Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima ametoa wito kwa taasisi za fedha zikiwemo benki kuwafuata wakulima na kuwapa mafunzo yatakayowasaidia ikiwemo mafunzo ya utunzaji, usimamizi wa fedha na namna ya kupata mikopo ya kuwasaidia katika kuongeza tija ya kilimo.
Mhe. Malima ameyasema hayo Agosti 07, 2020 wakati alipotembelea mabanda mbalimbali katika maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2020 ambayo yamefanyika katika uwanja wa Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
“ Elimu ambayo benki inatoa kwa wakulima na AMCOS ni nzuri sana kwani imesaidia sana nchi za Mashariki ya mbali ‘Far East’ wapate mafanikio makubwa sana; nafarijika sana na NMB Foundation kwa kuwafuata wakulima huko huko waliko vijijini,” alisema Malima.
Kwa upande wake Meneja wa NMB kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Sospeter Magesse amesema madarasa ya wakulima yalianza toka 2019 kukiwa na Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) 30, mwaka huu benki hiyo imefanikiwa kuendesha mafunzo kwa AMCOS 50.
Aidha, Magesse ameongeza kuwa benki ya NMB kupitia NMB Foundation imekuwa ikiwafikia wakulima mahali walipo vijijini na kuwafanyia mafunzo ambapo mwaka 2019/2012 jumla ya AMCOS 1520 zimepatiwa mafunzo na NMB foundation.
Akizungumza na watumishi wa wizara ya fedha na mipango mara baada ya kutembelea banda la wizara hiyo Mhe. Malima ameipongeza wzara hiyo kwa namna ilivyoboresha hali ya usimamizi wa mali za umma na nidhamu ya matumizi ya fedha za Umma huku akitoa wito kwa wizara kuona aina za kodi zinazoweza kumnufaisha mkulima na kuachana na kozi ambazo hazina manufaa kwa mkulima.
Akizungumza mbele ya
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima, mgunduzi wa viuadudu viitwavyo VURUGA Dkt.
Never kutoka Chuo cha Nelson Mandela amesema
amefanikiwa kutengeneza viuadudu hivyo ambayo vinasaidia sana kuzuia mazao kushaambuliwa na wadudu waharibifu hususani kwenye pamba.
Mhe. Malima pamoja na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Bi. Mary Makondo walipata fursa ya kutembelea mabanda ya wizara, taasisi, mashirika mbalimbali pamoja na mabanda ya wajasiriamali kujionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wajasiriamali hao na kujionea jinsi Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na taasisi mbalimbali zinavyofanya kazi ili kuhakikisha tunafikia Tanzania ya Viwanda Kupitia Kilimo.
Maonesho ya Nanenane
mwaka 2020 yanabebwa na Kauli Mbiu isemayo, “KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020.”
MWISHO.
TAZAMA PICHA MBALIMBALI MHE. MALIMA AKITEMBELEA MABANDA MBALIMBALI KATIKA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA 2020 KATIKA VIWANJA VYA NYAKABINDI BARIADI MKOANI SIMIYU.
0 comments:
Post a Comment