Thursday, August 31, 2017

RC MTAKA: ZOEZI LA KUONDOA MIFUGO KWENYE MAENEO YA HIFADHI LIFANYIKE KWA WELEDI, HAKI NA UADILIFU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Meatu mkoani humo, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Dkt. Joseph Chilongani kutekeleza kwa weledi, uadilifu na haki zoezi la kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi litakaloanza September 04, 2017.

Mtaka ametoa kauli hiyo mara baada ya viongozi wa Serikali na Chama Mkoa na Wilaya, Wataalam, wafugaji na wadau wa uhifadhi na Utalii kukutana na kujadili suala la uondoaji mifugo katika Maeneo ya Hifadhi, yakiwemo ya  Pori la Akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) Makao wilayani Meatu.

“Mkafanye zoezi hili kwa weledi mkubwa na haki, lisije likawa zoezi la kuwaonea watu, kufanya utapeli kwa kujifanya mnachukua ng’ombe kwa ajili ya kutaifisha halafu mkagawana; viongozi na wote mtakaohusika mkalisimamie kwa makini sana suala hili” alisisitiza Mtaka
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe.Joseph Chilongani amesema baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi, wafugaji na wadau wa uhifadhi na utalii ametoa muda wa siku nne na kufikia Septemba 04 mwaka huu, wafugaji wawe wametoa mifugo katika maeneo ya hifadhi kwa hiari.

Dkt.Chilongani amebainisha kuwa Viongozi wa Wilaya ya Meatu walikutana na wafugaji katika maeneo yao na kuwatahadhalisha juu ya uingizwaji wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi, ili kuwasaidia waepuke adhabu ya kifungo na mifugo yao kutaifishwa kwa kuwa kuingiza mifugo hifadhini ni makosa kwa mujibu wa sheria.

“Maandalizi yote yako tayari, timu za kutekeleza zoezi hili zote zipo, nitoe muda wa siku hizi zilizobaki ili kufikia Jumatatu ya tarehe 04 zoezi la kuondoa mifugo kwenye Pori la Akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na WMA ya Makao lianze, tulishawapa wafugaji muda wa kutosha tulipokuwa tukipita kwenye vijiji kuzungumza nao juu ya madhara ya  kuingiza mifugo hifadhini” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Pori la Akiba la Maswa Lasato Masinde amezitaja baadhi ya changamoto za kuingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi kuwa ni ushindani wa malisho na maji kati ya wanyamapori na wafugwao,ongezeko la ujangili, kuuwawa kwa wanyamapori hasa walao nyama, magonjwa na mmonyoko wa udongo kutokana na wafugaji kukata miti.

Aidha, Masinde amefafanua kuwa suala la uingizwaji wa mifugo katika hifadhi linachangiwa pia na baadhi ya viongozi wa vijiji wasiokuwa waadilifu ambao hupokea fedha kwa wafugaji na kuwaruhusu kuingiza mifugo yao, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Meatu kuwachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wafugaji kupima maeneo yao wanayomiliki na kuyawekea miundombinu ya mifugo kama vile visima vya maji na mabwawa, majosho na mashamba ya malisho ili waweze kufuga kisasa na kuondokana na adha ya kuhangaika kutafuta maji na malisho.

Katika kikao hicho wafugaji kwa pamoja wamekubali kutoa mifugo katika maeneo ya  hifadhi na kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wa kupima maeneo yao na kuweka miundombinu, hivyo wameomba watalaam wa Ardhi na Mifugo waweze kuwasaidia namna wanavyoweza kutumia maeneo yao kufuga kisasa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani humo.
Baadhi ya viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Meneja wa Pori la Akiba la Maswa, Lusato Masinde akiwasilisha taarifa yake kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.

Katibu wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanayamapori ya Makao, Robert Simon akiwasilisha taarifa yake kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mhifadhi kutoka Ranchi ya MWIBA, Julius Makaroti  akiwasilisha taarifa ya ranchi hiyo kwa viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg.Donald Magesa akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwiburi akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mmoja wa wafugaji wa Wilaya ya Meatu akichangia hoja katika kikao kilichofanyika wilayani Meatu kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe.Pius Machungwa akichangia hoja katika kikao kilichofanyika wilayani Meatu kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao wilayani Meatu na ambaye pia ni mfugaji, Anthony Philipo akichangia hoja katika kikao kilichofanyika wilayani Meatu kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,Said Samba akifafanua jambo katika kikao kilichofanyika Mjini Mwanhuzi  kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.
Mhifadhi kutoka Shirika la Frankfoot, Sylevester Bwasama akifafanua jambo katika kikao kilichofanyika Mjini Mwanhuzi  kujadili suala la kuondoa mifugo katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao, Pori la Akiba la Maswa na Ranchi ya Mwiba wilayani humo.

Wednesday, August 30, 2017

WITO UMETOLEWA KWA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI VYUMBA VYA MADARASA

Wananchi  wa Kata ya Nkololo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wametakiwa kutambua wajibu wao katika kuchangia ujenzi wa Vyumba vya madarasa ili kupunguza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka wakati alipokuwa akijibu kero mbalimbali za wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nkololo Kata ya Nkololo Wilayani Bariadi.

Mtaka amesema ni vema wananchi wakahamasika kuchangia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kama wanavyochangia katika masuala mengine ili watoto wao wawe na mazingira mazuri ya kusomea.

“Kujenga vyumba vya madarasa siyo wajibu wa walimu wetu ni wajibu wenu wenu wazazi, ni lazima wananchi wa Nkololo mjenge vyumba vya madarasa kama mnavyojitoa katika mambo mengine, najua hamuwezi kushindwa kutoa angalau mfuko mmoja wa saruji kila kaya; Nkololo itajengwa na wana Nkololo wenyewe” amesema Mtaka.

Aidha, Mtaka ametoa wito kwa wananchi hao kuzingatia suala la uzazi wa mpango kwa kuwa ongezeko kubwa la watoto ndio linalopelekea idadi kubwa ya wanafunzi ikilinganishwa na vyumba vya madarasa.

“Mhe.Diwani nikuombe tengeneza utaratibu hapa na watu wako, Nkololo ni moja ya centre(kituo) kubwa wachangie, wala wasiseme tumechangia sana ni lazima wachangie; na kama hatutajirekebisha kwenye kuzaana, tutachanga, tutachanga, tutachanga” amesema Mtaka.

Naye Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Doreen Rutahanamilwa amesema, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya elimu vikiwemo vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo, hivyo wananchi wanao wajibu kuunga mkono jitihada hizo ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.

Kuhusu kero ya uharibifu wa mazao unaofanywa na wanyamapori hususani Tembo, ambayo ilitolewa na Luja Masala Mkazi wa Kijiji cha Bubale, Mkuu huyo wa Mkoa amesema, Serikali kupitia watalaam wake wa Wanyamapori watakabiliana na tatizo hilo, hivyo akawataka wananchi wasiache kulima na wazingatie ushauri wanaopewa na watalaam hao.

Akitoa ufafanuzi wa kitaalam juu ya kero hiyo, Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili, Ndg.Mazengo Sabaya amesema, Halmashauri imekuwa ikipeleka askari wa Wanyamapori katika maeneo yanayovamiwa na tembo na akawataka wananchi kuendelea kufuata ushauri wa kutumia uzio wa pilipili katika mashamba yao ili kuwazuia tembo hao.

Katika suala la upatikanaji wa mbegu bora, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka Serikali kupitia kwa wakala wa mbegu ina mpango wa kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora katika bei wanayoweza kuimudu.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa maelekezo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kuhakikisha inaweka mipango ya ujenzi wa stendi, soko na barabara katika kituo cha Nkololo ambacho ni moja vituo vikubwa vya kibiashara wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa ameanza ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi katika Kata ya Nkololo na baadaye atafanya ziara katika kata za Dutwa na Ngulyati ambapo atafanya mikutano ya hadhara na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Nkololo wilayani Bariadi (hawapo pichani) katika Mkutano wa Hadhara, wakati wa ziara yake aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kata ya Nkololo (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wilayani humo aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi
Luja Masala Mkazi wa Kijiji cha Bubale Kata ya Nkololo akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa ziara  aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na viongozi wengine wa Mkoa na Wilaya ya Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa ziara  aliyofanya katika Kata ya Nkololo wilayani Bariadi, kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili, Ndg.Mazengo Sabaya akitoa maelezo ya Kitalaam kujibu hoja za wananchi wa Kata ya Nkololo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wilayani Bariadi aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Doreen Rutahanamilwa akitoa maelezo ya Kitalaam kujibu hoja za wananchi wa Kata ya Nkololo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wilayani Bariadi aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Baadhi ya wananchi  wa Kata ya Nkololo wilaya ya Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka katika Mkutano wa Hadhara aliofanya katika Kata hiyo wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg. Donald Magesa akizungumza na wananchi wa Kata ya Nkololo (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka wilayani Bariadi, aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Yusufu Masunga Mkazi wa Nkololo akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa ziara  aliyofanya Kata ya Nkololo wilayani Bariadi kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Baadhi viongozi na Wataalam wa Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa ziara  aliyofanya katika Kata ya Nkololo wilayani Bariadi, kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Maduhu Kalimilo Mkazi wa Kijiji cha Ikungulyandili wilayani Bariadi akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa ziara  aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Baadhi ya wananchi  wa Kata ya Nkololo wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka katika Mkutano wa Hadhara aliofanya katika Kata hiyo wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Thursday, August 24, 2017

NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI KUTAMBUA MAENEO YASIYOENDELEZWA NA YASIYOMIKILIWA KIHALALI

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), ameziagiza Halmashauri nchini, kuyatambua na kuyatolea taarifa  maeneo yanayohodhiwa na watu bila kuendelezwa na yale ambayo hayakupatikana kihalali ili Wizara iweze kuchukua hatua stahiki.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, kisha Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyu kuanza ujenzi wa mradi wa maji katika eneo hilo utakaonufaisha vijiji vinne vya kata ya Lamadi.

Mhe.Mabula amesema Halmashauri zinapaswa kutambua maeneo yasiyoendelezwa na yanayomilikiwa kinyume cha sheria na kuwasilisha taarifa katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili yaweze kuyarejesha kwa wananchi na kupangiwa matumizi mengine yenye manufaa zaidi kwa jamii.

“Maeneo yote yaliyohodhiwa ambayo hayajaendelezwa na ambayo pengine hayakupatikana kihalali, ni jukumu la Halmashauri kuyatambua na  kuleta taarifa zake Wizarani ili Wizara iweze kuchukua hatua ya kuweza kuyarudisha katika matumizi kwa Umma na yaweze kufaidisha watu wengi zaidi badala ya mtu mmoja” amesema Naibu Waziri Angelina Mabula

Aidha,Naibu Waziri Mabula amebainisha sababu zilizopelekea Mwekezaji Hermati Pateli kufutiwa hati ya eneo hilo na Serikali kuwa ni udanganyifu wa Uraia pamoja na upatikanaji wa hati ambao haukuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Naibu Waziri huyo amesema eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji huyo isivyo halali ambalo limefutiwa hati miliki limegawanyika katika ploti mbili, ploti Namba 01 na Namba 02 Block C  lenye ukubwa wa hekta 7.62 na Block Namba 03 C hekta 5.45.

Akitoa maelezo kwa  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Maji wa Lamadi kutoka Kampuni ya EAU Consult, Baraka Felix amesema Tanki la Maji litakalojengwa katika eneo hilo litakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 3000 kwa siku.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya amesema Mradi wa  Maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo hilo utawanufaisha wananchi wa Vijiji Vinne vya Kalago, Lamadi, Lukungu na Mwabayanda.

Mradi huu wa maji unaojengwa katika eneo hili lililokuwa linamilikiwa isivyo halali na Mwekezaji Pateli, utagharimu kiasi cha Yuro milioni 2.8, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei, 2019.
Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali
Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea kuona Ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Lamadi itakayosimamia mradi wa maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)akizungumza na waandishi wa habari  katika mahojiano maalum mara baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya wakati alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Busega mara baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, (kushoto) Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Tano Mwera.

Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi hao Wilayani Busega(hawapo pichani).

WAKURUGENZI WATAKIWA KUSIMAMIA IDARA YA ARDHI KUHAKIKISHA INAPIMA MAENEO NA KUTOA HATI

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula  amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani Simiyu  kuwasimamia watumishi wa Idara ya Ardhi na kuhakikisha wanapima maeneo  na kutoa hati miliki kwa wananchi.

Mhe.Mabula ameyasema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu ambayo imelenga kufuatilia utekelezaji wa maelekezo mbalimbali aliyoyatoa wakati wa ziara yake Novemba 2017, mwenendo wa ukusanyaji wa kodi za ardhi na  kukagua Jengo la Kanda ya Ardhi Simiyu itakayohudumia Mikoa ya Simiyu,Shinyanga na Mara,

“Mtumishi aliyeajiriwa kama surveyor (mpima ardhi) hana sababu za kukaa ofisini kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 9:30 alasiri wakati kazi zake nyingi ziko uwandani; Mwisho atajikuta amepima viwanja 58 mwaka mzima, maana yake ni kwamba atakuwa hajajua wajibu wake, wakurugenzi badilikeni katika kuwasimamia watumishi wa sekta ya ardhi” amesema Mabula

Amesema ikiwa Watumishi wa Idara ya Ardhi wakitimiza wajibu wao Ardhi ikapimwa, wananchi wakapewa hati miliki ya maeneo yao ya viwanja na mashamba;  migogoro itapungua, Serikali itakusanya maduhuli kupitia kodi ya Ardhi na uendelezaji wa miji utafanyika katika mpango mzuri

Pamoja na kupima maeneo na kutoa hati miliki, Mhe.Naibu Waziri amesema Idara ya Ardhi inapaswa kuhakikisha wananchi waliomilikishwa maeneo wanajenga kwa kuzingatia sheria Namba 8 ya mwaka 2007 ya Mipango Miji, ili kuepukana na ujenzi holela unaopelekea kuwa na miji isiyopangwa.

Aidha, Mhe.Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, amesisitiza maeneo yote ya Taasisi za Serikali yapimwe na kutolewa hati miliki ili kuyalinda na uvamizi.

Sanjali na hilo, Mhe.Naibu Waziri amewataka wataalam wa Ardhi kukusanya maduhuli ya Serikali yatokanayo na kodi za ardhi kwa kutumia mifumo ya Kielektroniki iliyowekwa katika kufuatilia na kuhakikisha wananchi wote wanaostahli kulipa kodi ya ardhi wanalipa kwa wakati.

Naibu Waziri ameelekeza Kamati za Halmashauri zinazosimamia Ardhi zihakikishe zinaifanya agenda ya Makusanyo ya maduhuli kuwa ya kudumu katika vikao vyao vya kila robo, ili kila wanapokutana itolewe taarifa ya hali ya makusanyo, wananchi waliopewa notisi na wale wanaotakiwa kupelekwa katika mabaraza ya Ardhi ya Wilaya kwa kushindwa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati.

Akiwasilisha taarifa ya Wilaya ya Bariadi Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Festo Kiswaga amesema Halmashauri zote mbili zinazounda Wilaya ya Bariadi zinaendelea na kuhamasisha wananchi kupima maeneo yao na kupata hati miliki ili kuongeza ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali kupitia kodi ya Ardhi, ambapo Halmashauri ya Wilaya Bariadi pekee kwa mwaka 2017/2018 inatarajia kupima viwanja 2400 katika Vituo vya Kibiashara vya Nkololo,Dutwa na Ngulyati.

