Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
ameishauri Mamlaka ya Chakula na Dawa hapa nchini (TFDA) kufungua Ofisi katika
Mikoa ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza ufanisi hususani
katika kipindi hiki ambacho Serikali ya awamu ya Tano inahimiza utekelezaji wa
ajenda ya Viwanda.
Mtaka ameyasema hayo Mei 23 wakati
akifungua kikao kazi cha Wahariri na waandishi wa habari wa mikoa ya Simiyu na
Mara kilicholenga kuhamasisha Sheria ya Chakula, dawa na vipodozi sura Na.219, ambacho
kilifanyika Mjini Bariadi.
Amesema wakati huu ambao Sera ya Viwanda
ni kipaumbele cha nchi ni vema Ofisi za TFDA zikawepo katika kila Makao Makuu
ya mkoa ili pale watu wanapotaka kujenga
viwanda vitakavyozalishwa dawa, chakula na vipodozi waweze kupata huduma
zinazotakiwa kwa wakati badala ya kufuata huduma katika ofisi za kanda.
“Mhe. Rais anapohimiza ajenda ya viwanda
kwenye nchi TFDA inabidi ione umuhimu wa kuwa na Ofisi kwenye mikoa, ili mfano watu
wa Simiyu wanapohitaji kufungua kiwanda cha bidhaa ambazo zinaihusu TFDA
wasilazimike kwenda Mwanza kufauta huduma” alisema.
Aidha, Mtaka ameishauri Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini - TFDA
kutoa ufafanuzi wa mara kwa mara kuhusu dawa, chakula na vipodozi kupitia
vyombo vya habari, ili jamii iweze kuwa na uelewa mpana wa madhara yatokanayo
matumizi na bidhaa bandia na zenye madhara kwa binadamu.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa waandishi wa habari
baada ya kupata mafunzo kutoka TFDA kuwa mabalozi wazuri wa TFDA katika kufafanua masuala yote
yenye sintofahamu na kuandika habari za kiuchunguzi zilizofanyiwa utafiti kuhusu
dawa, chakula na vipodozi.
Naye
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi Agnes Sitta Kijo amewataka Waandishi wa
habari kutoa taarifa pale wanapobaini uwepo bidhaa ambazo si salama kwa
matumizi ya binadamu huku akiwasisitiza kujikita katika uandishi wa Habari za kiuchunguzi.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho kutoka Mikoa ya Simiyu na Mara
wamesema mafuzo waliyapata yamewasaidia kupata uelewa wa Sheria ya ya Chakula,
dawa na vipodozi sura Na.219 na masuala mbalimbali yahusuyo chakula, dawa na
vipodozi hivyo watakuwa mabalozi wazuri watakaowasaidia wananchi kupata uelewa
juu ya masuala hayo.
“ Elimu niliyoipata imenisaidia na kupitia elimu hii kuhusu masuala ya
chakula, dawa na vipodozi mimi kama mwandishi nitakuwa balozi mzuri ili kuwasaidia
wananchi kujua madhara ya bidhaa zisizo salama kwa afya ya binadamu” alisema
Shushu Joel kutoka Simiyu.
“Mafunzo haya yatatusaidia waandishi habari kujikita katika kuandika habari
za kiuchunguzi zitakazowasaidia wananchi kujua madhara ya bidhaa zisizo salama
kwa afya ya binadamu ” alisema Frankius Cleopas Mwandishi kutoka mkoani Mara.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka akifungua kikao kazi cha Wahariri na waandishi wa habari wa mikoa ya Simiyu
na Mara kilicholenga kuhamasisha wa sheria ya Chakula, dawa na vipodozi sura Na.219,
ambacho kilifanyika Mjini Bariadi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi Agnes
Sitta Kijo akizungumza na Wahariri na waandishi wa habari wa mikoa ya Simiyu na
Mara katika kikao kazi kilicholenga kuhamasisha wa sheria ya Chakula, dawa na
vipodozi sura Na.219, ambacho kilifanyika Mjini Bariadi
Baadhi ya Wahariri na waandishi wa
habari wa mikoa ya Simiyu na Mara katika wakiwa katika kikao kazi kilicholenga
kuhamasisha wa sheria ya Chakula, dawa na vipodozi sura Na.219, ambacho
kilifanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wahariri na waandishi wa
habari wa mikoa ya Simiyu na Mara katika wakiwa katika kikao kazi kilicholenga
kuhamasisha wa sheria ya Chakula, dawa na vipodozi sura Na.219, ambacho
kilifanyika Mjini Bariadi.
Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa TFDA, Bi Agnes Sitta Kijo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga wakifuatilia kikao kazi cha
wahariri na waandishi wa habari wa mikoa ya Simiyu na Mara kilicholenga
kuhamasisha wa sheria ya Chakula, dawa na vipodozi sura Na.219, ambacho
kilifanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Maafisa kutoka Mamlaka ya
Chakula na Dawa(TFDA) wakiteta jambo katika kikao kazi cha wahariri na
waandishi wa habari wa mikoa ya Simiyu na Mara kilicholenga kuhamasisha wa
sheria ya Chakula, dawa na vipodozi sura Na.219, ambacho kilifanyika Mjini
Bariadi.
0 comments:
Post a Comment