Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Taifa
Kheri James amewaasa viongozi wa dini ,chama na Serikali
kutotofautiana lugha kuhusu haki za wananchi katika kukomesha dhuluma na pia
wawakemee wanaokwamisha juhudi za Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi.
James amesema hayo katika futari
iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka katika viwanja vya ofisi
ya mkoa, na kuhudhuriwa na waumini wa Dini ya Kiislamu wakiongozwa na Shekh
Mahamudu Kalokola ,viongozi wa madhehebu mbalimbali na viongozi wa chama na
serikali ,ikiwa ni desturi yake kila mwaka kujumuika pamoja katika kipindi cha mfungo
mtukufu wa Ramadhan.
“Maendeleo
yanayofanywa sasa ni kwa ajili ya watu wote sisi kama viongozi tunao wajibu wa
kushiriki ili tuweze kuhakikisha kuwa yanafikiwa kwa wakati, viongozi wa dini,
chama na Serikali tusitofautiane lugha katika kutetea haki za wananchi, tuhakikishe
tunasimamia wananchi wetu wanapata haki na dhuluma inakomeshwa” alisema James.
James
amesema viongozi wa madhehebu ya dini wana mchango mkubwa kwa Serikali katika kuhimiza maendeleo kupitia
makanisa na misikiti ,hivyo ni vema kuendelea kuliombea taifa kudumisha amani
pasipo kutofautiana na chama na Serikali.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amewashukuru viongozi wa dini kwa namna
wanavyoshirikiana na Serikali katika masuala mbalimbali , huku akiwaomba kuendelea
kusaidia katika malezi ya watoto hasa katika mkakati wa mkoa wa kuinua kiwango
cha ufaulu madarasa la mitihani, ambapo Kidato
cha nne na darasa la saba wapo katika kambi za Kitaaluma.
“Watoto
wetu wa kidato cha nne na darasa la saba wako katika kambi za kitaaluma kwa
ajili ya kujiandaa na mitihani ya Taifa, sisi kama Serikali tumetoa nafasi ya
kama nusu saa kwa watoto kushiriki ibada kila siku katika kambi hizo, tunaomba
viongozi wetu wa dini mfike kwa ajili ya kuwausia na kuwasisitiza kusoma kwa
kuwa tunahitaji watoto wetu wafanye vizuri “ alisema.
Shekhe
wa Mkoa wa Simiyu Mahamudu Kalokola ameishukuru
Viongozi wa Serikali Mkoani humo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka
kwa namna wanavyoshirikiana na Madhehebu yote ya dini naye akaahidi kuendelea
kushirikiana na Serikali katika Nyanja
mbalimbali za maendeleo.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi ambaye yupo SIMIYU na viongozi wa
vikundi vya vijana Kongwa kwa lengo la kujifunza Simiyu ilivyofanikiwa kwa
miradi ya vijana, akiwa katika futari hiyo amesema Simiyu imejipambanua vema katika masuala ya vijana
hususani katika uzalishaji mdogo mdogo jambo ambalo liwawafanya waje kujifunza
ili waweze kuwasaidia vijana wa Kongwa kuanzisha miradi endelevu na yenye tija.
MWISHO
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitambulisha viongozi na makundi ya
watu mbalimbali walioshiriki futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka kwa ajili ya Viongozi wa Dini,
Waumini wa Kiislamu, Viongozi wa Chama
na Serikali Mkoani humo, Mjini Bariadi.
Kutoka
kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana UVCCM Taifa Kheri James wakifurahia jambo baada ya shughuli
fupi ya futari iliyoandaliwa na Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa
ajili ya Viongozi wa Dini, Waumini wa Kiislamu, Viongozi wa Chama na Serikali Mkoani
humo, Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi akizungumza na Viongozi wa Dini, Waumini
wa Kiislamu, Viongozi wa Chama na Serikali
Mkoani Simiyu, baada ya shughuli fupi ya futari
iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa
makundi tajwa Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na Viongozi wa Dini, Waumini wa Kiislamu, Viongozi wa Chama naSerikali Mkoani
Simiyu,baada ya shughuli fupi ya futari iliyoaandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa Mjini
Bariadi, kwa ajili ya makundi tajwa.
Baadhi
ya Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Simiyu wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa
ajili ya Viongozi wa Dini, Waumini wa Kiislamu, Viongozi wa Chama na Serikali Mkoani
humo, Mjini Bariadi
Baadhi
ya Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja
wa Vijana UVCCM Taifa Kheri James wakati wa shughuli ya futari iliyoandaliwa na
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
kwa ajili ya Viongozi wa Dini, Waumini wa Kiislamu, Viongozi wa Chama na Serikali Mkoani
humo, Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Simiyu wakipata futari
iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa ajili ya Viongozi wa Dini, Waumini wa Kiislamu, Viongozi wa Chama na Serikali Mkoani
humo, Mjini Bariadi.