Viwanda, Biashara na Uwekezaji


SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOA WA SIMIYU

Sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Simiyu inashughulika na shughuli mbalimbali zinazohusu Viwanda, Biashara, Masoko na Uwekezaji kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Biashara, Sera ya Taifa ya Uwekezaji, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2011/12-2015/16, Mkakati wa Kupunguza na Kuondoa Umasikini Awamu ya Pili (MKUKUTA II) na Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda 1996-2020.

Shughuli zinazofanywa ni kusimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweza kufanikisha Sera, Sheria na Mipango mbalimbali ya kitaifa, kusimamia utekelezaji wa Sheria za Biashara na Viwanda, Kutoa ushauri wa kibiashara kwa wadau mbalimbali, Kuratibu shughuli za usajili wa Leseni za Biashara, Kusimamia mwenendo wa Masoko, Kuhamasisha shughuli za Wajasiriamali, Biashara Ndogo, Kati na Viwanda Vidogo (SME’s), Kuhamasisha na kuvutia Uwekezaji katika maeneo ya Kilimo, Madini, Utalii na Viwanda hususani viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo.

1.    VIWANDA

   Idadi ya Viwanda vilivyopo katika Mkoa wa Simiyu
Mkoa wa Simiyu una takribani ya viwanda 14 ambavyo vingi vinajishughulisha na uchambuzi wa Pamba ghafi na usindikaji wa mafuta ya pamba mbegu. Pia kuna viwanda vidogo (mashine za usindikaji mazao) zaidi ya 1,021 vinavyojishughulisha na usindikaji wa mafuta yatokanayo na zao la Alizeti,  kukoboa na kusaga mazao ya mpunga na  mahindi. Ifuatayo ni orodha ya idadi ya viwanda vya kati na vidogo vilivyopo Mkoani Simiyu.

   Idadi ya Viwanda
IDADI YA VIWANDA VYA KATI NA VIWANDA VIDOGO MKOANI SIMIYU
Na.
HALMASHAURI
VIWANDA VYA KATI
VIWANDA VIDOGO
Aina ya uzalishaji
Aina ya uzalishaji/usindikaji
Pamba ghafi & mafuta
Mpunga
Mahindi
Mafuta
Jumla
1
MASWA DC
6
123
73
18
220
2
BUSEGA DC
3
70
165
0
238
3
ITILIMA DC
0
44
44
23
111
4
MEATU DC
1
20
60
13
94
5
BARIADI DC
1
71
199
4
275
6
BARIADI TC
3
31
56
7
97
JUMLA
14
359
597
65
1035
  Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (2016)

BIASHARA NA MASOKO

UTARATIBU WA KUTOA LESENI YA BIASHARA

Leseni ya Biashara
Hiki ni kibali maalum cha Serikali kinachotolewa kwa mfanyabiashara yeyote anapotaka kufanya biashara hapa nchini. Sheria ya Leseni za Biashara Na. 25 ya 1972 – Kifungu cha 3(a) kimeweka bayana kuwa, Kibali hicho maalumu kinaitwa Leseni ya Biashara. Kwa hiyo basi, kufanya biashara yoyote bila kuwa na kibali hiki ni kosa la jinai.

Ili Mwombaji Apate Leseni Ya Biashara Anapaswa Kumbatanisha Nyaraka Zifuatazo:
 • Nakala ya hati ya kuandikisha jina la Biashara au Kampuni (Photocopy of Certificate of Incorporation or Registration & Extract);
 • “Memorandum, and Articles of Association” ambazo zitaonyesha kuwa Kampuni imeruhusiwa kisheria kufanya biashara inayoombwa, pamoja na majina ya wamiliki wa kampuni, hisa zao na utaifa wao;
 • Uthibitisho wa uraia kwa kuwasilisha, nakala ya hati ya kusafiri nje ya nchi ya Tanzania au hati ya kusafiri katika nchi za Afrika Mashariki, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo (Affidavit) kuonyesha kuwa ni Mtanzania, na kama mgeni alete hati ya kuishi nchini daraja la kwanza (Residence Permit Class A).
 •  Endapo wenye hisa wote wapo nje ya nchi itabidi maombi yaambatane na hati ya kiwakili (Power of Attorney) ya kumpa mamlaka raia wa Tanzania, raia wa kigeni mwenye hati ya kuishi nchini daraja “A” au hati ya kufanya kazi nchini daraja “B” zinazoainisha kuwa anasimamia kampuni husika.
 • Nakala ya ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa kufanyia biashara (lease agreement, Title deed, Certificate of occupancy, e.t.c);
 •  Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi (Tax Payer Identification Number - TIN).
 • . Hati ya uthibitisho wa ulipaji kodi (Tax Clearance Certificate)


Utaratibu Wa Kupata Leseni:

 • Mamlaka za Serikali za Mitaa(Halmashauri) zinahusika na utoaji wa Leseni za Biashara ambazo zinatambulika kama Leseni za Biashara za kundi B(Makundi yameainishwa katika Sheria ya Fedha na. 2 ya mwaka 2014). Ili kupata Leseni inatakiwa ufike Halmashauri ambayo unataka kufanyia biashara yako na kuwasilisha maombi yako pamoja na kupata maelekezo mengine ya taratibu za usajili wa Leseni ya Biashara.
 • Jaza fomu ya maombi ya Leseni (TFN 211 ya 2004)
 • Ambatisha nyaraka kama ilivyoainishwa hapo juu kwa ajili ya ukaguzi (assessment) na kujulishwa kiasi cha ada cha kulipia;


