Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amewataka wataalam kufanya ukaguzi wa
matumizi ya chumvi isiyo na madini joto katika maeneo tofauti mkoani Simiyu ili
kuweza kupata uhalisia wa hali ya matumizi ya chumvi hiyo na matokeo yake yaweze kuwasaidia wataalam kutoa
elimu juu ya madhara ya matumizi ya chumvi kwa afya ya watumiaji.
Mmbaga
ametoa agizo hilo jana Machi 03, 2021 wakati akizungumza na baadhi ya viongozi
na wataalam katika kikao cha Kamati ya lishe ya mkoa kilichofanyika Mjini
Bariadi kwa lengo la kujadili utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe.
“Wataalam
wetu wa afya tengenezeni vigezo vya kisayansi vya ukaguzi wa chumvi isiyo na
madini joto utakaotupa picha halisi ya mkoa wetu ili taarifa yetu ya ukaguzi
ikitoka sisi wenyewe au mtu yeyote tukimweleza aweze kuelewa; siyo tufanye
ukaguzi ili ionekane tumefanya kwa kuwa sisi kama viongozi na watalaam tuna
hatari kwenye jamii yetu kwamba kuna watu watapoteza maisha na pia tutakuwa na
watu ambao hawana uelewa kwa sababu tu ya kutumia chumvi isiyokuwa na madini
joto,” alisema
Aidha,
Mmbaga ametoa wito kwa wataalam kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa
chumvi isiyo na madini joto na kuwashauri badala ya kuimwaga au kuharibu chumvi
inayokamatwa baada ya kubainika kuwa inauzwa au kupelekwa kwa watumiaji pasipo
kukidhi vigezo vya kiafya.
Afisa
Lishe wa mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige amesema madhara ya chumvi isiyo na
madini joto ni pamoja na wajawazito kujifungua watoto ambao hawajatimiza miezi
tisa, watoto kuwa na uwezo mdogo wa kiakili(kufikiri) kwa kuwa chumvi yenye
madini joto husaidia katika ukuaji wa ubongo wa watoto wakiwa tumboni,
kuharibika kwa mimba na kusababisha goita.
Katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha
kamati ya lishe ya mkoa kilichofanyika Machi 03, 2021 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kamati ya lishe ya mkoa
wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika Machi 03, 2021 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Itilima, Bw. Filbert Kanyilizu
akichangia hoja katika kikao cha kamati ya lishe ya mkoa kilichofanyika Machi
03, 2021 Mjini Bariadi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Boniface Richard
akifafanua jambo katika kikao cha kamati ya lishe ya mkoa kilichofanyika Machi
03, 2021 Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mpango wa Kudhibiti Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu
(COVID 19), Dkt. Khamis Kulemba akiwasilisha mada katika kikao cha kamati ya
lishe ya mkoa kilichofanyika Machi 03, 2021 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment