Thursday, December 17, 2020

RC SIMIYU ASITISHA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI MGODI WA LUBAGA

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesitisha matumizi ya leseni 18 za uchimbaji madini katika mgodi wa Dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa wilaya ya Bariadi na Busega, mpaka pale zitakapotolewa ufafanuzi na Waziri mwenye dhamana ya madini juu ya uhalali wake katika uendeshaji wa shughuli za madini.

 

Mtaka ametoa uamuzi huo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika eneo la mgodi Desemba 17, 2020 akiwa amefuatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kwa ajili ya kwenda kusikiliza kero za wachimbaji wadogo mgodini hapo na kuzitafutia ufumbuzi.

 

“Sisi kama viongozi wa mkoa tunasitisha matumizi ya leseni za eneo lote hili, mpaka pale waziri mwenye dhamana atakapokuja kutoa ufafanuzi kwa wananchi, kwa sababu sheria inamtamka waziri kwenye kufuta leseni lakini sisi mkoa kwa tuliyoyaona hapa tunasitisha; kwa sasa  mgodi utaendelea kuwa chini ya usimamizi wa maelekezo ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa,” alisema Mtaka.

 

Aidha, Mtaka amesema Maafisa kutoka katika Ofisi zote zinazopaswa kutoa huduma kwa wachimbaji hao ikiwa ni pamoja na maafisa wa Soko la Madini kuanzia Desemba 18, 2020 watakuwa katika eneo la mgodi ili kuwapunguzia wachimbaji hao adha ya kufuata huduma mbali na eneo hilo huku akisisitiza wachimbaji hao wauze dhahabu kwa bei iliyopo sokoni.

 

Mtaka pia amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Bariadi na Busega kufanya tathmini ya mashamba yaliyoharibiwa na shughuli zinazoendelea katika eneo la mgodi ili wakulima hao waweze kulipwa fidia, huku akiwataka Wakurugenzi hao  pia kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa matundu ya vyoo yasiyopungua 12 kuimarisha hali ya usafi mgodini.

 

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa onyo kwa wachimbaji na watu wote wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji madini kujiepusha na utoroshaji wa dhahabu, kwamba  watakapobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutaifisha dhahabu hiyo.

 

Awali wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba na wamiliki wa maduara  waliwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye mgodi huo ambazo baadhi zilipatiwa ufumbuzi  na uongozi wa mkoa na baadhi zitashughulikiwa na Waziri mwenye dhamana ya madini.

 

“Usimamizi wa ukusanyaji wa mapato kwenye mgodi huu uimarishwe zaidi, ili Serikali ipate sehemu yake, wachimbaji na sisi tupate sehemu yetu na kila tozo au ushuru wanaotutoza wahakikishe wanatoa risiti za kielektriniki,” alisema Flugence Ekondo mchimbaji mdogo.

 

“Katika ugunduzi wa mgodi huu mke wangu alikuwa anapalilia mahindi akaokota jiwe, alivyolileta tulikuwa na wasiwasi nalo tukalipeleka mgodi wa Gasuma tukaambiwa ni dhahabu, hiyo ilikuwa tarehe 05/11/2020 kesho yake wachimbaji wakaanza kuchimba na mgao ukafanyika; binafsi nilijua hiyo itakuwa rashi itakayotunufaisha wachimbaji wadogo na jamii inayotuzunguka,lakini baadaye tukasikia kuna leseni tunaomba tusaidiwe na sisi tupate haki yetu kwenye mgao,” Ntimba Masalu mwakilishi wa wenye mashamba

 

Akitoa ufafanuzi kuhusu mgao, Afisa madini Mkazi wa Mkoa, Mhandisi. Oscar Kalowa amesema “katika mifuko 100 asilimia saba ni fedha ya serikali, wamiliki wa mashamba asilimia 15, msimamizi/mmiliki wa leseni asilimia 15 na mwenye duara husika anapata asilimia zinazobaki na huu ndiyo utaratibu unaohusika.”

