Thursday, November 24, 2016

WANAUME WAHAMASISHWA KUFANYA TOHARA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akizungumza na wadau wa Mapambano dhidi ya Ukimwi  katika Uzinduzi wa Mpango mkakati wa Mkoa huo uliofanyika  katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na wadau wengine wa Mapambano dhidi ya Ukimwi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo (hayupo pichani) katika Uzinduzi wa Mpango mkakati wa Mkoa huo uliofanyika  katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Mageda Kihulya akiwasilisha mada katika  Mkutano wa wadau wa Mapambano dhidi ya Ukimwi wa mkoa huo  uliofanyika  katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akichangia jambo katika  Mkutano wa wadau wa Mapambano dhidi ya Ukimwi wa mkoa huo  uliofanyika  katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa Mapambano dhidi ya Ukimwi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo (hayupo pichani) katika Uzinduzi wa Mpango mkakati wa Mkoa huo uliofanyika  katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.
Mchungaji wa Kanisa la  AICT Bariadi Mjini, Amosi Ndaki(kushoto)  na Shekhe wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola (kulia) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano wa wadau wa Mapambano dhidi ya Ukimwi wa mkoa huo  uliofanyika  katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.
Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la AGPAHI Mkoa wa Simiyu na Shinyanga, Dkt. Gastor Njau akiwasilisha katika  Mkutano wa wadau wa Mapambano dhidi ya Ukimwi wa mkoa huo  uliofanyika  katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.
Mchungaji wa Kanisa la  AICT Bariadi Mjini, Amosi Ndaki(kushoto)  akichangia jambo katika  Mkutano wa wadau wa Mapambano dhidi ya Ukimwi wa mkoa huo  uliofanyika  katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi
Na Stella Kalinga
Wanaume ambao bado hawajafanyiwa tohara mkoani Simiyu wamehamasishwa  kufanya hivyo ili kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi Mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka katika ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa Mapambano dhidi ya Ukimwi na Uzinduzi wa Mpango mkakati wa Mkoa huo uliofanyika jana katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki  la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.

Mtaka amesema kwa mujibu wa tafiti  zilizofanyika nchini Afrika ya Kusini, Kenya na Uganda  imethibitishwa pasipo shaka  kuwa tohara kwa wanaume hukinga maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60, hivyo wanaume wajitokeze waweze kupata huduma hiyo bure.

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa Mapambano dhidi Ukimwi Mkoa wa Simiyu, Mratibu wa Mapambano dhidi ya Ukimwi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Daktari Wilfred Magulu amesema ni asilimia 32 tu ya wanaume Mkoani Simiyu ambao wamefanyiwa tohara.

Daktari Magulu amesema Serikali imeweka mkakati wa kutoa elimu kwa wananchi hususani wanaume na kuwahamasisha ili wawe na mwamko na kuona umuhimu wa kufanyiwa tohara pasipo gharama yoyote katika Hospitali zote na vituo vyote vya kutolea huduma za afya, kwa lengo la kufikia asilimia 72 ya Kitaifa.

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema wataalam wa afya na wadau wa Ukimwi kwa ujumla wanao wajibu wa kuwaelimisha wananchi juu  ya kujikinga na maambukizi, umuhimu wa kupima VVU na kuwajengea ujasiri wa kupokea matokeo ya vipimo vyao ili wanapogundulika kuwa na maambukizi waanze matibabu mapema.

Mtaka amesema wataalam hao wanatakiwa kuliepusha Taifa katika maambukizi mapya ya VVU kwa kuwaeleza wananchi ukweli juu ya njia sahihi za kujikinga na maambukizi mapya ikiwa ni pamoja na Matumizi sahihi ya kondomu.

“Waratibu waelezeni watu umuhimu wa kujikinga na maambukizi, fanyeni utafiti kuona maduka mangapi ya vijijini yanauza kondomu mkikuta hakuna wapimeni wananchi katika hivyo vijiji muone hali ya maambukizi ikoje, Msisiishie kuyazungumza masuala haya kwenye makongamano na warsha” , alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa Waratibu wa Mapambano dhidi ya Ukimwi katika Halmashauri zote za Mkoa huu wahakikishe baa  na nyumba zote za kulala wageni zilizopo mijini na maeneo yote yenye watu wengi zinawekewa kondomu  na elimu ya matumizi sahihi ya kondomu hizo itolewe kwa wananchi.

Wakati huo huo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt.Mageda Kihulya amesema wananchi wajijengee utaratibu wa kupima afya na wanapogundulika kuwa na maambukizi Virusi vya Ukimwi watembelee vituo vya kutolea huduma za Afya ili waanze kupewa huduma mapema.

Hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi/UKIMWI ni asilimia 3.6 kama ilivyooneshwa kwenye utafiti wa mwaka 2011-2012 ukilinganishwa na kiwango cha Kitaifa cha asilimia 5.1.


