Mkoa wa Simiyu umeahidi kushiriki kikamilifu katika
maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajia kufanyika Oktoba mkoani Kagera.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga Agosti 28,
2020 wakati akizungumza na baadhi ya viongozi wa BAKWATA wa Mikoa ya Simiyu na
Kagera waliomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kuomba ushirikiano na mkoa wa
Simiyu kushiriki katika kufanikisha Maulidi hiyo.
“Tumelipokea
jambo hili kwa mikono miwili na tunaahidi kulifanyia kazi kwa wepesi kwa
kushirikiana na viongozi, ninaomba kupitia Katibu wa BAKWATA wa Mkoa wetu tutakaa pamoja tuone namna
tutakavyolitekeleza na baadaye tutalifanyia maamuzi ndani ya muda mfupi tu ili
maandalizi yaendelee,” alisema Bi. Mmbaga.
Kwa
upande wake Sheikh wa Mkoa wa Kagera, Haruna Kichwabuta amesema ili sherehe ya
Maulidi Kitaifa iweze kufanikiwa inahitaji ushirikiano wa Viongozi wa mikoa jirani
jambo ambalo limekuwa likifanyika wakati wote huku akisisitiza kuwa anashukuru
mkoa wa Simiyu kuonesha utayari wa kushiriki kufanikisha siku hiyo.
“Tumetoka
Kagera tukiwa na Baraka zote za Mhe. Mkuu wa Mkoa wetu na alituhakikishia kuwa
ameshawasiliana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu hivyo tunategemea kupata
ushirikiano kutoka Simiyu kwa kuwa sisi ni mikoa jirani, kama mlivyoshiriki
mwaka jana kupitia kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa
Mhe. Mtaka Mkoani Mwanza naamini hata mwaka huu tutakuwa pamoja ,” alisema
Sheikh Kichwabuta.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi wa
BAKWATA mkoa wa Simiyu na Kagera ambao wamemtembelea ofisini kwake kwa lengo la
kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa
inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera. Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ( wa pili kulia) akifurahia jambo na Sheikh wa
Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola mara baada ya mazungumzo kati yake na
viongozi wa BAKWATA wa Mikoa ya Simiyu
na Kagera yaliyolenga kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika
kufanikisha maandalizi ya Maulidi ya
Kitaifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera. Sheikh wa Mkoa wa
Simiyu, Mahamoud Kalokola akitoa taarifa ya utangulizi kwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (kushoto)
juu ya ujumbe wa viongozi wa BAKWATA
wa Mikoa ya Simiyu na Kagera uliofika ofisini kwake kuomba ushirikiano
na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha
maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba
2020 mkoani Kagera. Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya viongozi wa BAKWATA mkoa wa Simiyu na Kagera mara baada ya mazungumzo kati
yake na viongozi hao na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
yaliyolenga kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa
inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera. Sheikh wa mkoa wa
Kagera, Haruna Kichwabuta akisalimiana na Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.
Ernest Hinju mara baada ya mazungumzo kati ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Bi. Miriam Mmbaga na viongozi wa BAKWATA
wa Mikoa ya Simiyu na Kagera yaliyolenga kuomba ushirikiano na mkoa wa
Simiyu katika kufanikisha maandalizi ya
Maulidi ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera. Baadhi ya viongozi wa
BAKWATA wa Mikoa ya Simiyu na Kagera
wakiwa ofisini kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya mazungumzo
yaiyolenga kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa
inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera. Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi wa
BAKWATA mkoa wa Simiyu na Kagera ambao wamemtembelea ofisini kwake kwa lengo la
kuomba ushirikiano na mkoa wa Simiyu katika kufanikisha maandalizi ya Maulidi ya Kitaifa
inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 mkoani Kagera.
0 comments:
Post a Comment