Naye Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Kanda, Makwasa Biswalo amesema Mtalaam kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amefika Mkoani Simiyu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji wa kodi za Ardhi,  kwa watumishi wa Halmashauri zote ambao utawawezesha kutengeneza ankara (bill) ya makusanyo ya kodi na tozo zote.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshukuru Wizara ya Ardhi kwa kuona Umuhimu wa kuanzisha Kanda ya Ardhi ya Simiyu na akaomba Wizara ifanye utaratibu wa kumleta Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Maswa kutokana na aliyekuwepo kasimamishwa kazi, hali iliyopelekea mashauri mengi kutofanyiwa kazi.

Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses amesema kuanzia mwezi Septemba 2017 atakuwepo Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Maswa  ambaye atasikiliza kesi, ambapo pia ameleeza kuwa Wizara ina mpango wa kuanzisha mabaraza mawili ya Ardhi na Nyumba katika Wilaya ya Bariadi na Busega ambayo yataanzishwa muda wowote baada ya kupatikana majengo kwa ajili ya Ofisi.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) yuko katika ziara ya siku mbili Mkoani Simiyu ambapo akiwa Mjini Bariadi amefanya kikao na  Viongozi, wataalam wa Ardhi na Watendaji wa Kata,Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Mji Bariadi na Halmashauri ya Wilaya Bariadi kilichofanyika Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) (wa pili kushoto)akizungumza na viongozi, watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Bariadi(kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) kuhusu jengo lililoandaliwa kwa ajili ya Ofisi ya Ardhi Kanda ya Simiyu ambayo inatarajia kuanza kazi hivi karibuni, ambayo itahudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)azungumze na Viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Bariadi(hawapo pichani) kabla ya kuanza ziara yake Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)azungumze na Viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Bariadi(hawapo pichani) kabla ya kuanza ziara yake Mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akiwaasilisha taarifa ya Wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto)wakati akiwa katika Ziara ya siku Mbili Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa mji wa Bariadi, Ndg.Melkizedek Humbe akichangia hoja katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb), viongozi, watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi, kilichofayika mjini Bariadi  wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo  Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa mji wa Bariadi, Ndg.Melkizedek Humbe akichangia hoja katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb), viongozi, watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi, kilichofayika mjini Bariadi  wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo  Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa mji wa Bariadi, Ndg.Melkizedek Humbe akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) wakati alipotembelea Ofisi ya Idara ya Ardhi ya Halamashauri hiyo kujionea namna inavyokusanya mapato yatokanayo na Ardhi, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi hao mjini Bariadi.
Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Kanda, Makwasa Biswalo akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi hao mjini Bariadi.
Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Kanda, Makwasa Biswalo akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi hao mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)  kuhusu eneo la uwanja wa ndege wa Kidulya lililokuwa limevamiwa na mwananchi mmoja na namna Serikali ilivyolishughulikia, wakati alipolitembelea eneo hilo akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Melkizedek Humbe(kulia) akimweleza  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)  hatua zilizochukuliwa na Halmashauri dhidi ya mwananchi aliyevamia eneo la uwanja wa ndege Kidulya, wakati alipolitembelea eneo hilo akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji, Ndg.Speratus Boniphace akichangia hoja katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi, kilichofanyika Mjini Bariadi wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo Mkoani Simiyu.

Baadhi ya watumishi wa Idara ya Ardhi Mkoa na Wilaya na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea eneo la Uwanja wa Ndege wa Kidulya Mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Mtaalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Ndg. Martha Zongo hoja katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi wa Idara ya Ardhi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Wilaya ya Bariadi, kilichofanyika Mjini Bariadi wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Msaidizi ehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu wa Sekretarieti ya Mkoawa Simiyu(ambaye alimwakilisha Katibu Tawala Mkoa) akiwatambulisha viongozi na watumishi mbalimbali walioshiriki katika ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bariadi na baadhi ya wataalam wa Ofisi ya Ardhi Kanda ya Ziwa wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Mji Bariadi, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb)(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja wakuu wa idara wa Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Bariadi, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!