Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana
kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na
hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.
Jenerali Mabeyo ametoa ushauri
huo wakati alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Juni 07, 2018.
Mabeyo amesema vyombo vya habari
vinapaswa kuwahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze
kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri na hivyo waondokane na dhana ya
kuajiriwa .
“Vijana tunaowachukua JKT ni kwa
ajili ya kuwapa elimu na stadi za kazi ili hata kijana akikosa nafasi katika
vyombo vya Ulinzi na Usalama anaweza kurudi kijijini akafanya vitu vya
maendeleo, mimi nadhani watu wanahamasishana vibaya kuwa kila anayekwenda JKT
lazima aajiriwe, ipo haja ya kubadili
mtazamo” alisema Jenerali Mabeyo
“Jeshi linachukua vijana elfu
ishirini kwa mafunzo, wanaochukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama hawazidi
vijana 2000 sasa hawa wengine 18,000 wanaenda wapi, kama mawazo yatakuwa ni kwenda
JKT ili kuajiriwa hatutafanikiwa lakini kama watakwenda JKT kujifunza stadi za
kazi kuwasaidia ili ziwasaidie kujiajiri na kubadili maisha yao tutafanikiwa
sana” alisisitiza
Katika hatua nyingine Jenerali
Mabeyo ametoa pongezi kwa juhudi
zinazofanywa na Mkoa wa Simiyu katika mkakati wa Kilimo cha Umwagiliaji ili
kuwa na ziada ya chakula cha kutosha.
“Suala la umwagiliaji halikuwepo
katika fikra za watu wengi, walio wengi wanategemea mvua na isiponyesha
hawalimi na maisha yanakuwa duni wanaanza kuilalamikia Serikali, lakini sisi hapa
tunayo maji ya Ziwa Victoria, Mkuu wa Mkoa nawapongeza sana kwa juhudi
zinazofanywa katika kilimo cha Umwagiliaji, zitasaidia kuwatoa wananchi kwenye
ufukara” amesema Mabeyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Anthony Mtaka amesema mkoa huo umeweka malengo ya kujitosheleza kwa chakula na
kupitia mkakati wa kuwa na mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Mwamanyili
wilayani Busega, ambapo amebainisha kuwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo imeahidi
kutoa shilingi bilioni 12kwa ajili ya mradi huo.
“ Lengo letu kama mkoa ni
kuifanya wilaya ya Busega kuwa eneo ambalo linafanya vizuri katika kilimo cha
umwagiliaji kwa kuwa lina maji ya uhakika ya Ziwa Victoria, Benki ya Kilimo
wameahidi kutupa shilingi bilioni 12 kwa ajili ya mradi wa Kilimo cha
Umwagiliaji wa Mwamanyil” alisema Mtaka.
Akizungumzia suala la elimu Mtaka
amesema mkoa huo umejipanga kiushindani ambapo madarasa ya mitihani. yatakuwa na
makambi ya kitaaluma ambazo
zitawakutanisha wanafunzi kwa ajili ya kupitia maeneo yaliyo magumu ili waweze
kujiandaa na mitihani ya Kitaifa.
Mkuu wa Majeshi nchini,
Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati
alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Ofisini kwake Juni 07,
Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akitoa taarifa fupi
ya mkoa kwa Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo (kulia) wakati alipomtembelea ofisini kwakeJuni 07,
2018 Mjini Bariadi na kuzungumza na Kamati ya Ulinzi n aUsalama ya Mkoa.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maafisa wa Jeshi walioongozana na Mkuu wa Majeshi hapa Nchini
wakati alipomtembelea Mkuu wa mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu huyo majeshi Mjini Bariadi alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akimtambulisha Mkuu
wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo viongozi mbalimbali wa mkoa huo
waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili mjini Bariadi Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa
nchini Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.
Festo Kiswaga mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi wakati alipomtembelea Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa
nchini Jenerali Venance Mabeyo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi Mkoani Simiyu Juni 07, 2018,(kulia) Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mkuu wa Majeshi hapa
nchini Jenerali Venance Mabeyo ( wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa
wa Simiyu mara baada ya kumaliza mazungumzo
na viongozi hao Mjini Bariadi, ,Juni 07, 2018.
Baadhi ya Wajumbe wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maafisa wa
Jeshi walioongozana na Mkuu wa Majeshi hapa
Nchini wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka Mjini Bariadi, wakimsikiliza Mkuu huyo
majeshi Bariadi alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu.
Kutoka kushoto Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga, Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali
Venance Mabeyo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakifurahia jambo wakati Mkuu huyo wa Majeshi
alipomaliza kuzungumza na viongozi wa Mkoa huo Mjini Bariadi Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa
nchini Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Simiyu, ACP Boniventure Mushongi mara
baada ya kuwasili Mjini Bariadi Mkoani
Simiyu Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa
nchini Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka wakiteta jambo baada ya Mkuu huyo
wa Majeshi kuzungumza na viongozi Mkoani humo Juni 07, 2018.
0 comments:
Post a Comment