi ya Uviko-19



Mkuu wa Mkoa Mhe. Kafulila akikagua kiasi cha Zege 

Mkuu wa Mkoa Akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya Itilima Mhe. Faiza Suleiman



Mkuu wa Mkoa akiwa ameambataka na viongozi mbalimbali wakikagua miradi ya Ujenzi wa Shule za 
Uviko-19, Wilayani Itilima hivi karibuni


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila, amewataka viongozi wa Wilaya ya Itilima  pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kuongeza ufuatiliaji katika ujenzi wa madarasa  ya Uviko-19 kwani Wilaya hiyo bado ipo nyuma kwa kiwango kikubwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mhe.Kafulila ameyasema hayo mara baada ya kupokea taarifa ya miradi ya ujenzi wa madarasa kwa kutumia fedha za Uviko-19, wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa hayo hivi karibuni. 

“Mpaka sasa mlitakiwa muwe mmefikia asilimia zaidi ya 50, lakini mpo asilimia 20, hii kasi ni ndogo sana, ongezeni kasi tokeni maofisini nendeni site mkaangalie hali ikoje kama kuna matatizo mtatue. Mkuu wa Wilaya unatakiwa kuanzisha mkakati wa kujenga usiku na mchana, tafuteni taa, kila sehemu ambapo wanajenga waambieni wajenge usiku na mchana. Waalimu na Wasimamizi, simamieni kwa umakini na haraka ili hayo majengo yajengwe kwa kiwango bora, thamani ya pesa iwepo lakini pia  msiache kuchukua hatua kwa wabadhilifu..”Amesisitiza Mhe. Kafulila.

Akitoa taarifa kuhusu kuchelewa kwa miradi hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Faiza Suleiman ameeleza kuwa sababu ya kuchelewa kwa ujenzi wa miradi hiyo imetokana na kuchelewa kupata  vifaa ikiwa pamoja na vifaa kuchelewa kufika kwenye maeneo husika kutokana na changamoto ya barabara.Aidha Mhe.Faiza alieleza kuwa ujenzi wa miradi hiyo umefikia asilimia 20 na upo usawa wa msingi katika maeneo yote. 

Mwisho

 

Thursday, November 18, 2021

UZINDUZI WA UGAWAJI PIKIPIKI KITAIFA KWA MAAFISA UGANI KATIKA MIKOA INAYOZALISHA MAZAO KIMKAKATI, WAFANYIKA MKOANI SIMIYU.

Akizungumza,Mkurugenzi mkuu Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga alitoa shukrani kwa Waziri wa kilimo Mhe. Adolf Mkenda kwa kukubali kuhudhuria zoezi la ugawaji wa pikipiki. 

Pongezi kwa mkoa wa Simiyu kwa kuzalisha zaidi ya asilimia 61 ya pamba yote nchini msimu huu wa kilimo.Tatizo la msingi katika sekta ya kilimo ni kupungukiwa maarifa kwa sababu ya wataalamu kutowezeshwa ipasavyo.

Mkakati wa Wizara ni kuimarisha huduma za ughani. Maafisa ughani wote watakuwa na pikipiki kwa sababu ni vigumu kwa afisa ugani mmoja asiye na usafiri kutembelea kata nzima.Hivyo leo wataalam watapewa vitendea kazi ili waweze kuwafikia wakulima.Wakulima wafuate kanuni za kilimo.Lengo la zoezi la leo ni kuhakikisha mkulima anaboreshewa kielimu. Maafisa ughani wasitumie pikipiki kama biashara.Halmashauri zinapaswa kusimamia vizuri zoezi la kilimo cha pamba ili kuongeza mapato 


Dr. Sophia Kashenge Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Mbegu za Kilimo,Tanzania, alitoa pongezi na shukrani kwa Wizara ya Kilimo kwa kutoa kipaumbele kikubwa kwa kazi ambazo zilikuwa hazipewi kipaumbele. Kazi ya Wakala wa mbegu za Kilimo ni kuhakikisha mbegu zinazogunduliwa na mtafiti zinamfikia mkulima na kuzizalisha kwa wingi ili zifike kwa mkulima kuendana na uhitaji.

Wakala wanafanya kazi kupitia mashamba kumi na nne ya mbegu ya serikali. Ombi letu kwa Serikali, ni kutuongeza mashamba kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu.

Mkoa wa Simiyu umepokea mbegu za alizeti tani 114 ambapo tani 60 zimepelekwa Halmashauri ya Wilaya ya itilima, tani 34 Meatu na tani 20 Maswa kwa ajili ya kilimo cha alizeti.Aidha, Wakala wa mbegu za kilimo wameanzisha duka la mbegu mkoa wa Si 

Akizungumza,Balozi wa Pamba Bw. Agrey Mwanri alitoa Shukrani kwa Wizara/Serikali kwa maamuzi ya kukubali mbegu zitolewe kwa mkopo. Hili ni jambo la busara kwani Wakulima watakatwa mikopo hiyo wakati wakiuza mazao yao.