 • Kwa biashara za Kundi A (Sheria ya Fedha na. 2 ya mwaka 2014), utapata maelekezo kutoka kwa Afisa Biashara aliyepo eneo lako na baada ya maombi yako kukubaliwa malipo yafanyike kupitia Benki ya CRDB mahali popote kwa kutumia Akaunti Namba 0150413356300; Jina Revenue Collection Trading Licence – MIT;
 • Kisha utafika Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo utawasilisha “pay in slip” ya Benki Barua na Fomu(TFN 211 ya 2004) kutoka katika Halmashauri yako ili kupata risiti halali ya Serikali na Leseni ya Biashara;


USAJILI WA MAKAMPUNI
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inatoa ushauri wa usajili wa Majina ya Biashara na Makampuni kwa kushirikiana na Taasisi ya Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA). Wananchi wote mnakaribishwa kupata ushauri wa usajili wa majina na makampuni ili muweze kuwa na biashara zinazotambulika kisheria ambayo itakuwezesha kupata masoko ya Kitaifa na Kimataifa katika Bidhaa na Huduma.Pia unaweza kwenda kwenda moja kwa moja kwenye wavuti ya BRELA kwa ajili ya kusajili Majina ya Biashara na Makampuni www.brela.go.tz

MASOKO
Mkoa wa Simiyu una masoko ya kila siku ya bidhaa katika kila Halmashauri, vilevile kuna masoko ya minada na magurio ipatayo 16 ambayo huendesha biashara ya uuzaji wa mifugo mbalimbali hasa ng’ombe, mbuzi na kondoo. Pia katika minada hiyo kuna magurio ambayo wafanyabiashara na wachuuzi huuza bidhaa na mazao mbalimbali.

Jedwali 5: Orodha ya Masoko ya Minada na Magurio
NO.
HALMASHAURI
JINA LA MNADA
SIKU YA MNADA KWA WIKI
1.
BARIADI
Dutwa
Alhamisi
2.
BARIADI MJI
Bariadi Mji
Jumanne
3.
BUSEGA
Nyang’hange
Jumapili
Mwasamba
Jumamosi
4.
ITILIMA
Migato
Jumapili
Laini
Jumatatu
5.
MASWA
Lalago
Jumatatu
Malampaka
Jumatano
Jija
Alhamisi
Senani
Jumamosi
Nyalikungu
Jumapili
6.
MEATU
Bukundi
Jumatano
Mwanhunzi
Jumapili
Sanga Itinje
Jumanne
Tindabulige
Alhamisi
Mwankali(Usiulize)
Jumatatu
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (2016)

HUDUMA ZA FEDHA NA MAWASILIANO
Huduma za Fedha na Mawasiliano katika Mkoa zinaongezeka kwa kasi na uhitaji wa huduma hizo ni mkubwa kutoka na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na idadi ya wahitaji kuongezeka hivyo Mkoa una watoa huduma za  fedha na mawsiliano kama wafuatao;
                             
                                      Huduma za Fedha na Mawasiliano
Na.
BENKI
HUDUMA ZA MIKOPO
MAWASILIANO
1.
CRDB
PLATNUM CREDITS
AIRTEL
2.
NMB
BAYPORT CREDITS
MPESA
3.
POSTA
SACCOS
TIGO
4.


HALOTEL
                                    Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (2016)

  UWEKEZAJI

Mkoa wa Simiyu umejaliwa maliasili nyingi ambazo zinatoa fursa mbalimbali za uwekezaji, fursa hizi zinapatikana katika maeneo ya maliasili na utalii, kilimo, mifugo, madini na uvuvi. Pia kuna miundombinu na maeneo yaliyotengwa kwaajili ya shughuli za sekta ya uwekezaji kama ifuatavyo:-
a)    Barabara: Mkoa unazo barabara za lami, changarawe na udongo zinazopitika mwaka mzima, Barabara za lami ni jumla ya kilomita 72 ambazo zinaunganisha Mkoa na barabara ya Mwanza-Musoma na kilometa 849.3 za changarawe.
b)   Reli: Mkoa una huduma za reli Malampaka wilyani Maswa, Usafirishaji wa abiria na mizigo unafanyika katika kituo cha Malampaka.
c)    Maeneo ya Viwanda:- Mkoa una maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda katika kila wilaya, pia eneo la ukubwa wa hekta 2000 zimebainishwa kwa ajili ya uwekezaji katika  Ukanda wa Usafirishaji Bidhaa Nje (EPZ) katika wilaya ya Bariadi.


Pakua(download) nyaraka, Fomu na taarifa mbalimbali1 comment:

 1. Tovuti ina maelezo yenye kujitosheleza kuhusu uwekezaji ndani ya mkoa wa Simiyu. Kama TRA hawajafungua ofisi ya mkoa basi juhudi zifanyike ofisi hiyo iweze kufunguliwa ili kurahisisha huduma kwa wafanya biashara na wananchi kwa ujumla.

  ReplyDelete

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!