Friday, December 31, 2021
Salamu za Mwaka Mpya- RC KAFULILA
Tuesday, December 28, 2021
RC KAFULILA ALIA NA KAMPUNI YA UJENZI YA CHICCO .
Aliyesimama ni Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga akichangia jambo, Kushoto Mbunge wa Vijana Mkoa wa Simiyu Mhe.Lucy Sabu. Kulia Mbunge wa Maswa Mashariki Mhe. Stanlaus Nyongo. |
Aliyesimama Mbunge wa Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo, akichangia hoja , aliyekaa kulia Mbunge wa Meatu, Mhe.Leah Komanya |
Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa,Eng.John Mkumbo, akitoa taarifa ya Mtandao wa Barabara na jinsi ujenzi wa barabara unavyoendelea mkoani Simiyu, kwenye kikao cha barabara kichofanyika leo mjini Bariadi |
Akizungumza leo kwenye kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi,amesema kuwa atawasiliana na Waziri wa ujenzi na Uchukuzi, Mhe.Prof. Makame Mbarawa kupata maelezo kuhusu uhalali wa kampuni ya Ukandarasi wa Barabara CHICCO kupewa kandarasi ya ujenzi huo.
Amesema kampuni hiyo awali ilipewa kandarasi ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa Km 57 kutoka Mwighumbi hadi Maswa kwa gharama ya Sh Bilioni 75 lakini wakajenga chini ya kiwango na kutakiwa kuirudia upya kipande cha barabara chenye urefu wa Kilomita 15.Mwisho.
RC.Kafulila alibaini kujengwa kwa kiwango cha chini barabara hiyo mara baada ya kutembelea ujenzi huo Mwezi Juni mwaka huu na kuagiza maeneo yote ambayo ujenzi haukukidhi viwango kurudiwa na hadi sasa mkandarasi anaendelea na kazi ambayo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.Mwisho.
Thursday, December 23, 2021
WAKANDARASI TEKELEZENI MIRADI YA MAJI KWA UADILIFU NA KWA WAKATI-RC KAFULILA
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na washiriki wa hafla ya kusaini mikata 24 ya RUWASA,.Kulia KUU ya Mkoa na baadi ya wafanyakazi wa RUWASA Simiyu |
Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga akichangia jambo |
Mwenyekiti wa chama cgha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed akisisituiza jambo wakati wa hafla ya kusaini mikataba 24 ya RUWASA |
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria akichangia hoja |
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faiza Seleman alichangia hoja kulia kwake,ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge |
Wakandarasi na Local Fundi wakisikiliza yanayojiri wakati wa hafla ya kuaini mikataba 24 ya RUWASA |
Wednesday, December 22, 2021
MIKOA YOTE IGENI SIMIYU MIKATABA YA UWAJIBIKAJI
Naibu Waziri- TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange, leo amepongeza Mkoa wa Simiyu kwa ubunifu wa kuanzisha mikataba ya uwajibikaji ambapo Mkuu wa Mkoa David Kafulila amesaini na wakuu wote wa wilaya na kisha Katibu Tawala Mkoa kusaini na wakurugenzi wote wa Halmashauri ambao nao wamesaini na wasimamizi wa sekta ya afya ngazi ya wilaya mpaka vijiji kwa lengo la kupima ufanisi wa kila Kiongozi na mtendaji kuanzia ngazi ya mkoa ( performance contract ) na kutaka mikoa mingine kuiga ili kuongeza tija katika usimamizi majukumu ya Serikali.
Naibu waziri amesema hayo baada ya kupokea taarifa ya Mkoa wa Simiyu leo kuhusu masuala ya elimu na afya katika ziara yake ya siku moja mkoani simiyu, ambapo imelezwa kuwa ndani ya nusu mwaka mifumo ya ya mapato GOTHOMICS imeboreshwa na kusababisha ongezeko la mapato kwa asilimia zaidi ya 300%, kutoka makusanyo ya takribani milioni 200 mpaka zaidi ya milioni 600.
Aidha mafanikio makubwa ktk usimamizi wa afya za lishe hata kufikia asilimia 92 mwezi Novemba , kiwango ambacho kinategemea kuipaisha simiyu katika tathimini ijayo itakayofanyika Januari 2022. " kwa ufanisi wa asilimia 92% sasa ni wazi tathimini ijayo Januari mkoa utakuwa 3 bora kutoka nafasi ya 23 kitaifa katika tathimini ya mwisho alisisitiza Kafulila. Mwisho.
Mikoa yote igeni Simiyu Uwajibikaji- Naibu Waziri TAMISEMI( Afya)
Wito huo umetolewa leo na Mhe.Dkt.Festo Dungage- Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serilkali za Mitaa (TAMISEMI-AFYA), mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19 Mkoa wa Simiyu.
Mhe.Dugange,amepongeza Sekreta
"Hongera kwa kazi nzuri sana mnayofanya mkoa wa Simiyu.Hatua ya ujenzi wa madarasa kufikia 85%, hiyo ni hatua kubwa sana. Lengo la Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha kwamba watoto wetu wanaoingia kidato cha kwanza 2022, wote wanaingia darasani kwa pamoja,na hivyo kutokuwa na uchaguzi wa mara ya pili kwa ajili ya kuingia kidato cha kwanza yaani (second Selection).
Serikali ya Awamu ya sita imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 15000 kati ya hayo madarsa 12000 ni kwa ajili ya shule za sekondari na madarasa 3000 kwa ajili ya shule za msigi. Mkoa wa Simiyu umepatiwa shule 380.
Kuhusa sekta ya afya pongezi kwako Mkuu wa Mkoa, RHMT na RMO,kwani sekta hii ilikuwa na changamoto sana, mikataba ambayo inatoa viwango vya upimaji utendaji kazi (Key Performance Indicator - KPI) na vikao vya kila robo mwaka ni ubunifu wa hali ya juu kwani inaleta uwajibikaji.Kabla ya kuwa Naibu Waziri nilikuwa Mwanasimiyu/mganga Mkuu wa Mkoa na hivyo namba yangu ya simu ilitumika kupokea malamiko mbalimbali ya wanasimiyu. Kipindi cha nyuma kulikuwa na malalamiko mengi sana ila ndani ya miezi 6 sijapata malalamiko yeyote.
"Asilimia 95 ya huduma za afya hutolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zipo chini ya TAMISEMI.
Niwapongeze sana Mkoa wa Simiyu kwani kwa kipindi cha miezi sita mlianza matumizi ya mfumo wa GoThomis, na 65% ya vituo vyenu vya afya vinatumia mfumo huo kwa ajili ya kukusanya mapato. Kama aliyoeleza mkuu wa Mkoa mfumo huo umewasaidia kuongeza mapato kutoka kiasi cha Tsh.200mln–600mln. Makusanyo haya yanasaidia sana kuacha utegemezi toka Serikali kuu au wafadhili. Hivyo ni vyema Halmashauri zote ziige mkoa wa Simiyu" amesema Mhe. Dugange .
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amemshukuru Mhe.Dugange kwa kutembelea mkoa wa Simiyu,na kumhakikishia kuwa ujenzi wa madarasa ambao umefikia 85% utamalizika kwa wakati. Kwa upande wa sekta ya afya Mhe. Kafulia amemfahamisha Naibu Waziri Tamisemi /afya kuwa mafanikio katika sekta ya afya yametokana na utendaji kazi mzuri wa Mganga mkuu wa mkoa pamoja na timu yake,kwani kwa kipindi cha miezi sita mapato yameongezeka kwa asilimia 300."Nimesaini mkataba wa utendaji kazi kati yangu na Wakuu wa wilaya.Niwapongeze wakuu wa Wilaya kuwa sasa tunasomana" amesema Kafulila.
Akiwasilisha taarifa ya hali ya utekelezaji mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 mkoa wa Simiyu, Kaimu Katibu Tawala,Injinia Mashaka Luhamba alieleza kuwa Mkoa wa Simiyu umetengewa jumla ya Tshs 20,476,951,633.30 kwa ajili ya kutekeleza miradi inayolenga kuimarisha miundombinu ya Sekta za Elimu na Afya na mapambano dhidi ya UVIKO 19. Fedha hizo zimetolewa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Shule za Sekondari,Shule Shikizi,Hospitali za Wilaya katika ngazi za Halmashauri za Wilaya, Miji ,Manispaa na Majiji. Aidha, fedha zingine zimepelekwa kutekeleza miradi ya kipaumbele katika Hospitali ya Rufaa za Mkoa na Mamlaka za maji.
