Akizungumza na wataalam hao Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu,
Bi. Miriam Mmbaga amesema ni vema maonesho hayo yakaakisi mahitaji ya wakulima,
wafugaji na wavuvi ili kuwasaidia kupata elimu na kuona teknolojia mbalimbali
zitakazowawezesha kufanya shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa tija.
Aidha , Bi. Mmbaga ameongeza kuwa ushiriki wa taasisi
mbalimbali za Umma na binafsi katika maonesho haya una manufaa kwa wakulima,
wafugaji na wavuvi kwa kuwa huwa zinatoa huduma ambazo zinayagusa makundi hayo
yote matatu.
"Ili kuboresha
Maonesho ya Nanenane suala la uendelevu wa viwanja ni la kulizingatia sana
hususani katika dhana ya kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kupata elimu ya
kilimo bora, wakati wote wanapohitaji kupitia viwanja hivyo," alisema Bi.
Mmbaga.
Pichani ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga
akizungumza na wataalam hao na akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara
hiyo.
0 comments:
Post a Comment