MWISHO

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesitisha matumizi ya leseni 18 za uchimbaji madini katika mgodi wa Lubaga uliopo mpakani mwa wilaya ya Bariadi na Busega, mpaka pale zitakapotolewa ufafanuzi na Waziri mwenye dhamana ya madini juu ya uhalali wake katika uendeshaji wa shughuli za madini.

Baadhi ya wachimbaji wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa  Wilaya ya Bariadi na Busega, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipotembelea mgodi huo akiwa na viongozi wa Chama na Serikali mkoani humo Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia walioketi) akiwa na baadhi viongozi wa Chama na Serikali mkoani humo katika mkutano wake na wachimbaji wadogo (waliosimama) katika mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa  Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Kutoka kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mhe. Enock Yakobo,  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga wakiteta jambo  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

:-Afisa Madini Mkazi mkoa wa Simiyu, Oscar Kalowa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Majengo kilichopo Kata ya Dutwa wilayani Bariadi akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wengine wakielekea kwenye mkutano wa hadhara  uliofanyika eneo la Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Debora John mmoja wa wachimbaji wadogo  kwenye Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega katika mktano wa hadhara uliofanyika kwenye eneo hilo, Desemba 17, 2020.

Mmoja wa wachimbaji wadogo  kwenye Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega katika mktano wa hadhara uliofanyika kwenye eneo hilo, Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Festo Kiswaga  akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo katika eneo la mpaka wa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020


Baadhi ya wachimbaji wadogo katika mgodi wa dhahabu wa Lubaga uliopo mpakani mwa  Wilaya ya Bariadi na Busega, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipotembelea mgodi huo akiwa na viongozi wa Chama na Serikali mkoani humo Desemba 17, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wengine wakielekea kwenye mkutano wa hadhara  uliofanyika eneo la Mgodi wa dhahabu wa Lubaga  uliopo mpakani mwa Wilaya ya Bariadi na Busega, Desemba 17, 2020.

Wednesday, December 16, 2020

WAZIRI WA KILIMO PROF. MKENDA, NAIBU WAZIRI TAMISEMI DKT DUGANGE WANOGESHA RCC SIMIYU

 

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda na Naibu  Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange wameshiriki kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), ambapo walitumia fursa hiyo kuwasilisha masuala ya kilimo na afya kwa viongozi wa chama na serikali, wakuu wa Taasisi za Umma na binafsi, viongozi wa Dini na wadau wengine wa maendeleo.

 

Akizungumzia kuhusu kilimo cha zao la pamba katika kikao hicho kilichofanyika Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi Prof. Adolf Mkenda amesema Wizara ya kilimo itafanya mapitio ya  mifumo mbalimbali ya kitaasisi ili kuongeza tija katika  uzalishaji wa pamba kufikia lengo la kuzalisha tani milioni moja ndani ya miaka mitano ijayo.

Miongoni mwa mifumo aliyoibainisha Profesa Mkenda ni pamoja na mfumo wa kushughulikia pembejeo za kilimo huku akibainisha kuwa Wizara yake  inaendelea kufanya uchunguzi ili kuona kama uwezekano wa kuzalisha viuatilifu  nchini ili kupunguza uagizaji wa viuatilifu kutoka nje ya nchi na kuweza kudhibiti ubora wa viuatilifu hivyo.

“ Katika kufikia tija kwenye zao la pamba pia tunapitia upya na kwa haraka sana mfumo mzima wa kitaasisi wa kuzalisha na kugawa mbegu za pamba, utaratibu mpya hautakuwa umekamilika kwa kipindi hiki cha msimu huu, lakini tumekusudia na tumekubaliana tutafanya mapitio ili wakulima wapate mbegu bora kwa wakati,” alisema Profesa Mkenda.

Awali Kabla ya kuzungumza katika  kikao hicho Prof. Mkenda, wajumbe wa Kikao cha RCC waliwasilisha changamoto mbalimbali katika kilimo cha pamba ikiwa ni pamoja na tatizo la upungufu wa mbegu na mbegu kutowafikia wananchi kwa wakati.