Kuhusu miradi ya ujenzi wa madarasa mkoani Simiyu,Injinia Luhamba amesema, hadi sasa miradi iliyoanza kutekelezwa ni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 380 vya shule za Sekondari na vyumba vya madarasa 69 vya Shule Shikizi.Mpaka sasa ujenzi huo umefikia 85% ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa. Injinia Mashaka Luhamba ameeleza kuwa, pamoja na mafanikio haya katika ujenzi wa madarasa Mkoa umekuwa ukikabiliwa na changamoto mbalimbali hususani katika halmashauri ya wilaya ya Maswa na Itilima ambapo changamoto kubwa imekuwa upatikanaji wa vifaa.Vifaa vya viwandani kama vile bati na saruji kuchelewa kufika katika maeneo husika hasa kwa Halmashauri ambazo zilitumia mfumo wa manunuzi ya pamoja. Bei ya vifaa kupanda ghafla mara tu miradi ilipoanza na hivyo kusababisha gharama ya mradi kuongezeka.Shule ambazo ziliomba kibali cha kuhamisha fedha kwenda katika maeneo mengine kwa ajili ya ujenzi zilichelewa kupata kibali na hivyo kusababisha kuchelewa kuanza kwa mradi.
Kuhusu sekta ya afya,mganga Mkuu Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniface Marwa, ameeleza kuwa kwa kipindi cha miezi tisa kumekuwa na mafanikio makubwa sana katika sekta ya afya Mkoani Simiyu.Awali kulikuwa na vituo vya afya 218 lakini sasa kuna vituo vya afya 221.Aidha upatikanaji wa dawa nao umeongezeka kufikia asilimia 91.
Dkt. Marwa amesema mafanikio yote haya yamepatikana kutokana ushirikiano uliopo baina ya wafanyakazi wa Sekta ya Afya, uongozi bora toka kwa mkuu wa mkoa na menejimenti yake. DKt Marwa amemfahamisha Naibu Waziri kuwa moja ya siri kubwa ya mafanikio haya ni usainishaji wa mikataba ya utendaji kazi katika sekta ya afya kati ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya ambao nao walisainishana na maafisa tarafa,Katibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri zote ambao nao wamesainishana na waganga wakuu wa halmashauri.
"Lengo la kusaini mikataba hii ni kuhakikisha utendaji kazi katika sekta ya afya unafanyika kwa weledi zaidi. Aidha ripoti za utendaji kazi zimekuwa zikitolewa kila robo mwaka na kwa kweli kumekuwa na mafaniko makubwa sana.Lengo letu ni kutaka kuwe na usimamizi na utendaji wa pamoja katika mkoa"amesema.Dkt Marwa.
Akijibu hoja kuhusu changamoto ya uhaba wa watumishi sekya ya afya Mhe. Dugange amekiri kuwa mkoa wa Simiyu ni mmoja kati ya mikoa inayokabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa Watumishi wa sekta ya afya. Serikali imeliona hilo na inafanyia kazi kwa kuendesha zoezi la kujua daktari na N esi ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wanaopaswa kuhudumiwa na dakkati /nesi mmoja ( Doctor/Nurse Patient ratio).Lengo la Serkali ni kuhakikisha kuwa kila mkoa uwe na watumishi angalau si chini ya 60% ya mahitaji yao. Akizungumzia 40% ya mapato ya ndani baada ya kutoa mapato lindwa, Mhe. Dugange amesema kuwa lazima fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo.
Naibu Waziri TAMISEMI (Afya)
Naibu Waziri TAMISEMI( Afya) Mhe.Dkt. Festo Dugange akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.
Naibu Waziri TAMISEMI- AFYA Mhe. Festo Dugange akizungumza na kutoa wito wa Halmashauri zote kuiga Mkoa wa Simiyu |
Washiriki wa Kutoka hospitali ya mkoa wa Simiyu pamoja na Makatibu Tawala wasaidizi wakifuatilia kwa makini maelezo ya viongozi mbalimbali wakati wa kikao hichoo. |
Tuesday, December 14, 2021
RC Kafulila Aagiza Wazawa Malampaka Wapewe Kipaumbele
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na Wananchi wa Malampaka- Maswa |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila ameagiza wazawa wa Malampaka wapewe kipaumbele kwenye ajira ya Ujenzi wa reli ya kisasa(SGR), Mwanza/ Isaka.
Maagizo hayo yametolewa, mara baada ya mamia ya wananchi wa mji wa Malampaka wilaya ya Maswa, kumlilia mkuu wa mkoa awasaidie kupata ajira kwenye kituo cha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Mwanza kwenda Isaka kilichopo kwenye mji huo, inayojengwa na kampuni ya CCECC ya nchini China.
Wananchi hao walitoa kilio chao katika mkutano wa hadhara uliondaliwa na Mkuu wa mkoa kwa ajili ya kusikiliza malalamiko yao kuhusu kubaguliwa kwao katika masuala ya ajira pamoja na kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwenye mradi huo unaofanyika mjini Malampaka.
Wananchi hao walimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa wakati mradi huo unatambulishwa kwa mara ya kwanza kwao na viongozi wa serikali walielezwa kuwa wakazi wa eneo hilo ambapo panajengwa bandari ya nchi kavu watapatiwa kipaumbele kwenye masuala ya ajira.
Walisema kuwa kwa sasa shughuli zimekwisha anza lakini waliopatiwa ajira ni watu wachache tu ambao hawazidi 15 kulinganishwa na idadi watu 300 walioko kwenye kambi hiyo. Ambapo wengi wao wametoka nje ya mkoa wa Simiyu.
'Mwanzoni tulielezwa kuwa mradi utakapoanza kipaumbele kitatolewa kwa wananchi ambao wanaishi katika eneo ambalo mradi unatekelezwa lakini cha kushangaza mambo yamekwenda kinyume kabisa wengi wa waajiriwa wanatoka nje kabisa ya mkoa wa Simiyu,"
"Sisi tumekuwa tukibaguliwa katika masuala ya ajira na jambo baya zaidi katika kupata ajira hizo vitendo vya rushwa vimeshamiri sana,"alisema Juma.
Kutokana na malalamiko hayo Mkuu wa Mkoa ameagiza vyombo vya dola kufutailia suala la rushwa kama lipo na kutaka wahusika watakaobainika kuchukuliwa hatua za kusheria.
Aidha ametaka kupelekewa majina ya watu walioajiriwa kama wanatoka mkoa wa Simiyu au la kwani Serikali imekuwa ikitaka wanufaika wa kwanza wawe wanaoishi kwenye eneo la mradi.
MWISHO.
Thursday, December 9, 2021
Kuna Watu Wengi wa Maana Kaburini Kuliko Tuliobaki
Pongezi Kwa Kuadhimisha Miaka 60 ya Uhuru 1961-2021
Salamu za Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika
Thursday, December 2, 2021
Simiyu Yafanya Vizuri Viashiria vya UKIMWI, Kitaifa na Kimataifa-RC KAFULILA
Mhe. Kafulila ameyasema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kimkooa katika Viwanja Vya Halmashauri Bariadi, Mkoani Simiyu.
Aidha Mhe. Kafulila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutilia mkazo agenda ya afya, kwani afya imekuwa kipaumbele kikubwa sana katika Serikali ya Awamu ya Sita.Toka miaka ya 1980 wakati janga la UKIMWI lilipoikumba Dunia,Dunia imefanikisha kwa kiasi kikubwa kupambana na janga la hili, ili hali Changamoto kubwa ikiwa imebakia katika nchi zilizopo kusini mwa Jangwani la Sahara .
