Wednesday, July 14, 2021

MKUU WA MKOA AELEKEZA WATENDAJI KUPIMWA KWA MIKATABA AIDHA CHMT ITAKAYOSHINDWA KUSIMAMIA AFYA KUVUNJWA

Ku


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na Wadau wa Sekta ya afya 


 

Katibu Tawala Bi. Prisca Kayombo akiwatambulisha Viongozi Mbalimbali waliofuatana na mkuu wa mkoa 

                                        


                                        Wadau wa sekta ya afya wakijiandaa na kikao kazi








Wadau wakisikiliza mada wakati wa Kikao kazi

Kufuatia taarifa ya tathimini kuonesha usimamizi duni sekta ya Afya, RC Kafulila amelekeza kuandaliwa mikataba ya usimamizi kati ya RMO na DMOs,  RAS na DEDs na yeye mwenyewe RCs a DCs ili kuhakikisha wilaya na halmashauri zinasimamia sekta ya afya kikamilifu.  

Maelekezo hayo ameyatoa kufuatia tathimini ya usimamizi wa sekta ya afya kuonyesha kuwa kwa muda mrefu usimamizi wa Kamati za Afya Wilaya ( CHMT) ni dhaifu,  wakurugenzi na wakuu wa wilaya hawajawa na msukumo wa kutosha kuhakikisha usimamizi.

Aidha Mhe. Kafulila ameagiza KUVUNJWA kwa Kamati za usimamizi wa huduma ya Afya (CHMT)  itakayoshindwa kusimamia sekta ya afya katika halmashauri husika.  Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo kufuatia taarifa ya tathimini ya robo mwaka kuonyesha kuwa CHMT zote mkoani Simiyu kwa kipindi kirefu  zimekuwa na usimamizi dhaifu hata kusababisha vifo kizembe. 

Katika tathimini hiyo  Bariadi DC ilipata alama C, Busega D, Bariadi mji C, Meatu E , Maswa F huku Itilima ikipata F. Mhe.Kafulila ameelekeza kuwa katika taarifa ya oOktoba, halmashauri itakayopata chini ya alama B, basi CHMT husika itavunjwa na  wengine kuchukuliwa hatua za kiutumishi.

Mwisho

TANZANIA INAJENGA SGR KWA GHARAMA NAFUU- KAFULILA.

 


 Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo wakati wa kikao na Waandishi wa habari.


 
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Simyu wakiwa katia mkutano na waandishi wa Habari.

Kuanzia kulia Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo, Mkuu wa Mkoa Mhe. David Kafulila na Meneja Mradi  Ujenzi wa reli ya kisasa Mwanza- Isaka Eng. Machibya Masanja wakiwa katika kikao na waandishi wa habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.


Hayo ameleza jana RC KAFULILA wakati akifungua kampeni ya kuhamasisha uelewa wa wananchi kuhusu mradi wa SGR kipande cha Mwanza - Isaka( 341km), kitakachojengwa kwa gharama ya Tsh.3trn sawa na $1.3bn. 


Mhe.Kafulila amempongeza Rais kwa kuendeleza ujenzi huo kwa kasi zaidi na kusema kuwa gharama hii ni nafuu kulinganisha na Kenya na hata Ethiopia na hivyo inathibitisha usimamizi madhubuti wa fedha za Serikali.

 " Hii inazidi kuthibitisha ripoti ya jukwaa la kimataifa kuhusu uchumi- World Economic Forum 2019 kuonesha kwamba Tanzania ni nchi ya 29 katika nchi 186 duniani katika usimamizi thabiti wa matumizi ya fedha za umma".

 Mhe.Kafulila amesisitiza wananchi kujitokeza kwenye kampeni hiyo iliyoanza jana na itakamalizika  alhamisi ili kupata uelewa zaidi wa mradi. Amewahakikishia fidia kulipwa kwa mujibu wa sheria na zaidi kuwaomba wachangamkie fursa za biashara wakati wa ujenzi hususan eneo la Malampaka ambapo kambi kubwa ya ujenzi zinajengwa. Amesisitiza Shirika la reli kutoa upendeleo kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Simiyu kwa kazi ambazo zipo ndani ya uwezo.

Mwisho
Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!