Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amezitaka
taasisi za fedha hapa nchini kuongeza fursa za mikopo kwa wakulima, wafugaji na
wavuvi ili kuongeza tijakatika uzalishaji.
“Benki za CRDB, NMB na NBC zimejiongeza sana
katika kutoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, katika mikopo iliyotolewa
katika kipindi hiki ni asilimia 09 tu ya
mikopo ndiyo iliyokwenda kwenye sekta ya kilimo, ninaomba mikopo katika sekta
hii iongezwe ili tuweze kuongeza tija katika kilimo, mifugo na uvuvi,” alisema
Mhe. Makamu wa Rais.
Aidha, Makamu wa Rais
ametoa rai kwa Watafiti wote nchini kutoa matokeo ya tafiti zao ili yaweze
kuwasaidia maafisa ugani na wadau wengine ili wakulima waweze kunufaika na
mtokeo hayo.
Katika hatua nyingine
Mhe. Makamu wa Rais ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa kujenga jengo la kudumu katika
Viwanja vya Nyakabindi Bariadi na kwa kuwa limejengwa kwa gharama kubwa
ameelekeza litumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Akizungumzia Kauli Mbiu
ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 inayosema “ KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO
NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020,” Mhe. Makamu wa Rais ametoa wito kwa
wananchi wote kuwa wakati utakapofika wachague viongozi wenye sifa, wazalendo
na wenye kuweka maslahi ya Taifa mbele kuliko maslahi binafsi.
Kwa upande wake Waziri
wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga amesema serikali imeimarisha mfumo wa
upatikanaji wa pembejeo za kilimo ambapo kwa sasa serikali imehakikisha
pembejeo zinapatikana kwa wakati jambo lililopelekea nchi kuwa na utoshelevu wa
chakula kwa zaidi ya asilimia 120.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ipo hoja na haja kwa Wizara ya kilimo kufanya viwanja vya
Nyakabindi kuwa endelevu na kufikiria katika kanda walizonazo, (eneo gani) kanda
ipi kati ya hizo itakuwa kituo mahiri cha shughuli za wakulima, wafugaji na
wavuvi kufanya maonesho yatakayolenga kuwa maonesho ya Kimataifa badala ya
kufanya mzunguko katika kanda hizo.
0 comments:
Post a Comment