Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Mizengo K.Pinda , jumatatu tarehe 15/11/2021,alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kusaini Kitabu cha Wageni ambapo Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.Mhe David Z.Kafulila aliwasilisha kwake taarifa fupi katika Sekta mbalimbali za Miradi ya Maendeleo.
Mhe.Pinda alisisitiza miradi ya utekelezaji kwa fedha za covid 19 usimamiwe kikamilifu na Mkoa na kusiwepo na ubadhirifu wowote. Aidha alisisitiza viongozi wa CCM wasihusike kwa vyovyote vile katika utekelezaji wa miradi hiyo kuepusha mgongano wa maslahi.
Mhe.Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alisisitiza suala la Udumavu(Malnutrition), lisimamiwe kikamilifu ili takwimu za Mkoa kwenye udumavu lishuke au liishe kabisa.
Mwisho.*
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Mizengo K.Pinda atembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala, Mkuu wa Wilaya Bariadi |
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Mizengo K.Pinda akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Simiyu |
0 comments:
Post a Comment