Thursday, September 24, 2020

USIMAMIZI WA FEDHA UIMARISHWE ILI ZIFANYE KAZI ILIYOKUSUDIWA: RAS SIMIYU

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga ametoa rai kwa viongozi na watumishi katika wilaya ya Meatu kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani na matumizi ya fedha za miradi mbalimbali na kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za fedha zinazingatiwa ili fedha hizo zitumike kwa kazi zilizokusudiwa.

Mmbaga ametoa rai hiyo katika kikao alichofanya na viongozi na watumishi hao kilichofanyika Septemba 23, 2020 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mjini Mwanhuzi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa wilaya ya Meatu katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa wilaya ya Meatu wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani  akizungumza katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kulia) na baadhi ya viongozi na watumishi wa wilaya ya Meatu , kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.
Mkuu wa Shule ya Msingi Muungano, Mwl. Joseph Seni akichangia hoja katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadhi ya viongozi na watumishi wa wilaya ya Meatu , kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa wilaya ya Meatu wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza akifafanua jambo katika kikao cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kulia) na baadhi ya viongozi na watumishi wa wilaya ya Meatu , kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.

Baadhi ya viongozi na watumishi wa wilaya ya Meatu wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa wilaya ya Meatu wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa wilaya ya Meatu katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani  akizungumza katika kikao cha ndani kati ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kulia) na baadhi ya viongozi wilaya ya Meatu , kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.
Mkuu wa Idara ya utawala katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu akichangia hoja katika kikao cha ndani kati ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kulia) na baadhi ya viongozi wilaya ya Meatu , kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu akichangia hoja katika kikao cha ndani kati ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kulia) na baadhi ya viongozi wilaya ya Meatu , kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Meatu, Bw. Albert Rutaihwa akichangia hoja katika kikao cha ndani kati ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kulia) na baadhi ya viongozi wilaya ya Meatu , kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.
 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Meatu, Bw. Albert Rutaihwa akichangia hoja katika kikao cha ndani kati ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kulia) na baadhi ya viongozi wilaya ya Meatu , kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Meatu, Bw. Albert Rutaihwa akichangia hoja katika kikao cha ndani kati ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kulia) na baadhi ya viongozi wilaya ya Meatu , kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Septemba 23, 2020.

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 2.3 ZATOLEWA KWA WALENGWA WA TASAF 28984 SIMIYU

Serikali imetoa jumla ya shilingi 2,327,259,225 kwa walengwa  wa TASAF III awamu ya pili wapatao  28984 kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini katika kipindi cha mwezi Julai hadi Oktoba mwaka 2020 katika vijiji 376 mkoani Simiyu. 

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa TASAF mkoa wa Simiyu, Bw. Nyasilu Ndulu  Septemba 23, 2020 wakati wa zoezi la uhawilishaji fedha kwa walengwa wa TASAF wa kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu. 

“Fedha za walengwa tulizopokea ni shilingi 2,327,259,225 na hizi ni fedha za awamu mbili, mwezi Julai-Agosti na Septemba-Oktoba na zinalipwa kwa awamu moja;  fedha hizi zimefika kipindi muafaka cha maandalizi ya msimu wa kilimo nawashauri wazitumie vema katika maandalizi ya shughuli za kilimo lakini wajiwekee utaratibu wa kuwekeza kwenye shughuli za uzalishaji,” alisema Nyasilu. 

Akizungumza na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mwamishali  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ametoa rai kwa walengwa wao kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha hiyo ya ruzuku wanayopata ili waweze kufikia malengo yao. 

“Ninawasihi muendelee kujiamini na kila mmoja atambue kuwa anaweza, uwezeshaji ndiyo huu umeletwa na serikali hivyo ni kila mmoja akijiamini kuwa atafanikiwa kupitia kazi anayofanya atafanikiwa, kama mtu anafuga kuku, mbuzi, au ng’ombe akiwatunza vizuri akisaidiwa na wataalam wa halmashauri mtakuza vipato vyenu na mtafikia malengo yenu,” alisema Mmbaga. 

Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Kija Kayenze amesema ruzuku ya  fedha zilitolewa kwa walengwa wa TASAF zimefika katika kipindi muafaka, ambapo msimu wa kilimo unatarajiwa kufunguliwa Oktoba Mosi; huku akitoa wito kwa walengwa kutumia fedha hizo katika uandaaji wa mashamba, ununuzi wa mbegu bora ili waweze kupata mavuno bora. 

Nao baadhi ya walengwa wa TASAF wameishukuru Serikali kwa kutoa ruzuku ya fedha ambazo zimewasaidia kuanzisha miradi midogo midogo hususani katika kilimo, ufugaji na ujasirimali ambayo inawawezesha kupata mahitaji yao ya kila siku na kuweka akiba kwa ajili ya baadaye. 

“Naishukuru serikali kutusaidia kupitia TASAF, nilikuwa nafanya vibarua kupata hela ya matumizi na kuwanunulia wanangu mahitaji ya shule, lakini nilipoanza kupata hela za TASAF nikawa nazitunza baadaye nikanunua ng’ombe wawili ambao sasa hivi wamezaa, nategemea kuwauza wawili ili ninunue bati za kuezeka nyumba yangu na kupata mtaji,” alisema Sikitu Zengo mkazi wa Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu.

MWISHO

Bi. Sikitu Zengo(kulia) mlengwa wa TASAF III awamu ya pili kutoka Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu akipokea fedha za ruzuku inayotolewa kwa kaya maskini kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.
Bi. Sikitu Zengo mlengwa wa TASAF III awamu ya pili kutoka Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu akionesha ng’ombe aliwanunua kwa  fedha za ruzuku inayotolewa kwa kaya maskini kwa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wilaya  ya Meatu (hawapo pichani) wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga baada ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akizungumza na walengwa wa TASAF III Awamu ya Pili wa Kijiji cha Mwamishali wilayani humo kabla ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu, Bw. Nyasilu Ndulu akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wilaya  ya Meatu wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kushoto)  kabla ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.
Baadhi ya walengwa wa TASAF III Awamu ya Pili wa Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani humo.
Mmoja wa walengwa wa TASAF III awamu ya pili kutoka Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu akipokea fedha za ruzuku inayotolewa kwa kaya maskini kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na walengwa wa TASAF III Awamu ya Pili wa Kijiji cha Mwamishali wilayani humo kabla ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.

 

Baadhi ya walengwa wa TASAF III Awamu ya Pili wa Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani humo.

Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu, Bw. Nyasilu Ndulu (wa tatu kushoto)  akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wilaya  ya Meatu wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kushoto)  kabla ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.

Baadhi ya walengwa wa TASAF III Awamu ya Pili wa Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga(kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 katika kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu.
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu, Bw. Nyasilu Ndulu akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wilaya  ya Meatu wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (kushoto)  kabla ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.

 


Sunday, September 13, 2020

WADAU WA KILIMO SIMIYU WAJADILI MWONGOZO WA KILIMO CHA MKONGE

 Bodi ya Mkonge Tanzania imekutana na uongozi wa mkoa wa Simiyu na baadhi ya watendaji na wataalam wa kilimo kwa lengo la kujadili mwongozo wa kilimo cha mkonge mkoani hapa lengo likiwa ni kuhakikisha mkulima anazalisha mkonge bora na wenye thamani katika soko.

Akikabidhi muongozo huo kwa katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga na baadaye akawakabidhi maafisa Kilimo, Mratibu mkuu wa utafiti na masoko, Bw Hassan Kibarua amesema ni vema wataalam wa kilimo wakatoa elimu kwa wakulima wa mkonge juu ya kuzingatia ubora kuanzia uzalishaji ili usipungue thamani.

"Mkonge unatakiwa kuchakatwa si zaidi ya masaa 48 tangu kukatwa lakini kuna wakati mkulima anachakata mkonge uliokatwa zaidi ya siku tano, unakuwa umepungua ubora na unapofika sokoni unakuwa haupo kwenye daraja la ubora wa 3L ambalo lina bei ya juu, " alisema Kibarua.