Shukrani kwa Waziri Prof. Adolf Mkenda kwa kuja kutoa pikipiki. Tahadhari kwa Maafisa Ugani mnapaswa kutumia pikipiki kwa kazi iliyokusudiwa pekee. 

Nitumie fursa hii kuwashauri wakuu wa Wilaya/Mikoa kusimamia matumizi sahihi ya pikipiki hizo na kuhakikisha zinafanya kazi iliyo kusudiwa.

Kuleta vitendea kazi ambavyo watumishi wataenda kivitumia na kurahisisha kazi ya kilimo ni ukomavu wa kisiasa. 

Kila mkulima wa Pamba akimaliza kuvuna Pamba ahakikishe anatoa masalia yote ili kuhakikisha msimu mpya unapoanza yasiwepo mabaki na masalia yote ya pamba ili kukabiliana na wadudu waharibifu. 

Zoezi la kutoa masalia halijafanyika katika utimilifu kwani baadhi ya wakulima hawajatoa hivyo naomba Serikali kuwachukulia hatua. 

 M/kiti CCM Mkoa wa Simiyu Bi.Shemsa Mohamed alieleza lengo letu ni kuhakikisha Simiyu inakwenda kuwa kinara wa uzalishaji wa Pamba na kilimo cha biashara. Ombi la wakulima ni kupunguziwa makato ya (Amcos, Union, Bodi ya Pamba) pamoja na ongezeko la bei ya mbegu usiokuwa na utaratibu mzuri. 

Maafisa Ugani wanapaswa kutumia pikipiki kwa kazi ambayo Serikali imemtuma pamoja na kuhakikisha wakulima wanapata tija na kuongeza uzalishaji wa Pamba.

Amcos hazinufaishi wakulima. Pamba ni zao linalotegemewa na wakulima kuwainua ki uchumi hivyo  Amcos ziwe na utaratibu ambao mkulima atanufaika moja kwa moja.

Katibu mkuu wizara ya kilimo- Bw. Andrea Masawe,alisema ugawaji wa Pikipiki ni hatua ya utekelezaji wa kile Serikali ilichoahidi ikiwa ni kipaumbele cha tatu cha mkakati wa kuongeza tija ya kilimo nchini.

Nina imani kubwa kuwa uwekezaji uliofanyika una kwenda kuboresha huduma za ugani ili mkulima apate elimu ya uhakika ya kanuni bora za kilimo.

Maafisa ugani 258 kutoka mikoa 3 na 1018 kutoka mikoa 18, wamepata mafunzo. Mkoa wa Simiyu una maafisa ugani 134 ambao wamepata mafunzo hayo.

Tunategemea kutakuwa na mashamba darasa mawili kwa kila afisa ugani na shamba darasa moja la mfano. Uzinduzi huu ni sehemu kidogo ya zoezi kubwa la kugawa vitendea kazi kwa wakulima.Wizara imeimarisha taasisi kutoa ushirikiano kwa taasisi zake katika utendaji wa kazi.Mkoa wa simiyu umepokea pikipiki 86. 

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila alieleza, Mkoa wa Simiyu ni mkoa wa kilimo. Asilimia 92 ya mkoa ni vijiji na wakazi wake ni Wakulima. 

Niwahakikishie kuwa Afisa Ugani yeyote atakayetumia Pikipiki kufanya bodaboda hatakuwa mtumishi wa Serikali katika mkoa wa Simiyu. 

Mkoa umetengeneza vikosi katika ngazi zote hivyo pikipiki hizi zitakwenda kusaidia hasa ngazi ya kijiji na kata ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa Pamba.

Utekelezaji wa azimio la Meatu la uzalishaji wa Pamba, Wizara ikiunga mkono mkakati huu itaongeza uzalishaji wa Pamba nchini. Mkoa utahakikisha watumishi ambao sio waadiilifu katika vyama vya Ushirika, Ushirika unawaondoa.Lengo la kuchukua hatua kali ni sababu ya kilio cha muda mrefu cha wakulima kudhurumiwa haki zao kwa sababu utaratibu unakiukwa huku sheria ikimbana mkulima auze katika ushirika. 

Mkoa una Amcos zaidi ya 300 hivyo mkoa unaomba kupatiwa mafunzo kwa watumishi wa Amcosi ili kuondoa mapungufu yaliyopo ambapo watumishi wanaonekana sio waadilifu kwa sababu ya kukosa maarifa.Wizara iendelee kuwezesha mikakati ya kuinua kilimo cha Pamba ambapo kwa sasa halmashauri zinabeba mzigo wa kuwezesha mikakati hiyo. 