“Kumekuwa na changamoto ya upungufu wa mbegu kwa wakulima, ninashauri ili mbegu ziwafikie wakulima wote na kwa wakati, makampuni yanayozalisha mbegu yazipeleke kwa Mkurugenzi ambaye ndiye mwenye wataalam wa kilimo wanaofahamu idadi ya wakulima na ukubwa wa maeneo wanayolima,” alisema Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Benson Kilangi.

“Pamoja na kutatua changamoto ya pamba, tunaomba serikali iajiri maafisa ugani  ili wananchi waweze kupata huduma za ugani na kuzalisha kwa tija,tutakapozalisha kwa tija tutapata mavuno mengi na mkulima atanufaika pamba yake, suluhisho la bei ya pamba ni kujenga kiwanda cha nguo mkoani Simiyu,” Mhe. Esther Midimu Mbunge Viti Maalum.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange ametoa rai kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Busega, Bariadi na Itilima kuanza kununua vifaa tiba kwenye Hospitali za Wilaya zilizojengwa kwa kutumia mapato ya ndani  huku akibainisha kuwa Serikali imetenga shilingi milioni 500 kwa kila hospitali kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.

Dkt. Dugange pia amesema katika miaka mitano ijayo Serikali ina mpango wa kujenga vituo vya kutolea huduma za afya takribani 655 huku akifafanua kuwa itaanza na ukamilishaji wa maboma yaliyojengwa na kwa nguvu za wananchi na kuomba Halmashauri kuweka mpango wa kuanza kukamilisha maboma hayo.

Dkt.Dugange amesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa mifumo ya ukusanyaji mapato  katika vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo amebainisha kuwa makusanyo yakiwa mazuri yatazipunguzia Halmashauri mzigo wa utegemezi kwa Serikali Kuu na wadau mbalimbali wa afya na kuwezesha vituo hivyo kujiendesha ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kununua dawa.

Akifunga kikao cha RRC Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewashukuru viongozi hao kushiriki katika kikao hicho, huku akitoa wito kwa viongozi wote wa Mkoa huo kuifanya elimu kuwa ajenda ya kudumu ya mkoa na ujenzi wa vyumba vya madarasa kuwa ni kipaumbele chao cha kwanza ili kila mwanafunzi aliyefaulu aweze kwenda shule.

MWISHO.

 

Waziri wa kilimo, Mhe. Profesa. Adolf Mkenda akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali, wakuuwa Taasisi za Umma na binafsi, viongozi wa Dini na wadau wengine wa maendeleo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu(RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali, wakuu wa Taasisi za Umma na binafsi, viongozi wa Dini na wadau wengine wa maendeleo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia kikao hicho  kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifunga kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu(RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe, Benson Kilangi akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu(RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akiwasilisha taarifa katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.
Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Leah Komanya akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) mkoa wa Simiyu, Mhe. Gungu Silanga wakiteta jambo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Busega  Mhe. Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Sheikh wa mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Mkoa wa Simiyu, Bw. Lameck Sendo akichangia hoja katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.


Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC), wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi
TANROADS SIMIYU KUTUMIA BILIONI 11.4 UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA

 

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Simiyu umepanga kutumia kiasi cha shilingi bilioni 11.4 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya matengenezo ya barabara na madaraja.

 

Hayo yamebainishwa na Meneja wa TANROADS mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent wakati akiwasilisha taarifa katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

 

“Bajeti iliyopangwa kwa mkoa wa Simiyu ni shilingi bilioni 11.44 na kuna ongezeko kidogo mwaka jana tulikuwa na bilioni 10.9; tumepanga kufanya kazi kwenye barabara zenye urefu wa kilomita 923.6 pamoja na madaraja mawili,” alisema Mhandisi Kent.