RUWASA SIMIYU YAAHIDI KUONGEZA HALI YA UPATIKANAJI WA MAJI

Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama Mkoani Simiyu unatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 51 ya mwaka 2019 hadi 57.4 ifikapo 0ktoba 2020 kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo (P4R ) hali itakayosaidia wananchi kuepukana na adha ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa uhakika na urahisi. 

Hayo yamesemwa Septemba 11, 2020 na meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) mhandisi Mariam Majala wakati wa makabidhiano ya mabomba yatakayotumika kutekeleza miradi ya maji Mkoani Simiyu yaliyofanyika katika ofisi za RUWASA mjini Bariadi.

“Tayari tumepokea mabomba asilimia 70 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo yana thamni ya zaidi ya shilingi milioni 800, tunaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa mradi wa P4R na tunaamini tutakapokuwa tumelaza mabomba haya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii na tutakuwa tumeongeza maji kwa asilimia 6.4, kutoka asilimia 51 hadi 57.4,” alisema Mhandisi Manjala. 

Naye  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amewapongeza watendaji wa RUWASA Mkoa wa Simiyu kwa namna wanavyotekeleza miradi kwa kasi huku akibainisha kuwa mradi wa P4R utatoa ajira kupitia utandazaji wa mabomba hivyo akatoa wito kwa Wana Simiyu kuchangamkia fursa hiyo ya ajira pamoja

Aidha, Mmbaga ametoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu hiyo ya maji itakayotandazwa katika maeneo hayo kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa P4R ili kuweza kuusaidia mkoa kufikia azma ya kuongeza hali ya upatikanaji wa maji.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Zabuni ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliyotumika kuandaa mchakato wa manunuzi wa mabomba hayo, Bw. Ekwabi Mujungu amesema anawapongeza RUWASA kwa kununua mabomba kulinga na sifa zilizoandishwa na kupitishwa na bodi hiyo huku akisisitiza miradi kwenda kutekelezwa kwa kiwango bora ili thamani ya fedha.

MWISHO

Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA), Mhandisi Mariam Manjala akionesha mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  wakati wa makabidhiano ya mabomba hayo Septemba 11, 2020 Mjini Bariadi, kulia ni Katibu Tawala  wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga.

Katibu Tawala  wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  wakati wa makabidhiano ya mabomba hayo Septemba 11, 2020 Mjini Bariadi, kushoto Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA), Mhandisi Mariam Manjala.
Sehemu ya mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  mkoani Simiyu.

 

Mjumbe wa Bodi ya Zabuni ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliyotumika kuandaa mchakato wa manunuzi wa mabomba hayo, Bw. Ekwabi Mujungu akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  wakati wa makabidhiano ya mabomba hayo Septemba 11, 2020.

Katibu Tawala  wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  wakati wa makabidhiano ya mabomba hayo Septemba 11, 2020 Mjini Bariadi, kushoto Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA), Mhandisi Mariam Manjala

 Katibu Tawala  wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabomba yanayotarajiwa kusambazwa katika wilaya zote kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa lipa kulingana na matokeo(P4R)  wakati wa makabidhiano ya mabomba hayo Septemba 11, 2020 Mjini Bariadi, wa pili kushoto Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA), Mhandisi Mariam Manjala                 

 


Friday, September 11, 2020

KITUO CHA AFYA LUKUNGU CHATAKIWA KUIMARISHA MFUMO WA UKUSANYAJI, USIMAMIZI WA MAPATO

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba ameutaka uongozi wa Kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega kuimarisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato (kudhibiti upotevu wa mapato) ili kuongeza mapato yatakayosaidia kununua dawa na kuboresha miundombinu kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Kulemba ameyasema hayo Septemba 10, 2020 katika nyakati tofauti wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi iliyofanyika katika kituo hicho, ambapo moja ya malengo ya ziara ilikuwa ni kukagua mifumo ya ukusanyaji wa mapato na hali ya utoaji wa huduma za afya kwa ujumla wake.