Mkoa wa Simiyu umeteuliwa kuwa mkoa ambao unazalisha mafuta kwa kiwango kikubwa .Hivyo naoimba Wizara kuwezesha mikakati ya kuhakikisha mkoa unafikia malengo ya kuongeza uzalishaji. Mkoa utatumia shule kama mashamba darasa katika kuzalisha alizeti na kila shule itakuwa na mshamba darasa ya Alizeti pamoja na Pamba. Mkoa unahamasisha vilimo mbalimbali vya biashara kwenye kila wilaya.

Matumaini yetu ni kuwa mkoa wa Simiyu utaendelea kuwa karibu na Wizara kwa sababu m 92% ni wakulima na ni mkoa wa mfano katika kilimo. 

Akizungumza, Waziri wa kilimo Mhe.Prof. Adolf Mkenda, alisema kugawa pikipiki ni zoezi la kurudisha hadhi ya maafisa ugani. Nimpongeze mkuu wa Mkoa kwa jitihada za kuhakikisha anaongeza tija kwenye kilimo katika Mkoa wa Simiyu.Kama hatutawathamini Madaico na Maafisa ugani hatutafikia kile kilichoagizwa na ilani ya chama cha mapinduzi 

Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila mkulima anapata kilo zaidi ya 1000 kwa ekari kwenye zao la Pamba.Tija ikiwa ndogo wanapata shida kwenye uzallishaji wa malighafi katika viwanda. Lengo kubwa la kilimo ni kupunguza bei ya mazao katika nchi yetu na kuongeza kipato cha wakulima. Hivyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha inamuwezesha mkulima kuzalisha mazao mengi zaidi ili hata kama bei ya mazao itakuwa ndogo mkulima bado atapata faida. Tunataka hata Bei ya mazao ikishuka lakini kipato cha mkulima kiongezeke.Hii inawekana kwa kuongeza tija ya kilimo. 

Changamoto kubwa kwenye kilimo ni tija. Baada ya utafiti wa kilimo bora na kupata mbegu bora za pamba kwa sasa tunaendelea na kuboresha kazi za ugani. Afisa ugani anajukumu la kupeleka matokeo ya utafiti kwa wakulima na kufundisha matumizi ya mbegu bora. Maafisa ugani wanajukumu la kuwafundisha wakulima mabadiliko ya hali ya hewa ili waweze kulima mazao yanayokabiliana na ukame. 

 Hatuwezi kupuuza huduma za ugani tukabaki salama Hakuna maafisa ugani wa kutosha, nchi ina maafisa ugani 6704 sawa na asilimia 32.6 uhitaji ukiwa ni maafisa ugani 20538. Hakuna Vitendea kazi vya kutosha kwa wasimamizi wa shughuli za ugani na ushirika (Daico) hawana vitendea kazi kama magari na hakuna bajeti ya kuwawezeaha kuendesha shughuli za ugani katika ngazi zilizo chini yao. Kuwapatia mafunzo maafisa ugani ili kurejesha kilimo cha kisasa . 

 Makusanyo ya mapato ya Halmashauri nyingi yanategemea kilimo, licha ya kuwa wasimamizi wa kilimo hawapewi kipaumbele cha mahitaji yao katika kuwawezesha kufanya kazi yao. Halmashauri hutenga fedha kwa ajili ya maafisa ugani, Wizara itatoa mafuta kwa msimu huu wa kilimo pamoja na vipuli baada ya msimu huu wa kilimo Halmashauri zitaendelea na zoezi hilo. 

 Niahidi; Maafisa ugani kufufua mashamba darasa pamoja kupatiwa mafuzo rejea. Maafisa ugani kwa mikoa mitatu kununuliwa simu janja kwa ajili ya kujaza taarifa za wakulima wanapo watembelea wakulima kutatua changamoto za wakulima Bodi zote za mazao zitanunua pikipiki kwa ajili ya kuboresha huduma za ugani. Maafisa ugani wanapaswa kutunza pikipiki vizuri. Wakulima wazingatie kung'oa mabaki ili kumaliza magonjwa ya pamba. Ambaye hajang'oa masalia atachukuliwa hatua za kisheria. 

Mwisho.

Waziri wa Kilimo Mhe.Prof. Adolf Mkenda akifanya uzinduzi wa Kitaifa wa Ugawaji Pikipiki kwa Maafisa ugani katika mikoa inayozalisha Mazao ya Kimkakati,

Picha za baadhi ya pikipiki zilizogawiwa kwa maafisa Ugani, jumla ya pikipiki 86 ziligaiwa kwa maafisa Ugani.


Picha za Viongozi baada ya uzinduzi wa ugawaji Pikipiki

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca  Kayombo akijaribu Pikipiki zilizogawiwa kwa maafisa ugani







Wakuu wa Wilaya za Dodoma wakipokea mbegu na mafuta ya alizeti kutoka kwenye duka la Wakala la mbegu, duka ambalo limefunguliwa Mkoani Simiyu.Mbegu hizo zilitolewa na Waziri wa kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!