Wastaafu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wamewaasa watumishi wa umma kumtanguliza Mungu, kuwa waadilifu na kujituma ili waweze kutimiza wajibu wao sawa sawa kwa maslahi yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na Bw. Elias Kasuka ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 35 na Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37 katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.
“Katika Utumishi wa Umma hampashwi kukata tamaa, binafsi nimeanzia mbali nikajiendeleza sikujali umri wangu, kikubwa ni kumtanguliza Mwenyezi Mungu katika kazi zenu mtafanikiwa tu,” alisema Bw. Godfrey Machumu.
“Siri kubwa ya kufikia mpaka kustaafu kwangu ni kufanya kazi kwa bidii na uadilifu, nilifanya kazi bila kusukumwa mfano mzuri ni kwa namna nilivyoshiriki kuandaa Maonesho ya nanenane mwaka 2018 na 2019 ; pia nawashauri mheshimu wakubwa kwa wadogo,” alisema Bw. Elias Kasuka.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi.Miriam Mmbaga amewapongeza wastaafu hao kwa utumishi uliotukuka mpaka kufikia kustaafu huku akitoa wito kwa watumishi wengine kuiga mema waliyojifunza kupitia utumishi wa wastaafu hao ikiwa ni pamoja na kuona umuhimu wa kujiendeleza kielimu wakiwa kazini na kujiendeleza kimaisha.
Katika hatua nyingine Bi. Mmbaga amewaasa watumishi
kuishi na watu wote vizuri huku akisisitiza umuhimu wa kuacha alama katika kazi
zao wanazofanya ili hata watakapo staafu
wakumbukwe kwa alama walizoacha kwenye maeneo waliyofanyia kazi.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya
pamoja na Bw. Elias Kasuka (wa pili
kushoto walioketi) ambaye kwa sasa
amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 35, Bw. Godfrey
Machumu (wa pili kulia) ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama
Mhasibu Mkuu baada ya kutumika kwa miaka
37 na mkewe pamoja na watumishi wengine wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
baada ya Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika
Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.
Kutoka kushoto Katibu
Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, Dkt. Gamitwe Mahaza, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya utawala na
Rasilimaliwatu Bw. Ekwabi Mujungu, Bw.
Elias Kasuka ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa
Kilimo Mkuu baada ya kutumika kwa miaka
35, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na Bw. Godfrey Machumu
ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37 na
Mhasibu Mkuu wa Mkoa, Bw. Francis Makombe katika picha ya pamoja baada ya Hafla fupi ya
kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini
Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi
Sehemu ya utawala na Rasilimaliwatu Bw. Ekwabi Mujungu(kulia) akiteta jambo na
Bw. Godfrey Machumu ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama
Mhasibu Mkuu baada ya kutumika kwa miaka
37 baada ya Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28,
2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,000,000/=
kwa Utumishi uliotukuka Bw. Elias Kasuka
ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Mhasibu Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 37, katika
Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28,
2020 Mjini Bariadi.
Bw. Elias Kasuka ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa
Kilimo Mkuu baada ya kutumika kwa miaka
35, akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya
kupokea zawadi ya cheti cha utumishi
uliotukuka na fedha taslimu shilingi 1,000,000/=kutoka kwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu(wa pili kushoto) katika Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu kwa
mwaka 2019/2020 iliyofanyika Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya
pamoja na Bw. Elias Kasuka (wa pili
kushoto walioketi) ambaye kwa sasa
amestaafu utumishi wa umma akiwa kama Afisa Kilimo Mkuu baada ya kutumika kwa miaka 35, Bw. Godfrey
Machumu (wa pili kulia) ambaye kwa sasa amestaafu utumishi wa umma akiwa kama
Mhasibu Mkuu baada ya kutumika kwa miaka
37 na mkewe pamoja na watumishi wengine wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
baada ya Hafla fupi ya kuwapongeza wastaafu hao wa mwaka 2019/2020 iliyofanyika
Agosti 28, 2020 Mjini Bariadi.