“Imarisheni mfumo wa ukusanayaji mapato nataka wakati ujao mapato yaongezeke mara mbili ya sasa, mkumbuke kuwa kwa kadri tunavyodhibiti upotevu wa mapato ndiyo tutakavyoboresha utoaji wa huduma; tutaweza kununua dawa na kufanya maendeleo ya kituo chetu hali itakayochangia kuongeza ufanisi katika huduma zinazotolewa kwa wananchi,” alisema Kulemba.

Ameongeza kuwa Uongozi wa Kituo hicho unapaswa kuhakikisha kuwa mfumo wa GoT-HOMIS unaohusika na usimamizi na uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya unafungwa na kufanya kazi kituoni hapo, ili kudhibiti aina yoyote ya upotevu wa mapato kwa kuwa taarifa ya kila huduma na mapato zitaingizwa katika mfumo huo.

Naye Afisa Afya kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema pamoja na kuimarisha mfumo wa mapato uongozi huo uboreshe mazingira kwa kusafisha mara kwa mara maeneo ya kituo hicho pamoja na kupanda bustani za maua.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa idara ya afya wilaya ya Busega, Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya amesema watatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na mganga mkuu wa mkoa ili kutimiza azma ya serikali ya kutoa huduma zinazotakiwa kwa wananchi na kwa wakati.

Baadhi ya wananchi waliopata huduma za matibabu katika kituo cha afya Lukungu wameupongeza uongozi wa kituo kwa namna ulivyoboresha utoaji wa huduma na kuomba hali ya upatikanaji wa dawa iimarishwe zaidi na miundombinu ya kutoa huduma ikiwemo huduma za upasuaji, wodi za kulaza wagonjwa ziongezwe  ili wapate huduma zote kituoni hapo.

“ Kwa upande wa huduma mimi nimehudumiwa vizuri, nimepokelewa vizuri na wauguzi wamenisikiliza baada ya kunisikiliza nimeenda kwenye vipimo na nilivyorudi kwa daktari amenieleza tatizo langu akaniandikia dawa,  nashukuru dawa zote nilizoandikiwa nimepewa,” Mandege William Manyama, mkazi wa Kijiji cha Lukungu.

“Huduma zote nilizokuwa nazihitahitaji nimezipata na nimehudumiwa ndani ya muda mfupi, ombi langu serikali ione namna ya kuongeza huduma hasa za kulaza wagonjwa ili tuipate hapa hapa badala ya kupelekwa kwenye vituo vingine na hospitali,” alisema Daud Moshi mkazi wa Kijiji cha Lukungu.

MWISHO


Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(katikati) akitoa maelekezo kwa  baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(kulia) akifanya ukaguzi katika wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba akitoa maelekezo kwa  baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Mfamasia wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akichangia jambo katika kikao kati ya Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Busega pamoja na watumshi wa Kituo cha Afya Lukungu wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(katikati) akitoa maelekezo kwa  baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Baadhi ya wananchi wakisubiri huduma katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega.

Jengo la huduma za wagonjwa wa nje katika Kituo cha Afya cha Lukungu wilayani Busega

Baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Lukungu wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo kwa  watoa huduma hao wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Afisa Afya katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  akichangia jambo katika kikao kati ya Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Busega pamoja na watumshi wa Kituo cha Afya Lukungu wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.

Afisa Afya katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  akichangia jambo katika kikao kati ya Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Busega pamoja na watumshi wa Kituo cha Afya Lukungu wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10, 2020.

Moja ya majengo ya kutolea huduma katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega.

Wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega.



Baadhi ya Maafisa wa Idara ya Afya mkoa wa Simiyu na Wilayani ya Busega na watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Lukungu wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo kwa  watoa huduma hao wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.


Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba na Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao cha Idara ya Afya mkoa wa Simiyu na Wilayani ya Busega na watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Lukungu kilichofanyika wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(kulia) akitoa maelekezo kwa  baadhi ya watoa huduma za afya katika kituo cha Afya Lukungu wilayani Busega wakati akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika kituo hicho Septemba 10,  2020.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!