Thursday, December 2, 2021

Simiyu Yafanya Vizuri Viashiria vya UKIMWI, Kitaifa na Kimataifa-RC KAFULILA

 Mhe. Kafulila ameyasema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani  yaliyofanyika kimkooa katika Viwanja Vya Halmashauri Bariadi, Mkoani Simiyu.

 Akizungumza Mhe Kafulila alieleza kuwa Siku ya Ukimwi Duniani ni siku muhimu sana kwani ni siku ambayo tathmini ya jinsi gani janga la ukimwi lilivyoleta na linavyoendelea kuleta athari kubwa kuanzia mtu mmoja, familia hadi Taifa kwa ujumla hufanyika. Aidha siku hii ni muhimu kwa Dunia na kwetu wana Simiyu kwani hutoa fursa ya kuhamasisha Watanzania na Wana Simiyu na kuwaeleimisha jinsi gani wanavyoweza kupambana na maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI..

Aidha Mhe. Kafulila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutilia mkazo  agenda ya afya, kwani  afya imekuwa kipaumbele kikubwa sana katika Serikali ya Awamu ya Sita.Toka miaka ya 1980 wakati janga la UKIMWI lilipoikumba Dunia,Dunia imefanikisha kwa kiasi kikubwa kupambana na janga la hili, ili hali Changamoto kubwa ikiwa  imebakia katika nchi zilizopo kusini mwa Jangwani la Sahara .

Dunia Inaendelea kupambana na jangwa la UKIMWI kwa Sababu  athari zake ni kubwa,nazo huathiiri mtu mmoja mmoja, familia na hadi Taifa. Mkoani Simiyu  idadi ya maambukizi ya UKIMWI ni asilimia  3.9%  ambayo ni chini ya kiwango cha Kimataifa ambacho ni asilimia 5.1%,hii inaonyesha kwamba kazi imefanyika.Pamoja na mafanikio haya hii haimaniishi kwamba tulane badala yake tuzidishe mapambano, na iwe agenda kwenye vikao vyetu kuanzia ngazi ya kata.

"Vikao vya kamati ya maendeleo ni vyema vikajadili suala hili. Mabaraza ya Madiwani RMO,kwenye vikao vyote vya RCC,DCC na vikao vya Madiwani mada kuhusu magonjwa ya UKIMWI na UVIKO namna na  jinsi ya kujikinga ni lazima ziwe agenda za mawasiliano" Tukijenga uelewa mzuri kuhusu magonjwa haya tuna uwezo mkubwa wa kujikinga na hatimaye kuepukana  magonjwa yote ".Alisisitiza Mhe.Kafulila.

Ujumbe wa Mwaka huu wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani  unasema "ZINGATIA USAWA, TOKOMEZA UKIMWI, TOKOMEZA MAGONJWA YA MLIPUKO". Kauli mbiu hii ni pana na inabeba mambo mengi.Kama viongozi tunapaswa kuzungumzia magonjwa haya ya mlipuko.

I" Asilimia 43% ya maambukizi mapya Tanzania, yanatokea kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15-24,  hii ndio nguvu kazi ya nchi .Hali hii inaonyesha kuwa tusipochukua hatua, tutabaki na Taifa dhaifu sana, kwani huwezi kujenga Taifa lenye nguvu kama  lina vijana wenye afya dhaifu. Ukubwa wa Taifa ni rasilimali watu ambao hupimwa kwa mambo matatu,afya,uadilifu na maarifa. Nitoe wito "pale ambapo itakuwa umeathirika huo sio mwisho wa maisha yako.Kupata ukimwi haimaanishi ni mwisho wa maisha yako na mwisho wa kufanya kazi,hivyo tujitahidi  kukabiliana na janga hili.Tuwahi kupima ili tujue afya zetu,kwani kwa kuwahi kutumia dawa sahihi na kwa usahihi kutafubaza  wadudu wa UKIMWI" Amesema Kafulila.

Aidha Mhe. Kafulika alionya tabia ya wanaume kutegemea wake zao kupima VVU na kuamini kwamba majibu ya mke wake ni majibu ya wote."Hii ni dhana potofu na wanaume tunatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kujua afya zetu".

