Serikali mkoani Simiyu imesema
imekusudia kuiimarisha shule ya Sekondari ya Bariadi ambayo ilitengwa kuwa
Shule ya Michezo, kwa kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike na wa kiume na
kuiwekea miundombinu yote muhimu, ikiwemo viwanja vya michezo yote kwa
lengo la kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipokuwa akifunga mashindano ya UMISSETA na
UMITASHUMTA kimkoa katika viwanja vya Shule ya sekondari ya Wasichana Maswa.
"Ningehitaji tuifanye Shule ya
Sekondari Bariadi kuwa shule maalum ya kimichezo ya Kimkoa, yenye mabweni ya
wavulana na wasichana na tuiwekee miundombinu yote ya michezo ili watoto wote
wenye vipaji vya michezo waende pale na nitaomba kibali walimu wa michezo
wahamie hapo, tufike mahali ambapo Bariadi Sekondari itatoa wachezaji wa
kutumainiwa kwenye Taifa" amesema Mtaka.
Aidha, amewataka wanafunzi wote kuwa na
mtazamo tofauti katika michezo kwa kuondokana na nadharia ya kuwa michezo ni
afya, burudani na kwenda kwenye dhana ya michezo kama taaluma, ajira na
biashara, ambapo amehimiza kuwa mkoa huo unafanya uwekezaji na mapinduzi ya
michezo kibiashara katika Shule hiyo.
Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka
wanafunzi hao kuuwakilisha vema mkoa na kuwatakia heri na ushindi katika
mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa yatakayofanyika jijini
Mwanza, huku akiwataka kuwa na nidhamu kipindi chote watakachokuwa huko na
akaahidi kutoa zawadi mbalimbali kwa washiriki wote watakaporudi na ushindi.
Katika hatua nyingine Mtaka akiwakabidhi
walimu na wanafunzi jezi zilizotolewa kwa udhamini wa Halmashauri ya Wilaya ya
Maswa, kupitia mradi wake wa Kiwanda cha Chaki (MASWA CHALKS) amewataka Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi mkoani humo kujipanga kwa ajili ya kudhamini
mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA mwaka 2019 kupitia miradi inayotekelezwa
kwenye maeneo yao ili kuendelea kuutangaza mkoa huo.
Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius
Nestory amesema changamoto kubwa zilizowakabili washiriki wa mashindano hayo ni
pamoja na upungufu wa viwanja katika shule za msingi na sekondari na kukosa
wafadhili kutoka nje ili kuwezesha wanafunzi kukaa kambini muda mrefu kujiandaa
na mashindano.
Kwa upande wao wanafunzi/ washiriki wa
UMISSETA na UMITASHUMTA mkoa wa Simiyu wamemhakikishia Mkuu mkoa na wananchi
kwa ujumla kuwa watarudi na ushindi katika mashindano hayo Kitaifa.
"Mwaka 2018 tumejipanga na ushindi
ni lazima kwa mwaka huu sisi tunaenda Mwanza kushinda na kuchukua makombe,
tunamhakikishia Mkuu wa Mkoa na wananchi wote wa Simiyu kuwa tunarudi na
ushindi" Alisema Mwanaidi Khamis kutoka Maswa.
Jumla ya washiriki 811 wa michezo
mbalimbali kutoka katika Halmashauri zote Sita za Mkoa wa Simiyu wameshiriki
mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa kwa mwaka 2018.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia) akikabidhi kombe la msindi wa jumla michezo
ya UMISSETA kimkoa mwaka 2018 kwa Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya
Busega, Mwl. Yassin Kitentya wakati wa kufunga mashindano ya UMISSETA
UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wanamichezo katika hafla ya kufunga
Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA katika
viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa nne kulia) na baadhi ya wana michezo wakionesha jezi
zilizotolewa na Kiwanda cha MASWA CHALK kama udhamini katika michezo ya
UMISSETA na UMITASHUMTA, wakati wa kufunga mashindano ya UMISSETA UMITASHUMTA
katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe (wa nne kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia), wakati wa kufunga mashindano ya UMISSETA
UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa .
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe (wa nne kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia), wakati wa kufunga mashindano ya UMISSETA
UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtakaakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
washiriki wa michezo, mara baada ya kufunga Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA kimkoa katika
viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Wanamichezo kutoka
Wilaya ya Busega wakionesha onesho lao la ngoma za asili mbele ya Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu na Viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mashindano hayo katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick
Sagamiko akitoa taarifa ya vitu ambavyo kiwanda cha Maswa Chalks
Kimedhamini katika Mashindano ya
UMISSETA na UMITASHUMTA kimkoa, wakati wa kufunga mashindano hayo katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa na baadhi ya viongozi na wawakilishi wa
wanamichezo wakionesha jezi zilizotolewa na Kiwanda cha MASWA CHALK kama mdhamini
katika michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA, wakati wa kufunga mashindano ya
UMISSETA UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akionesha moja ya jezi zilizotolewa na Kiwanda
cha MASWA CHALK kama mdhamini katika michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA, wakati
wa kufunga mashindano ya UMISSETA UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mashindano
ya UMISSETA na UMITASHUMTA kimkoa, mara baada ya kufunga mashindano hayo katika
viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya
wanamichezo mara baada ya kufunga Mashindano
ya UMISSETA na UMITASHUMTA kimkoa katika
viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.