Thursday, September 24, 2020

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 2.3 ZATOLEWA KWA WALENGWA WA TASAF 28984 SIMIYU

Serikali imetoa jumla ya shilingi 2,327,259,225 kwa walengwa  wa TASAF III awamu ya pili wapatao  28984 kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini katika kipindi cha mwezi Julai hadi Oktoba mwaka 2020 katika vijiji 376 mkoani Simiyu. 

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa TASAF mkoa wa Simiyu, Bw. Nyasilu Ndulu  Septemba 23, 2020 wakati wa zoezi la uhawilishaji fedha kwa walengwa wa TASAF wa kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu. 

“Fedha za walengwa tulizopokea ni shilingi 2,327,259,225 na hizi ni fedha za awamu mbili, mwezi Julai-Agosti na Septemba-Oktoba na zinalipwa kwa awamu moja;  fedha hizi zimefika kipindi muafaka cha maandalizi ya msimu wa kilimo nawashauri wazitumie vema katika maandalizi ya shughuli za kilimo lakini wajiwekee utaratibu wa kuwekeza kwenye shughuli za uzalishaji,” alisema Nyasilu. 

Akizungumza na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mwamishali  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ametoa rai kwa walengwa wao kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha hiyo ya ruzuku wanayopata ili waweze kufikia malengo yao. 

“Ninawasihi muendelee kujiamini na kila mmoja atambue kuwa anaweza, uwezeshaji ndiyo huu umeletwa na serikali hivyo ni kila mmoja akijiamini kuwa atafanikiwa kupitia kazi anayofanya atafanikiwa, kama mtu anafuga kuku, mbuzi, au ng’ombe akiwatunza vizuri akisaidiwa na wataalam wa halmashauri mtakuza vipato vyenu na mtafikia malengo yenu,” alisema Mmbaga. 

Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Kija Kayenze amesema ruzuku ya  fedha zilitolewa kwa walengwa wa TASAF zimefika katika kipindi muafaka, ambapo msimu wa kilimo unatarajiwa kufunguliwa Oktoba Mosi; huku akitoa wito kwa walengwa kutumia fedha hizo katika uandaaji wa mashamba, ununuzi wa mbegu bora ili waweze kupata mavuno bora. 

Nao baadhi ya walengwa wa TASAF wameishukuru Serikali kwa kutoa ruzuku ya fedha ambazo zimewasaidia kuanzisha miradi midogo midogo hususani katika kilimo, ufugaji na ujasirimali ambayo inawawezesha kupata mahitaji yao ya kila siku na kuweka akiba kwa ajili ya baadaye. 

“Naishukuru serikali kutusaidia kupitia TASAF, nilikuwa nafanya vibarua kupata hela ya matumizi na kuwanunulia wanangu mahitaji ya shule, lakini nilipoanza kupata hela za TASAF nikawa nazitunza baadaye nikanunua ng’ombe wawili ambao sasa hivi wamezaa, nategemea kuwauza wawili ili ninunue bati za kuezeka nyumba yangu na kupata mtaji,” alisema Sikitu Zengo mkazi wa Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu.

MWISHO

Bi. Sikitu Zengo(kulia) mlengwa wa TASAF III awamu ya pili kutoka Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu akipokea fedha za ruzuku inayotolewa kwa kaya maskini kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.
Bi. Sikitu Zengo mlengwa wa TASAF III awamu ya pili kutoka Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu akionesha ng’ombe aliwanunua kwa  fedha za ruzuku inayotolewa kwa kaya maskini kwa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wilaya  ya Meatu (hawapo pichani) wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga baada ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akizungumza na walengwa wa TASAF III Awamu ya Pili wa Kijiji cha Mwamishali wilayani humo kabla ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu, Bw. Nyasilu Ndulu akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wilaya  ya Meatu wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kushoto)  kabla ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.
Baadhi ya walengwa wa TASAF III Awamu ya Pili wa Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani humo.
Mmoja wa walengwa wa TASAF III awamu ya pili kutoka Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu akipokea fedha za ruzuku inayotolewa kwa kaya maskini kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akizungumza na walengwa wa TASAF III Awamu ya Pili wa Kijiji cha Mwamishali wilayani humo kabla ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.

 

Baadhi ya walengwa wa TASAF III Awamu ya Pili wa Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani humo.

Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu, Bw. Nyasilu Ndulu (wa tatu kushoto)  akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wilaya  ya Meatu wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (wa pili kushoto)  kabla ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.

Baadhi ya walengwa wa TASAF III Awamu ya Pili wa Kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga(kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 katika kijiji cha Mwamishali wilayani Meatu.
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu, Bw. Nyasilu Ndulu akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wilaya  ya Meatu wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Miriam Mmbaga (kushoto)  kabla ya uzinduzi wa zoezi la uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini Septemba 23, 2020 wilayani Meatu.

 


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!