Mkuu wa wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, Mhe. Aswege Kaminyoge amezindua bodi ya Kampuni ya Ng'hami (Ng'hami Industries Company Ltd), ambayo iko chini ya Halmashauri ya wilaya ya Maswa itakayoendesha viwanda vinavyomilikiwa na halmashauri hiyo.
Akizindua bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo jana katika
ukumbi wa Halmashauri ya Maswa mkuu huyo wa wilaya amesema uzinduzi wa bodi
hiyo unaashiria utekelezaji wa dhamira njema ya kuwa na viwanda vya kimkakati
ndani na nje ya Mkoa wa Simiyu.
Kaminyoge amesema matokeo ya utekelezaji wa miradi ya
kimkakati kwa sekta ya viwanda Wilayani Maswa yameanza kuonekana dhahiri kwa
vitendo na kukuza uchumi wa wananchi wao kwa ujumla.
Bodi hiyo itasimamia viwanda vitano ambavyo ni kiwanda cha
kusindika Unga lishe wa viazi,Kiwanda cha Chaki,Kiwanda cha vifungashio
,kiwanda cha unga wa gypsum na cha kutenga madaraja ya mchele.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment