Wito huo umetolewa leo na Mhe.Dkt.Festo Dungage NaibuWaziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serilkali za Mitaa (TAMISEMI-AFYA), mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19 Mkoa wa Simiyu.
Mhe.Dugange,amepongeza Sekretarieti ya Mkoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na viongozi wote wa Mkoa wa Simiyu,kwa kazi nzuri wanayofanya.
"Hongera kwa kazi nzuri sana mnayofanya mkoa wa Simiyu. Hatua ya ujenzi wa madarasa kufikia 85%, hiyo ni hatua kubwa sana. Lengo la Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha kwamba watoto wetu wanaoingia kidato cha kwanza 2022, wote wanaingia darasani kwa pamoja , hivyo hakutakuwa na uchaguzi wa kuingia kidato cha kwanza kwa mara ya pili yaani (second Selection).
Serikali ya Awamu ya sita imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 15000 kati ya hayo madarsa 12000 ni kwa ajili ya shule za sekondari na madarasa 3000 kwa ajili ya shule za msigi.Mkoa wa Simiyu umepatiwa shule 380.
Kuhusa sekta ya afya pongezi kwako Mkuu wa Mkoa, RHMT na RMO, kwani sekta hii ilikuwa na changamoto sana, mikataba ambayo inatoa viwango vya upimaji utendaji kazi (Key Performance Indicator - KPI) na vikao vya kila robo mwaka ni ubunifu wa hali ya juu kwani inaleta uwajibikaji Kabla ya kuwa Naibu Waziri nilikuwa Mwanasimiyu/mganga Mkuu na hivyo namba yangu simu yangu ilitumika kupokea malamiko mbalimbali ya wanasimiyu.Kipindi cha nyuma kulikuwa na malalamiko mengi sana ila ndani ya miezi 6 sijapata malalamiko yeyote.
"Asilimia 95 ya huduma za afya hutolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambzo zipo chini ya TAMISEMI. Niwapongeze sana Mkoa wa Simiyu kwani kwa kipindi cha miezi sita mlianza matumizi ya mfumo wa GoThomis, na 65% ya vituo vyenu vya afya vinatumia mfumo huo kwa ajili ya kukusanya mapato. Kama aliyoeleza mkuu wa Mkoa mfumo huo umewasaidia kuongeza mapato kutoka Tsh.200mln–600mln. Makusanyo haya yanasaidia sana kuacha utegemezi toka Serikali kuu au wafadhili. Hivyo ni vyema Halmashauri zote ziige mkoa wa Simiyu" amesema Mhe. Dugange .
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amemshukuru Mhe. Dugange kwa kutembelea mkoa wa Simiyu,na kumhakikishia kuwa ujenzi wa madarasa ambao umefikia 85% utamalizika kwa wakati. Kwa upande wa sekta ya afya Mhe. Kafulia amemfahamisha Naibu Waziri Tamisemi /afya kuwa mafanikio katika sekta ya afya yametokana na utendaji kazi mzuri wa Mganga mkuu wa mkoa pamoja na timu yake RMO,kwani kwa kipindi cha miezi sita mapato yameongezeka kwa asilimia 300. "Nimesaini mkataba wa utendaji kazi kati yangu na Wakuu wa wilaya .Niwapongeze wakuu wa Wilaya kuwa sasa tunasomana" amesema Kafulila.
Akiwasilisha taarifa ya hali ya utekelezaji mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 mkoa wa Simiyu,Kaimu Katibu Tawala M,Injinia Mashaka Luhamba alieleza kuwa Mkoa wa Simiyu umetengewa jumla ya Tshs 20,476,951,633.30 kwa ajili ya kutekeleza miradi inayolenga kuimarisha miundombinu ya Sekta za Elimu na Afya na mapambano dhidi ya UVIKO 19. Fedha hizo zimetolewa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Shule za Sekondari,Shule Shikizi,Hospitali za Wilaya katika ngazi za Halmashauri za Wilaya, Miji ,Manispaa na Majiji. Aidha, fedha zingine zimepelekwa kutekeleza miradi ya kipaumbele katika Hospitali ya Rufaa za Mkoa na Mamlaka za maji.
Kuhusu miradi ya ujenzi wa shule mkoani Simiyu,Injinia Luhamba amesema, hadi sasa miradi iliyoanza
kutekelezwa ni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 380 vya shule za
Sekondari na vyumba vya madarasa 69 vya Shule Shikizi. Mpaka sasa ujenzi
huo umefikia 85% ya utekelezaji wa
ujenzi wa vyumba vya madarasa.Injinia Luhamba ameeleza kuwa pamoja na mafanikio haya katika ujenzi wa
Madarasa Mkoa umekuwa ukikabiliwa na
changamoto mbalimbali hususani katika Wilaya ya Maswa na Itilima ambapo
changamoto kubwa imekuwa upatikanaji wa vifaa. Vifaa vya viwandani kama vile
bati na saruji kuchelewa kufika katika maeneo husika hasa kwa Halmashauri
ambazo zilitumia mfumo wa manunuzi ya pamoja. Bei ya vifaa kupanda ghafla mara
tu miradi ilipoanza na hivyo kusababisha gharama ya mradi kuongezeka.Shule
ambazo ziliomba kibali cha kuhamisha fedha kwenda katika maeneo mengine kwa
ajili ya ujenzi zilichelewa kupata kibali na hivyo kusababisha kuchelewa kuanza
kwa mradi.
Kuhusu sekta ya afya,mganga Mkuu Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniface Marwa, ameeleza kuwa kwa kipindi cha miezi tisa kumekuwa na mafanikio makubwa sana katika sekta ya afya Mkoani Simiyu.Awali kulikuwa na vituo vya afya 218 lakini sasa kuna vituo vya afya 221.Aidha upatikanaji wa dawa nao umeongezeka kufikia asilimia 91.
Dkt. Marwa amesema mafanikio yote haya yamepatikana kutokana ushirikiano uliopo baina ya wafanyakazi wa Sekta ya Afya, uongozi bora toka kwa mkuu wa mkoa na menejimenti yake. DKt Marwa amemfahamisha Naibu Waziri kuwa moja ya siri kubwa ya mafanikio haya ni usainishaji wa mikataba ya ya utendaji kazi katika sekta ya afya kati ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya ambao nao walisainishana na maafisa tarafa, Katibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri zote ambao nao wamesainishana na waganga wakuu wa halmashauri.
"Lengo la kusaini mikataba hii ni kuhakikisha utendaji kazi
katika sekta ya afya unafanyika kwa weledi zaidi. Aidha ripoti za utendaji kazi
zimekuwa zikitolewa kila robo mwaka na kwa kweli kumekuwa na mafaniko makubwa
sana.Lengo letu ni kutaka kuwe na usimamizi na utendaji wa pamoja katika mkoa"amesema.Dkt
Marwa.
Akijibu hoja kuhusu changamoto ya uhaba wa watumishi sekya ya afya Mhe. Dugange amekiri kuwa mkoa wa Simiyu ni mmoja kati ya mikoa inayokabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa Watumishi wa sekta ya afya.Serikali imeliona hilo na inafanyia kazi kwa kuendesha zoezi la kujua daktari na N esi ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wanaopaswa kuhudumiwa na dakkati /nesi mmoja ( Doctor/Nurse Patient ratio).Lengo la Serkali ni kuhakikisha kuwa kila mkoa uwe na watumishi angalau si chini ya 60% ya mahitaji yao .Akizungumzia 40% ya mapato ya ndani baada ya kutoa mapato lindwa, Mhe. Dugange amesema kuwa lazima fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo.
Mhe. Festo Dugange yupo ziara Mkoani Simiyu kwa lengo la kupitia miradi ya ujenzi wa madarasa ya Uviko na vituo vya afya,ili kuona shughuli zinazoendelea na Changamoto mbalimbali wanazokalibiana nazo katika utekelezaji wa shughuli hizo. Mwisho
NAIBU WAZIRI TAMISEMI (AFYA) MHE. DKT. FESTO DUGANGE AKISALIMIANA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MKOA WA SIMIYU MARA BAADA YA KUWASILI MKOANI HAPO |
KAIMU RAS , INJINIA MASHAKA LUHAMBA AKISOMA TAARIFA YA MKOA |
MGANGA MKUU OFISI YA MKUU WA MKOA SIMIYU DKT. BONIOFACE MARWA AKISOMA TAARIYA YA SEKYA YA AFYA |
0 comments:
Post a Comment