 

Kwa upande wake Mratibu wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Dkt. Eng. Philemon Msomba amesema katika mwaka wa fedha 2019/2020 TARURA imetengeza kilometa 690.31 za barabara huku bajeti ya mkoa ikiwa bilioni 5. 056 na katika mwaka wa fedha 2020/2021 TARURA imeingia mikataba 18 yenye jumla ya shilingi 3,048,528,759/=

 

Dkt. Msomba ameongeza  kuwa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 750 kimeidhinishwa kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ya Mwadobana na Ngashanda kwa mwaka wa fedha 2020/2021

 

Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Leah Komanya akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa amesema “Ninaiomba Serikali katika bajeti zijazo ipandishe hadhi kipande cha barabara ya Mwabuzo-Igunga, ili tuweze kuleta maana ya kuunganisha barabara hii katika kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya ya Meatu.”

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesisitiza usimamizi wa miradi ya barabara huku akiitaka TANROADS kuona uwezekano wa kutenga bajeti kwa ajili ya  ujenzi wa mzani wa kisasa katika eneo la Malampaka kwa kuwa ni eneo litakalopitiwa na reli ya kisasa (SGR).

 

TANROADS Mkoa wa Simiyu ina jukumu la kutunza na kuendeleza barabara zenye urefu wa kilometa 923.65 barabara kuu ikiwa ni kilometa 334.33, barabara za mkoa kilometa 521.62 na barabara moja ya wilaya yenye urefu wa kilometa 67.7; ambapo TARURA inahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya kilometa 4,038.16.

MWISHO

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Albert Kent akiwasilisha taarifa ya wakala huo katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 mjini Bariadi.

Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini  (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Dkt.Eng. Philemon Msomba akiwasilisha taarifa ya wakala huo katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga wakifuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 Mjini Bariadi.

Mbunge wa Maswa Mashariki, Mhe. Stanslaus Nyongo akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 mjini Bariadi.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika jana Desemba 15, 2020 mjini Bariadi.

Sunday, December 13, 2020

VIONGOZI, WANANCHI NA WADAU SIMIYU WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUKAMILISHA UJENZI WA MADARASA

 

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony Mtaka amewataka viongozi wa kisiasa kushirikiana pamoja na viongozi serikali na wadau wengine wa elimu katika kuhakikisha ujenzi wa madarasa unakamilika mapema, lengo likiwa kuhakikisha wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza wanapata madarasa ya kusomea.

 

Mtaka ameyasema hayo  Desemba 12,2020 kwenye kikao kazi cha mkoa cha kujadili uelekeo wa mkoa wa Simiyu katika kipindi cha miaka  mitano ijayo  (2020/2025 ) katika masuala mbalimbali ikiwemo afya,elimu,kilimo,viwanda na ajira kwa vijana, ambacho kimewashirikisha viongozi wa chama na serikali, ,wafanyabiashara ,viongozi wa dini ,taasisi za umma na binafsi na wadau wa maendeleo wa Mkoa, kilichofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu.

 

“Simiyu kipaumbele chetu cha kwanza ni elimu, nimekuwa nikiwaambia watu wa Simiyu tukitaka kushindana tusomeshe watoto, malizieni maboma ya madarasa watoto wapate mahali pa kusomea, kila mmoja abebe kwa uchungu jambo hili kuona madarasa yanakamilika lakini mkienda  kwenye mabaraza mkaanza kubishana hamtawasaidia wananchi,” alisema Mtaka

 

Aidha Mtaka ameongeza kuwa kwa maeneo ambayo yana madini pamoja na maeneo yanayonufaika na uhifadhii kama vile vijiji vya Makao, Mwangudo na vingine Wilayani Meatu, wananchi wasichangishwe badala yake asilimia zinazotolewa kwa ajili ya vijiji zielekezwe kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa.

 

Ameongeza kuwa mkoa huwa umejiwekea malengo ya kuongoza katika mitihani yote ya Taifa ambapo amewataka viongozi wa Serikali kuendelea kutoa motisha kwa walimu ikiwa ni pamoja na kuacha kutoa lugha za kuwaudhi na kuwakera walimu ili waendelee kufanya kazi kwa moyo.

 

Sambamba na hili Mtaka ametoa rai kwa Madiwani wote wa Mkoa huo kuacha tabia ya kuazimia watumishi wao kwa kuwa hali hiyo inawavunja moyo watumishi badala yake waweke mazingira ya watumishi kupenda kazi na ikiwa watumishi watafanya jambo lisilotakiwa wawasiliane na mamlaka nyingine ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu.

 

Katika hatua nyingine Mtaka amesema Simiyu Imejipanga kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa mikopo nafuu itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya ndani inayotolewa kwa vijana wanawake na walemavu, akibainisha kuwa fedha hizo zitatangazwa na kushindaniwa; ambapo vikundi havitapewa fedha badala yake Halmashauri zitalipia teknolojia zinazohitajika kupitia SIDO na sehemu ya fedha inayobaki itatumika kuwajengea uwezo wahusika wa vikundi hivyo.

 

Awali akitoa taarifa ya elimu mkoani hapo kwa niaba ya afisa elimu mkoa wa Simiyu , Jusline Bandiko  amesema mkoa huo una mahitaji ya vyumba vya madarasa 565 ,vilivyopo ni 419 huku  upungufu ukiwa vyumba 155 ambavyo vinatakiwa  kukamilika kwa ajili ya kidato cha kwanza 2021.

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simyu, Mhe. Enock Yakobo ametoa wito kwa viongozi kuona umuhimu wa kuanzisha mfuko wa elimu wa mkoa na kuwahamasisha wananchi kuchangia mfuko huo ili uweze kusaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na ununuzi wa viti na madawati.

 

Miriam Mmbaga ni Katibu Tawala wa Mkoa huo ametoa wito kwa viongozi wa Umma mkoani Simiyu kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo, sheria na taratibu na kwa uadilifu mkubwa wakijiepusha na masuala ya migongano ya maslahi katika maeneo yao, huku akisisitiza wafanye maamuzi sahihi kwa wakati sahihi kwa maslahi ya wananchi wanaowaongoza.

 

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James ambaye pia ni Mlezi wa CCM kwa mikoa ya Simiyu na Mara  amesema jamii inahitaji mageuzi ili kufikia mageuzi hayo inapaswa kuwa na viongozi wenye uthubutu na ujasiri, huku akitoa wito kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu kufanya kazi kwa ushirikiano na kutumia vizuri madaraka, mamlaka na ushawishi walio nao kwa manufaa ya wananchi wanaowaongoza.

MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi  pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu kwenye kikao kazi cha kujadili mwelekeo wa Mkoa katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana,  kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James akizungumza na wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi  pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu kwenye kikao kazi cha kujadili mwelekeo wa Mkoa  huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana,  kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.
Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika kikao kazi cha Mkoa wa Simiyu kilichowahusisha viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi  pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu kilicholenga  kujadili mwelekeo wa Mkoa  huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James wakati wa kikao kazi cha Mkoa kilichowahusisha viongozi wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi  pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu, kilicholenga  kujadili mwelekeo wa Mkoa  huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akiwasilisha mada katika kikao kazi cha Mkoa kilichowahusisha viongozi wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi  pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu, kilicholenga  kujadili mwelekeo wa Mkoa  huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha kikao kazi cha Mkoa kilichowahusisha viongozi wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi  pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu, kilicholenga  kujadili mwelekeo wa Mkoa  huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha kikao kazi cha Mkoa kilichowahusisha viongozi wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi  pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu, kilicholenga  kujadili mwelekeo wa Mkoa  huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi  pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu kwenye kikao kazi cha kujadili mwelekeo wa Mkoa katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James wakifurahia jambo wakati wa kikao kazi cha Mkoa kilichowahusisha viongozi wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi  pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu, kilicholenga  kujadili mwelekeo wa Mkoa  huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha kikao kazi cha Mkoa kilichowahusisha viongozi wa wa Chama na Serikali, viongozi wa wafanyabiasha, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za Umma na binafsi  pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu, kilicholenga  kujadili mwelekeo wa Mkoa  huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo(2020-2025) katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ajira, kilimo, viwanda na ajira kwa vijana, kilichofanyika Desemba 12, 2020 Mjini Bariadi.

TAZAMA PICHA NYINGINE KATIKA KIKOA KAZI HIKI CHA MKOA
Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!