Dunia Inaendelea kupambana na jangwa la UKIMWI kwa Sababu athari zake ni kubwa,nazo huathiiri mtu mmoja mmoja, familia na hadi Taifa. Mkoani Simiyu idadi ya maambukizi ya UKIMWI ni asilimia 3.9% ambayo ni chini ya kiwango cha Kimataifa ambacho ni asilimia 5.1%,hii inaonyesha kwamba kazi imefanyika.Pamoja na mafanikio haya hii haimaniishi kwamba tulane badala yake tuzidishe mapambano, na iwe agenda kwenye vikao vyetu kuanzia ngazi ya kata.
"Vikao vya kamati ya maendeleo ni vyema vikajadili suala hili. Mabaraza ya Madiwani RMO,kwenye vikao vyote vya RCC,DCC na vikao vya Madiwani mada kuhusu magonjwa ya UKIMWI na UVIKO namna na jinsi ya kujikinga ni lazima ziwe agenda za mawasiliano" Tukijenga uelewa mzuri kuhusu magonjwa haya tuna uwezo mkubwa wa kujikinga na hatimaye kuepukana magonjwa yote ".Alisisitiza Mhe.Kafulila.
Ujumbe wa Mwaka huu wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani unasema "ZINGATIA USAWA, TOKOMEZA UKIMWI, TOKOMEZA MAGONJWA YA MLIPUKO". Kauli mbiu hii ni pana na inabeba mambo mengi.Kama viongozi tunapaswa kuzungumzia magonjwa haya ya mlipuko.
I" Asilimia 43% ya maambukizi mapya Tanzania, yanatokea kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15-24, hii ndio nguvu kazi ya nchi .Hali hii inaonyesha kuwa tusipochukua hatua, tutabaki na Taifa dhaifu sana, kwani huwezi kujenga Taifa lenye nguvu kama lina vijana wenye afya dhaifu. Ukubwa wa Taifa ni rasilimali watu ambao hupimwa kwa mambo matatu,afya,uadilifu na maarifa. Nitoe wito "pale ambapo itakuwa umeathirika huo sio mwisho wa maisha yako.Kupata ukimwi haimaanishi ni mwisho wa maisha yako na mwisho wa kufanya kazi,hivyo tujitahidi kukabiliana na janga hili.Tuwahi kupima ili tujue afya zetu,kwani kwa kuwahi kutumia dawa sahihi na kwa usahihi kutafubaza wadudu wa UKIMWI" Amesema Kafulila.
Aidha Mhe. Kafulika alionya tabia ya wanaume kutegemea wake zao kupima VVU na kuamini kwamba majibu ya mke wake ni majibu ya wote."Hii ni dhana potofu na wanaume tunatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kujua afya zetu".
Nichukue fursa hii kuwakumbusha wananchi wote wa mkoa wa Simiyu wanaotumia dawa za kufubaza VVU, kuendelea kuzitumia kwa usahihi kama inavyoshauriwa na wataalam wetu ili tufikie 100%. Mashuhuda Wawili wa Kike na Kiume walitoa ushuhuda kuhusu jinsi ambavyo wameweza kuishi na VVU na UKIMWI kwa zaidi ya miaka 10, kiasi cha kupata watoto ambao hawajaathirika na hivyo kuwahamasisha wananchi kupima afya zao,kujikubali, kisha kunywa dawa sahihi zinazotolewa na vituo vya afya kama zinavyoshauriwa na wataalam.
Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, kimkoa yamefanyika Wilayani Bariadi, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Lupakisyo Kapange alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kukubali kuwa mgeni rasmi.Akizungumzia Ujenzi wa Madarasa ya Uviko-19 Mhe. Kapange amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa "tumefikia mwisho/finishing.
Mwisho
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani |
Mufti wa Mkoa wa Simiyu akisali wakati wa Maadhimisho ya UKIMWI Duniani |
Mhe. David Kafulila akisoma risala ya Waathirika wa UKIMWI,Katika Viwanja vya Halmashauri Bariadi |
Wanakwaya ya AICC Simiyu ikitumbuiza wakati wa Maadhimisho |
Mhe. Kafulila akiwa ameambatana na viongozi wengine wakikagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya Halmashauri Bariadi |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila pamoja na Katibu Tawala Mkoa wakifuatilia jambo. |
Wajumbe wa Kamati ya Usalama wakifuatilia jambo wakati wa maadhimisho ya UKIMWI Duniani |
.