Mkutanowa wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi Mkoani Simiyu umewashirikisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Halmashauri, Wabunge, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Waratibu wa Mapambano dhidi ya Ukimwi wa Wilaya zote na Wakuu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayojihusisha na Mapambano dhidi ya Ukimwi mkoani humo.

Thursday, November 17, 2016

WAKAZI WA MASWA KUPATA HATI MILIKI ZA VIWANJA NDANI YA SIKU 90


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja Modeco  wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu
Baadhi ya wanachi Wilaya ya Maswa wakimsikiliza : Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika viwanja vya Modeco wilayani humo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (kushoto) akipokelewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Donatus Weginah mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akisalimiana na Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Miundombinu, Mhandisi Deusdedit Mshuga mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Mkuu wa Wiaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja Modeco  wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(wa pili kushoto ) akizungumza na wataalam wa Ardhi wa Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Wataalam wa Ardhi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(kushoto) akiangalia Taarifa za Mfumo ukusanyaji wa tozo za ardhi kwenye Ofisi ya Idara ya Ardhi ya Halmashauri ya mji wa Bariadi, (kulia) ni Fundi Sanifu wa Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akisalimiana na Mbunge wa Maswa Magharibi Mhe.Mashimba Ndaki mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akisalimiana na Mbunge wa Maswa Mashariki Mhe.Stanslaus Nyongo  mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa.
Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya ya Maswa, Mhe. Mdimi Ilanga akitoa ufafanuzi wa masaula mbalimbali yanayohusu baraza hilo katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akipokea moja ya boksi la chaki za Maswa(Maswa Chalks) kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe mara baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza Chaki na kununua chaki katoni kadhaa wilayani humo wakati wa ziara yake.


Afisa Ardhi wa Wilaya ya Maswa, Musa Warioba akitoa ufafanuzi juu ya kero na malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na wananchi kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika jana katika uwanja wa Modeco wilayani humo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Wilaya ya Maswa na Vijana wa Maswa Family alipotembea kiwanda cha kutengeneza Chaki wakati wa ziara yake wilayani humo.
  


Na Stella Kalinga
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko kutoa hati miliki za viwanja kwa wakazi wa wilaya hiyo ndani ya siku 90 (hadi kufikia tarehe 15 Februari, 2017 )
 Mhe. Mabula aliyasema hayo jana alipozungumza  na wananchi wa Wilaya ya Maswa katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika uwanja wa Modeco akiwa katika ziara yake wilayani humo akitokea wilayani Bariadi

 Mhe. Mabula amesema wananchi walio na Matoleo ya Viwanja (Letter of offer) waliyopewa awali wawasilishe katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ili wapatiwe hati miliki ambazo zitawasaidia kuwahakikishia usalama wa nyumba zao kwa kupunguza hatari ya kutokea kwa migogoro isiyo ya lazima.

Aidha, Mhe.Mabula amesema wananchi watakapopata hati miliki hizo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi katika kupata mikopo ya Benki na Taasisi nyingine za kifedha kama dhamana yao.

Kwa upande wake Mbunge wa Maswa Magharibi Mhe.Mashimba Ndaki amesema pamoja na Halmashauri kutoa hati hizo baadhi ya wananchi wana hati za kimila ambazo zimekuwa zikikataliwa katika baadhi ya  Taasisi za kifedha hivyo aliomba Mhe. Naibu waziri awasaidie wananchi hao.

Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo Mhe.Mabula amesema Hati za Kimila ni halali na kuna taasisi takribani saba zinazopokea hati hizo ambapo aliahidi kuwa Wizara ya Ardhi inaendelea kufanya mazungumzo na Taasisi nyingine za kifedha ili ziweze kuzitambua.

Wakati huo huo Mhe. Mabula amesema Halmashauri ihakikishe inapima maeneo yote Taasisi za Serikali na kutoa hati miliki kwa taasisi hizo ili kuepuka uvamizi utakaopelekea migogoro katika Serikali na wananchi.

Naibu Waziri aliongeza kuwa baada ya kupima maeneo hayo ya Taasisi za Serikali Wenyeviti wa mitaa na vijiji wapewe ramani  za maeneo husika ili wayalinde dhidi ya uvamizi na ujenzi holela.

Sambamba na hilo Mhe. Mabula amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Halmashauri itaandaa utaratibu wa kuyajengea uwezo mabaraza ya Vijiji na Kata ili yashughulikie vema mashauri mbalimbali ya Ardhi kwa wakati na kuepuka kuliongezea mzigo Baraza la Ardhi la Wilaya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Maswa, Mhe. Mdimi Ilanga alisema amekuwa akipokeabaadhi ya  kesi ambazo zingeweza kufanyiwa kazi na Mabaraza ya kata hivyo endapo wajumbe wa mabaraza hayo watajengewa uwezo watasaidia kushughulikia kesi hizo.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo alitembelea Wilaya ya Busega, Bariadi na Maswa na kuzungumza na Watalaam wa Ardhi wa mkoa huo, kutembelea maeneo ambayo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajia kujenga nyuma na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.Tuesday, November 15, 2016

