Naibu
Waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana na ajira Mhe. Anthony Mavunde
ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli
za uzalishaji mali kwa vijana na wanawake..
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo Agosti 02,
2020 ambayo imetengwa maalum kwa ajili ya kuhamasisha Program ya Kilimo awamu
ya pili (ASDP II) baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Nanenane Kitaifa
mwaka 2020, katika viwanja vya Nyakabindi
Bariadi mkoani Simiyu.
“Mhe. Waziri Mkuu wa awamu ya tatu alitoa
maelekezo ya kutenga maeneo hayo, awamu ya nne akaja Mzee Pinda Novemba 2014
likaja azimio la kila mkoa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za
uzalishaji mali kwa vijana na wanawake, mpaka sasa zimetengwa hekari 203,000 tu
ambazo bado hazitoshi kulingana na ukubwa wa nchi yetu,” alisema Mavunde
0 comments:
Post a Comment