 Mhe. Kafulila alitaja baadhi ya mambo  yanayochochea UKIMWI mkoani Simiyu,kuwa ni kuwa na wenza wengi, Kurithi wajane,kuanza ngono katika umri mdogo, kujihusisha na makundi hatarishi,kulewa kupindukia,kutumia Dawa za kulevya, idadi ndogo ya wanaume wenye tohara na biashara ya ngono. Mkuu wa Mkoa alieza kuwa amepata taarifa kuwa baadhi ya wadada wanajiuza maeneo mmbalimbali na hivyo akatoa maelekezo kwa  wakuu wote wa  Wilaya kuhakikisha maeneo yote yanayotumika kwa biashara ya ngono yanadhibitiwa, kwani hiyo sio biashara halali, na sio utamaduni wetu. Mkuu wa Mkoa aliziagiza Kamati za Amani na kamati za Usalama kukutana  mara kwa Mara na kuhakikisha zinashirikiana katika kudumisha maadili.

 Akitaja  malengo matatu ya kidunia ya kupambana na maambukizi ya VVU na UKIMWI na uhalisia katika mkoa wa Simiyu Mhe. Kafulila ameeleza kuwa katika   95% ya kwanza ifikapo mwaka 2030 wananchi wenye maambukizi wawe wanafahamu hali zao, Mkoani Simiyu wananchi asilimia 84 wanatambua hali zao za maambukizi ya VVU. Katika 95% ya pili  dunia ilikubaliana kuwa ifikapo mwaka 2030, asilimia 95 ya wale wanaobainika  kuwa na maambukizi ya VVU, asilima 95 waanzishwe dawa za ARV kwa ajili ya kufubaza VVU. Katika lengo hili Mkoa wa Simiyu tumefikia 99% hii ni hatua kubwa sana inayohitaji Pongezi. Asilimia 95 ya tatu, wale wote walioko kwenye dawa baada ya miezi 6 virusi viwe vimefubaa kwa 95% kwa mkoa wa Simiyu tumefikia 96%. 

Nichukue fursa hii kuwakumbusha wananchi wote wa mkoa wa Simiyu wanaotumia dawa za kufubaza VVU, kuendelea kuzitumia kwa usahihi kama inavyoshauriwa na wataalam wetu ili tufikie 100%. Mashuhuda Wawili wa Kike na Kiume walitoa ushuhuda kuhusu jinsi ambavyo wameweza kuishi na VVU na UKIMWI kwa zaidi ya miaka 10, kiasi cha kupata watoto ambao hawajaathirika na  hivyo kuwahamasisha wananchi kupima afya zao,kujikubali, kisha kunywa dawa sahihi zinazotolewa na vituo vya afya kama zinavyoshauriwa na wataalam.

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, kimkoa yamefanyika Wilayani  Bariadi, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Lupakisyo Kapange alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kukubali kuwa mgeni rasmi.Akizungumzia Ujenzi wa Madarasa ya Uviko-19 Mhe. Kapange amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa "tumefikia  mwisho/finishing.

Mwisho





Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani

Mufti wa Mkoa wa Simiyu akisali wakati wa Maadhimisho ya UKIMWI Duniani

Mhe. David Kafulila akisoma risala ya Waathirika wa UKIMWI,Katika Viwanja vya Halmashauri  Bariadi

Wanakwaya ya AICC Simiyu ikitumbuiza wakati wa Maadhimisho

Kutoka kulia RAS wa Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Lupakisyo Kapange pamoja na DAS- Bariadi Bw.Shirima wakielekea kwenye jukwaa kuu.




Mhe. Kafulila akiwa ameambatana na viongozi wengine wakikagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya Halmashauri Bariadi



Mkuu wa Mkoa  wa Simiyu Mhe. David Kafulila pamoja na  Katibu Tawala Mkoa wakifuatilia jambo.


Wajumbe wa Kamati ya Usalama wakifuatilia jambo wakati wa maadhimisho ya UKIMWI  Duniani

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo(kulia), Mhe. David Kafulila(RC) na Mhe. Lupakisyo Kapange(DC- Bariadi) wakiondoka viwanja vya Halmashauri Bariadi mara baada ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani

 

.

 

 

 

 

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!