Uongozi wa mkoa wa Simiyu umetoa siku saba kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi na Ofisi ya Madini Mkoa wa Simiyu kupitia malalamiko na hoja zote za wachimbaji wadogo, wamiliki wa mashamba na wadau wengine katika mgodi wa dhahabu wa Bulambaka wilayani Bariadi na kuhakikisha shughuli za uchimbaji wa madini unafanyika kwa mujibu wa sheria.
Hayo
yameelezwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga mara baada ya
kiongozi huyo na viongozi wengine wa mkoa kuzungumza na wananchi hao waliofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Aprili
08, 2021 Mjini Bariadi ili kupata ufumbuzi wa malalamiko yao.
“
Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu imepokea wachimbaji na wadau mbalimbali wanaofanya
kazi katika mgodi wa Bulumbaka na kuwasikiliza baada ya kutoka kwa Mkuu wa
Wilaya; hoja za wachimbaji ni pamoja na wao kutokubaliana na utaratibu wa
utoaji leseni kwa kikundi kilichopewa leseni kufanya kazi katika eneo lile, ambapo
baadhi ya wanakikundi wamedai kuwa hawakitambua kwa kuwa hawakushirikishwa,”
“Baada
ya kuwasiliza pamoja na hoja nyingine tumeona hili suala bado liko ndani ya
uwezo wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya hivyo nimetoa siku saba kwa Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya na ofisi ya madini mkoa wa
Simiyu, wapitie hoja zote na kutoa ushauri na kufanyia kazi yale yote
wanayoweza kuyafanyia kazi kwenye ngazi yao kuhakikisha uchimbaji madini
ufanyike kwa mujibu wa sheria,” alisema Mmbaga.
Nao
baadhi ya wamiliki wa mashamba na wachimbaji wadogo ambao ni wananchi walioko
eneo la mgodi la Bulumbaka wamesema:
“Baadhi ya wenye mashamba hawajui leseni hii ilivyopatikana maana maana hawakushirikishwa, sisi wananchi ambao pia ni wachimbaji wadogo tunaomba haki itendeke, hatutaki mtu yeyote anyanyaswe,”
alisema Bw.Masuke Sahani mkazi wa Bulumbaka
“
Sisi tuna kilio kikubwa na mgodi wetu tumeshangaa kwamba Mwananyanzala amepata
leseni wakati sisi tuna muda mrefu tunatafuta hiyo leseni kwa watu wa madini
hatujapata, tunaomba Mkuu wa Wilaya atusaidie sisi wakazi wa Bulumbaka tupate
haki yetu,” alisema Monica Daniel mmoja wa wamiliki wa mashamba Bulumbaka.
Awali
akizungumzia na wananchi hao walipofika ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema malalamiko ya wananchi hao ameyapokea,
ambapo amebainisha kuwa maagizo aliyayatoa awali hayakufuatwa hivyo akawaomba wauone
uongozi wa mkoa ambao nao baadaye ukaelekeza ofisi yake iyashaghulikie kwa kuwa yako ndani
ya uwezo wake.
Mmiliki wa leseni katika eneo la Bulumbaka Seni
Mwananyanzala amesema kuwa leseni yake ilitolewa kihalali ambapo alifafanua kuwa
leseni hiyo ilisainiwa tarehe 19 Machi 2021.
MWISHO
Baadhi ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba katika eneo la mgodi wa Dhahabu wa Bulumbaka wilayani Bariadi wakisubiri kumuona Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (hayupo pichani) waliofika kumuona Aprili 08, 2021 ofisini kwake Mjini Bariadi ili kupata ufumbuzi wa malalamiko yao.
0 comments:
Post a Comment