Serikali
imeanza maandalizi ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka
yenye urefu wa kilomita 341 ambayo itajengwa kwa gharama ya shilingi trilioni
3.0267 fedha za ndani, ambapo katika mradi huu Bandari kavu na stesheni vinatarajiwa kujengwa katika eneo la Malampaka
wilayani Maswa mkoani Simiyu..
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja
Kadogosa Machi 08, 2021 katika kikao cha pamoja cha wadau ambacho kilifanyika
katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa kwa lengo la kujenga
uelewa wa pamoja juu ya utekelezaji wa mradi huu ili kufanya maandalizi muhimu.
“Hapa
Malampaka tutakuwa na kambi ya watu zaidi ya 3000 kwa hiyo ni vizuri wananchi
wakaandaliwa ili waweze kushiriki fursa mbalimbali, tunatarajia pia kujenga bandari
kavu kama ilivyo Isaka mizigo kutoka mikoa mbalimbali itaishia hapa; Malampaka
pia tutajenga stesheni jengo kubwa lenye mita za mraba 8000 ambayo ndani
itakuwa na benki, maduka na huduma nyingine,” alisema Kadogosa.
“Mradi
huu ni lazima uwe na maana kwa maisha ya watu wa kawaida, mahitaji mbalimbali
yatahitajika na watenda kazi kwenye mradi huu kama vile malazi, chakula mfano
kuku tu zitahitaji zaidi ya kuku 40,000 kwa mwezi, kwa hiyo hii ni fursa nzuri
itakayobadilisha maisha ya wengi, wananchi wajipange kutumia fursa hii,” alisisitiza.
Aidha, Kadogosa ametoa wito kwa
wananchi na wadau wengine kutoka taasisi mbalimbali kushirikiana na TRC ili
utekelezaji wa mradi huu usiathiri shughuli mbalimbali za wananchi na taasisi
hizo zinazotoa huduma kwa jamii, huku akiahidi kuwa TRC itaendelea kusimamia upatikanaji
wa fursa zipatikane kwa usawa kama ilivyoelekezwa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu umepokea mradi huo kwa asilimia 100 na
kuahidi kutoa ushirikiano, huku akiwahakikishia usalama wakandarasi na watu
wote watakaohusika na utekelezaji wa mradi huu.
Kiswaga ameagiza idara ya ardhi
Maswa kupima maeneo ili wananchi waweze kupata maeneo ya kujenga na kuwekeza
kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali, ambapo pia ametoa wito kwa wananchi
kununua maeneo hayo yatakapotangazwa, ili waweze kujenga nyumba za kuishi na
kuwekeza katika fursa mbalimbali kuinua uchumi wao, mkoa na Taifa kwa ujumla.
Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu, Bi.
Haula Kachwamba ametoa wito kwa Wananchi wa Malampaka kila mmoja kuwa mlinzi wa
mali za mkandarasi na serikali, “ Hatutegemei mali ya serikali na mkandarasi ikaibiwa,
tunategemea itafanya kazi iliyokusudiwa hivyo kila mmoja akawe mlinzi, lakini
pia mjiandae kutumia fursa hii, wakulima, wafugaji, mama ntilie kila mmoja kwa
namna yake.”
Mwenyekiti Kijiji cha Ikungu Bw.
Chuma Gashi amesema wananchi wa Kijiji hicho wameupokea mradi huo kwa mikono
miwili na wako tayari kupisha maeneo yatakayohitajika kwa kufuata taratibu huku
akibainisha kuwa yeye binafsi kama mwananchi amejipanga kufanya biashara ya
kuku katika kambi itakayojengwa Malampaka na baadaye reli ikikamilika
atasafirisha kwenda Dar es salaam.
Naye Julia Musa amesema “mradi wa
reli tumeupokea kwa furaha maana tunajua mji wetu wa Malampaka utapata
maendeleo, vijana watapata ajira, tunamuombea Mhe. Rais azidi kutuletea miradi
mingine ili sisi wana Malampaka tuzidi kupata maendeleo, tuko tayari kupisha
mradi na kwenda kwenye maeneo tutakayopangiwa na serikali tukilipwa fidia ili
kupisha ujenzi wa reli hii.”
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Aswege Kaminyoge amesema eneo la
Malampaka linakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 14,300.
Kikao cha uongozi wa TRC kilihusisha pia viongozi wa chama na Serikali ngazi ya mkoa nawwilaya ya Maswa, viongozi wa dini, wazee maarufu, baadhi ya wananchi na wakandarasi pamoja na watekeelzaji wengine wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).
MWISHO
Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa (wa tatu kushoto) akiwaonesha
jambo baadhi ya viongozi na wadau wa reli ya kisasa (SGR) baada ya kutembelea
eneo ambalo litajengwa stesheni ya Malampaka wilayani Maswa wakati wa utekelezaji
wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, mara baada ya kikao chake na
wadau hao kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii
Malampaka Maswa . Mtaalam kutoka Shirika
la Reli Tanzania (TRC) akitoa maelezo ya eneo linalotarajiwa kujengwa stesheni ya
Malampaka wilayani Maswa wakati wa utekelezaji wa reli ya kisasa (SGR) kipande
cha Mwanza-Isaka, mara baada ya kikao cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau
wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya
Jamii Malampaka wilayani Maswa.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya
kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, kikao ambacho kilihusisha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa
mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii
Malampaka wilayani Maswa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na
wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka
akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, kikao ambacho
kilihusisha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu
kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka
wilayani Maswa.Katibu wa CCM Mkoa wa
Simiyu, Bi. Haula Kachwamba akitoa salamu za Chama katika kikao cha wadau wa
mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, ambacho
kilihusisha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu
kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka
wilayani Maswa. Baadhi ya wadau wa mradi
wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, wakifuatilia kikao
cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi
08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa. Baadhi ya wadau wa mradi
wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, wakifuatilia kikao
cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi
08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.
Baadhi ya wadau wa mradi
wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, wakifuatilia kikao
cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi
08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa. Mkuu wa Wilaya ya Maswa,
Mhe. Aswege Kaminyoge akizungumza katika kikao wadau wa mradi wa ujenzi wa reli
ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, kilichohusisha uongozi wa TRC na
viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo
cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa. Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Maswa, Eng. Paul Jidayi akitoa salamu za Chama wilaya katika kikao
cha wadau wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, ambacho
kilihusisha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu
kilichofanyika Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka
wilayani Maswa. Baadhi ya wadau wa mradi
wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, wakifuatilia kikao
cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi
08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa. Baadhi ya wadau wa mradi
wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Mwanza-Isaka, wakifuatilia kikao
cha uongozi wa TRC na viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu kilichofanyika Machi
08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.
Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa ( kushoto) akiwaonesha
jambo baadhi ya viongozi na wadau wa mkoa wa Simiyu baada ya kutembelea eneo ambalo litajengwa
stesheni ya Malampaka wilayani Maswa wakati wa utekelezaji wa reli ya kisasa (SGR)
kipande cha Mwanza-Isaka, mara baada ya kikao chake na wadau hao kilichofanyika
Machi 08, 2021 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka Maswa .