Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, mhe.Anthony Mtaka amewahakikishia wazazi wote mkoani humo kuwa
Serikali itawalinda na kuwatunza watoto wote kwa muda wa siku zote watakaokuwa
katika Kambi za Kitaaluma kwa Kidato cha Nne na Darasa la Saba, ambazo zinazotarajiwa
kuanza rasmi mapema mwezi Juni mwaka huu kwa mkoa mzima.
Mtaka
ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wenyeviti wa Kamati na Bodi za Shule
katika Shule ya Msingi Mshikamano Wilayani Meatu katika kikao maalum
kilicholenga kujadiliana juu ya maandalizi
ya Kambi hizo Wilayani humo.
Amesema Serikali imebeba dhamana
ya kuwaweka wanafunzi kambini kwa lengo
la kuwaandaa vema ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao na kuongeza
ufaulu, hivyo haitawafumbia macho wale wote watakaoonekana kwa njia moja ama
nyingine kuharibu jitihada hizo.
“Nawaambia hapa wananchi wa
Meatu, kambi za wanafunzi wetu za kitaaluma mziogope kama ukoma, sisi hatuwezi
kubeba dhamana ya watoto wa watu kwenda kwenye makambi halafu aje mtu
anajipitisha pitisha kwenye kambi kufuatilia na kutaka kuwarubuni watoto wetu
wa kike, nawaeleza hapa mtakuwa halali ya polisi” alisema Mtaka.
Ameongeza kuwa wakati wote
wanafunzi watakapokuwa kambini Serikali itawawezesha walimu kupata stahili zao
kutekeleza majukumu yao na kwa kushirikiana na wadau wengine itatoa mahitaji
maalum kwa wanafunzi wa kike, hivyo akawataka wazazi kujiandaa kuchangia
chakula kwa ajili ya watoto wao ambacho ni sehemu ya kile ambacho kingetumika
wakiwa nao nyumbani.
Aidha, Mtaka amewataka wazazi,
walimu kushikamana na Serikali katika kufikia azma ya kufanya mapinduzi ya
Elimu mkoani Simiyu kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake badala ya kuwatupia
lawama walimu pekee kila wanafunzi wanapofanya vibaya katika mitihani yao, kwa
kuwa ufaulu wa mwanafunzi unategemea ushirikiano
katika ya walimu, wazazi na wanafunzi.
Kwa upande wao Wenyeviti wa Bodi
na Kamati za Shule wamepongeza kuwepo kwa kambi hizo za Kitaaluma na wakakiri
kuwa kambi hizo zinaweza kuwa suluhu ya kuondokana na daraja la nne na sifuri
kwa kidato cha nne na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba na
wakatoa maoni yao.
“ Binafsi nampongeza Mkuu wa mkoa
kwa kuja na wazo hili la kufanya makambi ya kitaaluma kwenye mkoa wetu,
napendekeza kambi hizi zisiishie kwenye hizo siku 21 za mwezi wa sita tu, wazazi tushikamane tuchange chakula watoto
wetu wakae kambi hata mwezi wa tisa” alisema Mchungaji Fabian Kuzenza.
“Naunga mkono kuwepo makambi ya
kitaaluma na namsukuru Mkuu wa Mkoa kuzungumza na sisi, hii imetusaidia kuwa na uelewa wa pamoja
naomba pia atusaidie wajumbe wetu wa kamati za shule wapewe mafunzo wawe na
uelewa mpana wa masuala mbalimbali, ili wawe wanawaeleza wazazi mambo wanayoyafahamu”
Elias Kamweji Mwenyekiti Kamati ya Shule ya Msingi Paji.
Mwezi Juni mwaka huu Wilaya zote
mkoani Simiyu zitafungua Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne na
Darasa la Saba kwa muda wa siku 21 na katika siku hizo wanafunzi wote watafanya
mtihani wa majaribio kwa ajili ya maandalizi ya Mitihani ya Kitaifa iliyo mbele
yao
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wenyeviti wa Kamati na Bodi za Shule za Wilaya ya Meatu (hawapo
pichani) , katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa
wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la Saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi
Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya msingi Mshikamano
Baadhi ya Wenyeviti wa
Bodi na Kamati za Shule wa Wilaya ya Meatu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao maalum cha maandalizi
ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la saba
zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya msingi
Mshikamano
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani ( wa kwanza mstari wa mbele) na viongozi wengine wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na
Wenyeviti wa Kamati na Bodi za Shule za
Wilaya hiyo (hawapo pichani) , katika
kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha
nne na Darasa la Saba, kilichofanyika Shule ya msingi Mshikamano.
Mchungaji Fabian
Kuzenza akichangia hoja katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka na Wenyeviti wa Kamati na Bodi za
Shule za Wilaya ya Meatu (hawapo pichani) , katika kikao maalum cha maandalizi
ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la Saba zinazotarajiwa
kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya msingi Mshikamano,
Bi.
Minza Sibaba Mjumbe Bodi ya Shule Nyanza akichangia hoja katika kikao cha Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Wenyeviti wa Kamati na Bodi za Shule za Wilaya ya Meatu (hawapo
pichani) , katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa
wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la Saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi
Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya msingi Mshikamano.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza akifafanua jambo katika kikao
cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Wenyeviti wa Kamati na Bodi za Shule za Wilaya hiyo, katika kikao
maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na
Darasa la Saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika
Shule ya msingi Mshikamano.
Baadhi ya Wenyeviti wa
Bodi na Kamati za Shule wa Wilaya ya Meatu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi
za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la saba zinazotarajiwa
kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya msingi Mshikamano.
0 comments:
Post a Comment