Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai
kwa Viongozi wa Serikali mkoani hapa kutumia busara na akili badala ya kutumia
nguvu katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika
maeneo waliyopo na kuhakikisha ufumbuzi unaotolewa unaleta tija kwa wananchi.
Mtaka
ametoa rai hiyo wakati akifungua kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa
(RCC) , kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu
ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.
“Wito
wangu kwa viongozi wenzangu tupunguze kutumia nguvu, tuongeze matumizi ya akili
tuone matokeo kwa wananchi wetu, leo tunapitisha mapendekezo ya bajeti ya mkoa
mwaka 2021/2022 lakini ningetamani kuona miradi mipya ya Halmashauri inayogusa
watu, halmashauri zetu zijielekeze kwenye kuanzisha miradi ambayo itakuwa
vyanzo vipya vya mapato,” alisema.
Aidha,
Mtaka ametoa rai kwa Viongozi wa Mkoa na Halmashauri kupima tija ya vikao vyao
na kuhakikisha vikao wanavyokaa vinaleta tija ikiwa ni pamoja na namna vikao hivyo
vinavyosaidia kubuni na kuongeza vyanzo vya mapato.
Akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti ya Mkoa wa Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi-Sehemu ya Mipango na Uratibu, Bw. Donatus Weginah amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Simiyu inatarajiwa kutengewa shilingi bilioni 200.5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, mishahara na matumizi mengineyo.
Akizungumza
kwa niaba ya wabunge Mwenyekiti wa
Wabunge wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa ameunga mkono
mapendekezo ya mpango na bajeti ya mkoa na kuahidi ushirikiaono wa wabunge hao
katika kupitisha bajeti hiyo bungeni.
Kwa
upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ametoa wito kwa
kwa viongozi wote mkoani Simiyu kushirikiana na vyombo vinavyohusika na
usimamizi wa fedha kudhibiti na kusimamia matumizi ya fedha zote za Serikali
ili ziweze kuleta tija.
Akitoa salamu kwa naiba ya Chama cha Mapinduzi,
Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba amewashauri wataalam kila
mmoja kutimiza wajibu wake katika kubuni vyanzo na mbinu za kuongeza mapato kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa mkoa wa Simiyu .
MWISHO
Baadhi ya wajumbe na waalikwa wa kikao cha Kamati ya
Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la
kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka
2021/2022.
Baadhi ya wajumbe na waalikwa wa kikao cha Kamati ya
Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la
kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka
2021/2022.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha Kamati ya
Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la
kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka
2021/2022.
0 comments:
Post a Comment