RC SIMIYU: WAMILIKI BODABODA MADEREVA WENU WAPEWE MAFUNZOMkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wakazi wa Bariadi Mkoani humo wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka na viongoi wengine wa Mkoa huo wakipokea maandamano ya madereva na watumiaji wengine wa barabara wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Baadhi ya madereva wa bodaboda na bajaji wakiwa katika maandamano na wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani)  wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani alipotembelea banda wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Usalama barabarani alipotembelea banda la kamati hiyo wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka akipata maelezo kutoka kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto alipotembelea banda la Jeshi hilo wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Waimbaji wa Kwaya ya AICT Bariadi Mjini wakiimba wimbo maalum wenye ujumbe wa Usalama Barabarani wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi SOMANDA B wakionesha igizo wakati wa sherehe za maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Baadhi ya wananchi wa Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka alipowahutubia wakati uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Usalama Barabarani Mkoani humo mara baada ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Usalama Barabarani Mkoani humo mara baada ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi, (wa tatu kuia) Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa Edson Mwakiaba.
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Simiyu, Edson Mwakiaba akiwasilisha taarifa ya Mkoa ya Usalama wakati uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo mara baada ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Usalama barabarani mara baada ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. AnthonyMtaka akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo na Waimbaji wa kwaya ya Kanila la AICT Bariadi.

                                                     Na Stella Kalinga
Katika kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani, wamiliki wa bodaboda wametakiwa kuhakikisha madereva wanaowakabidhi pikipiki wamepata mafunzo ya uendeshaji na usalama barabarani

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka wakati wa uzinduzi wa wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani uliyofanyika kimkoa mjini Bariadi  mkoani humo.

Mtaka amesema wamiliki wa bodaboda wanapaswa kutambua kuwa hiyo ni fursa kiuchumi hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kuwa wanawakabidhi pikipiki watu wenye ujuzi ambao watazilinda dhidi ya uharibifu unaoweza kusababishwa na ajali zisizo za lazima.

“Wamiliki wa bodaboda mnawekeza fedha nyingi katika kununua bodaboda lakini wengi wenu mnawakabidhi madereva ambao  hawana mafunzo na wanakuwa sababu ya ajali za barabarani. Hakikisheni wamepewa mafunzo na ambao hawana wasaideni wapate ili kuepuka kupoteza pikipiki zenu na nguvu kazi ya Taifa kwa ajali ambazo siyo za lazima”alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amewataka madereva wanaoendesha bodaboda kuheshimu kazi hiyo kwa kuwa inawapatia kipato hivyo wanapaswa kujifunza na kuzingatia matakwa ya sheria za usalama barabarani.

Akisoma taarifa ya Hali ya Usalama Barabarani Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Simiyu, ASP.Edson Mwakihaba amesema katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Desemba 2016 jumla ya ajali 111 zimetokea mkoani humo ambazo zimesababisha watu 71  kupoteza maisha na wengine 39 kujeruhiwa.

 ASP Mwakihaba amesema vyanzo vya ajali hizo ni elimu duni kwa waendesha bodaboda ambao wanabeba abiria bila kupata mafunzo na kutovaa kofia ngumu, matumizi yasiyo sahihi ya vyombo vya moto katika kubeba mizigo ya hatari na kuzidisha uzito ulioruhusiwa, ubovu wa barabara na vyombo vya usafiri,ukosefu wa maegesho na makosa ya kibinadamu.

Vyanzo  vingine ni pamoja na kukosekana kwa alama za barabarani,mapungufu ya sheria ya salama barabarani ambayo makosa mengi hayaendani na viwango vya adhabu, kukosekana kwa vyuo vya kutolea elimu kwa madereva na magari mengi ya minadani kuchanganya abiria na mizigo.

Mwakihaba amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikana na wadau mbalimbali limejiwekea mikakati mbalimbali katika kukabiliana na ajali za barabarani ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa watumia vyombo vya moto na wananchi kwa ujumla juu ya sheria za usalama barabarani, kukagua madereva na vyombo vya moto kabla ya safari.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka imelitaka Jeshi la Polisi Kikosi cha Barabarani kutowaruhusu madereva kuendesha magari ya abiria  wanapogundulika kuwa na kilevi pale wanapopimwa kabla ya kuendesha vyombo vyao.

Sambamba na hilo Mkuu huyo wa Mkoa amelitaka jeshi la Polisi Kikosi cha usalama Barabarani kuwapima madereva wa bodaboda na bajaji hususani wale walio katika miji mikuu ya wilaya badala ya kujikita kwa madereva wa magari pekee.


Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Mwaka 2016 ni“Hatutaki ajali,tunataka kuishi”  na hii ni mara ya nne tangu kwa maadhimisho haya kufanyika mkoani Simiyu tangu kuanzishwa kwake.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!