Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amesema dhamira ya Kanda mpya ya Maonesho
ya Kilimo na Sherehe za Nane Nane ya Ziwa Mashariki inayojumuisha mikoa ya
Simiyu, Mara na Shinyanga ni kuwa na Uwanja wa Nanenane utakaofanya Maonesho ya Kilimo Biashara.
Mtaka amesema hayo wakati akifungua kikao cha Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ya Kanda
ya Ziwa Mashariki yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi kilichowakutanisha
Wakuu wa Mikoa mitatu ,Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri na
Sekretarieti za Mikoa hiyo, ambacho kilifanyika mjini Bariadi.
Amesema pamoja na kufanya maonesho ya Kilimo Nanenane ambayo huwa yanafanyika
kuanzia Agosti Mosi hadi Agosti 08 kila mwaka, kutafanyika Maonesho mengine mara nne kwa
mwaka pamoja na matukio mengine yatakayofanyika katika uwanja huo ili kuwe na
tija kwa Halmashauri kuwekeza fedha
katika uwanja huo.
“Haiwezekani Halmashauri zetu zikawekeza katika uwanja wa NaneNane halafu
uwanja uwe unatumika kila tarehe 01 hadi 08 mwezi wa nane kila mwaka tu, ni
lazima tuwe na viwanja ambavyo vitafanya
maonesho ya kilimo biashara lakini eneo lile ukiacha maonesho haya ya NaneNane
tutafanya maonesho mara nne kwa mwaka” alisema.
Ameongeza kuwa ili kuendana na hali ilivyo sasa ni vema Halmashauri
zikakubaliana kujenga jengo la maonesho (exhibition
hall) na kuwa na maeneo ya nje kwa ajili ya vipando na mifugo kama ilivyopendekezwa
katika vikao vya awali, badala ya
kutumia vibanda na mahema kama ilivyozoeleka, ili kuifanya Nane Nane ya Kanda
Mpya ya Ziwa Mashariki kuwa ya tofauti.
Katika kikao hicho, Halmashauri 21 za Mikoa
ya Mara, Shinyanga na Simiyu zimeagizwa kuwasilisha mchango
wa kiasi cha shilingi milioni 20 ndani ya siku saba kwa ajili ya malipo ya awali ya ujenzi wa jengo la maonesho, huku
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akiwataka Wakurugenzi kutelekeleza agizo
hilo.
“.....tumekubaliana kuwa kila Halmashauri itatoa shilingi milioni 20 na
hili si jambo la masihara... ndani ya siku
saba tukitoka hapa kila Mkurugenzi atakuja na hundi yake ya shilingi milioni
20, ili itakapofika Juni Mosi haya mambo yakamilike” alisema Malima.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe.
Glorius Luoga ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote katika mikoa hiyo
kuwa wabunifu katika kuhakikisha fedha za kuwezesha ujenzi wa jengo hilo linalotarajiwa
kugharimu jumla ya shilingi bilioni 2.1 zinapatikana.
Hivi karibuni Wizara ya kilimo imetangaza Kanda Mpya ya Maonesho ya
Nanenane ijulikanayo kama Kanda ya Ziwa Mashariki, ambayo inajumuisha mikoa ya
Simiyu, Mara na Shinyanga na Uwanja utakaotumika kwa ajili ya Maonesho hayo uko
Eneo la Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo mwaka 2018 Kanda hiyo
itakuwa mwenyeji wa maonesho hayo kitaifa.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akifungua kikao cha
viongozi na wataalam wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga katika kikao maalum cha Maandalizi ya
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa
Mashariki, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Musoma mkoani , Mhe.Dkt. Vicent Naane akichangia hoja katika kikao cha viongozi
na wataalam wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga katika kikao maalum cha Maandalizi ya
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa
Mashariki, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wakuu wa
Wilaya na viongozi wengine wakifuatilia kikao
cha viongozi na wataalam wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga katika kikao maalum cha Maandalizi ya
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa
Mashariki , kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima Mkoani Simiyu, Mhe. Benson
Kilangi akichangia hoja katika kikao cha viongozi na wataalam wa mikoa ya
Simiyu, Mara na Shinyanga katika kikao
maalum cha Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki , kilichofanyika i Mjini
Bariadi.
Baadhi ya Wakurugenzi
wa Halmashauri na Maafisa wakifuatilia kikao cha viongozi na wataalam wa mikoa
ya Simiyu, Mara na Shinyanga katika
kikao maalum cha Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki inayohusisha mikoa kilichofanyika Mjini
Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Tarime mkoani Mara, Mhe.Glorius Luoga akichangia hoja katika kikao cha viongozi
na wataalam wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga katika kikao maalum cha Maandalizi ya
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa
Mashariki inayohusisha mikoa hiyo
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa
Sekretarieti ya Mkoa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kikao cha
viongozi na wataalam wa mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga katika kikao maalum cha Maandalizi ya
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa
Mashariki inayohusisha mikoa hiyo kilichofanyika
Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment