Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina ametoa wito kwa wizara ya kilimo kuona haja ya kuwa na maabara za kupima udongo kwa kila wilaya ili wananchi waweze kujua hali ya udongo, pamoja na aina ya mbolea zinazopaswa kutumika katika udongo huo kwa lengo la kuongeza uzalishaji.
Waziri Mpina ameyasema
hayo Agosti 06, 2020 wakati akitembelea
mabanda katika Maonesho ya Nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Simiyu
katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Aidha, Waziri Mpina amesema Wizara ya kilimo iwasaidie
wakulima kupata mbegu bora kwa urahisi na bei nafuu ili waweze kupanda mbegu
bora kwa lengo la kupata mavuno mengi na bora.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazao kutoka Wizara ya Kilimo,
Bw. Nyasebwa Chimagu amesema mpaka sasa wizara hiyo ina vituo takribani 17
ambavyo wanaweza kupata taarifa za haki ya udongo ila wakulima wengi hawana
taarifa hivyo wizara inaendelea kujipanga kutoa taarifa kwa wananchi waweze
kujua uwepo wa vituo hivyo.
Katika hatua nyingine Mhe. Mpina alifungua bonanza la michezo
ambalo lilishirikisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambapo kila Mkoa
ulitoa timu moja ya mpira wa miguu na katika mechi zilizochezwa timu ya
Kurugenzi FC kutoka Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea, ikifuatiwa na Shinyanga na
Mara.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mpina, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema lengo la kuwa na mashindano ya mpira wa miguu ni kuimarisha uhusiano kati ya mikoa hiyo mitatu pamoja na kutangaza bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika Mkoa wa Simiyu.
Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 yamebebwa na Kaulimbiu inayosema "KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020".
MWISHO
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(kulia) akipata maelezo
kutoka kwa afisa wa Shirika la PASS wakati alipotembelea banda la shirika hilo Agosti
06, 2020 katika maonesho ya Nanenane ambayo Kitaifa mwaka 2020 yamefanyika
katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
TAZAMA PICHA MBALIMBALI MHE. MPINA AKIWA NA VIONGOZI WENGINE WAKATI ALIPOTEMBELEA MABANDA MBALIMBALI, AKIFUNGUA BONANZA LA MICHEZO AGOSTI 06, 2020 KATIKA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MWAKA 2020 YALOYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA NYAKABINDI BARIADI SIMIYU
Baadhi ya wananchi wakipata elimu ya namna ya kuandaa vyakula vya mifugo wakati walipotembelea banda la PASS wakati wa Maonesho ya nanenane Agosti 06, 2020 viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment