Mkurugenzi Mkuu
wa Bodi ya Pamba nchini Marco Mtunga amewaonya wanunuzi wa Pamba watakaonunua
pamba nje ya mfumo wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) na kuwa endapo
watabainika Pamba hiyo itataifishwa na Serikali.
Onyo hilo
limetolewa Mkoani Simiyu katika kikao baina ya Viongozi wa mkoa huo, viongozi
wa vyama vya ushirika vya Msingi (AMCOS), wanunuzi wa Pamba na Naibu
Mrajisi kutoka Tume ya Maendeleo ya
Ushirika Dodoma Charles Malunde, lengo likiwa ni kukumbusha juu ya uadilifu katika
masuala ya ununuzi wa pamba, ikiwa ni maandalizi wa ununuzi pamba baada ya
msimu kufunguliwa.
Mtunga amesema mwaka huu Serikali imefanya uamuzi
kwamba pamba yote itakayozalishwa hapa nchini itanunuliwa kupitia Vyama vya
Msingi (AMCOS) jambo ambalo amesema limeelezwa vizuri katika mwongozo wa bodi.
“Tunawatahadharisha wanunuzi wa pamba kufuata
mfumo wa ununuzi wa pamba uliowekwa na Serikali, pamba yote itakayokamatwa ikiwa
haikununuliwa kupitia Chama cha Ushirika cha Msingi itataifishwa na
Serikali, katika mwongozo tulioutoa
maelekezo hayo yapo na yako chini ya sheria Namba 2 ya pamba ya mwaka 2001”
alisema Mtunga.
Kwa upande wake Naibu Mrajisi kutoka Tume ya
Maendeleo ya Ushirika Dodoma Charles Malunde amewataka viongozi wa Vyama vya
ushirika kuepuka aina yoyote ya wizi na ubadhilifu wa kutumia udanganyifu wa
kuwaibia wakulima kwa kuziharibu mizania.
Aidha, Malunde amesisitiza sheria na taratibu za
Ushirika zizingatiwe katika uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi, hivyo
akawataka viongozi wote waliochaguliwa kuongoza vyama hivyo ambao wana shutuma
zozote, watumishi wa Umma au Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa kuachia
mara moja nafasi hizo kwa kuwa hawana sifa kwa mujibu wa sheria.
Baadhi ya viongozi wa AMCOS waliwasilisha masuala
mbalimbali kama maombi yao kwa Serikali kuhusiana na ununuzi wa pamba ikiwa ni
pamoja na kuomba vyama vya ushirika vya msingi vipya vilivyo katika hatua ya usajili vikamilishiwe usajili
ili viweze kuingia katika mfumo huu wa ununuzi wa pamba.
Akihitimisha kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Anthony Mtaka amesema anatamani kuona ushirika wenye mtazamo wa kujibu
changamoto na mahitaji ya wakulima wa pamba, huku akitoa angalizo kwa viongozi
wa AMCOS watakaofanya ubadhilifu wa fedha za Vyama vya Ushirika kuwa Serikali mkoani
humo itawachukulia hatua kali.
“Ushirika wa Simiyu (is my own baby) ni mtoto
wangu mwenyewe, ni kitu ambacho nilitamani kuona kinatokea, Wanaushirika
wakakaokosa uadilifu wajihesabu kuwa wafungwa watarajiwa, nawaambia nitawafunga
na sitanii nitawafunga” alisisitiza Mtaka.
Katika hatua nyingine amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mji wa Bariadi kuaandaa eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Chama Kikuu cha
Ushirika Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga
akizungumza na Viongozi wa mkoa wa Simiyu, viongozi wa Vyama vya Ushirika vya
Msingi (AMCOS), wanunuzi wa Pamba na baadhi ya viongozi wa Tume ya Maendeleo
katika kikao kazi kilichofanyika Mjini Bariadi, lengo likiwa ni kukumbusha juu
ya uadilifu katika ununuzi wa pamba, ikiwa ni maandalizi wa ununuzi baada ya
msimu kufunguliwa.
Naibu Mrajisi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Dodoma Charles Malunde akizungumza na Viongozi
wa mkoa wa Simiyu, viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS), wanunuzi
wa Pamba na baadhi ya viongozi wa Tume ya Maendeleo katika kikao kazi
kilichofanyika Mjini Bariadi, lengo likiwa ni kukumbusha juu ya uadilifu katika
ununuzi wa pamba, ikiwa ni maandalizi wa ununuzi baada ya msimu kufunguliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa mkoa wa Simiyu, viongozi wa Vyama
vya Ushirika vya Msingi (AMCOS), wanunuzi wa Pamba na baadhi ya viongozi wa
Tume ya Maendeleo katika kikao kazi kilichofanyika Mjini Bariadi, lengo likiwa
ni kukumbusha juu ya uadilifu katika ununuzi wa pamba k ikiwa ni maandalizi wa
ununuzi baada ya msimu kufunguliwa.
Abeli Michael wa Chama cha Msingi Wilayani Meatu akizungumza katika kikao cha Viongozi wa mkoa
wa Simiyu, viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS), wanunuzi wa Pamba
na baadhi ya viongozi wa Tume ya Maendeleo , kilichofanyika Mjini Bariadi,
lengo likiwa ni kukumbusha juu ya uadilifu katika ununuzi wa pamba ikiwa ni maandalizi wa ununuzi baada ya msimu
kufunguliwa.
Baadhi ya viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
(AMCOS) Mkoani Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa
katika kikao kati ya viongozi hao na Viongozi na watendaji wa Serikali mkoani
humo, wanunuzi wa Pamba na baadhi ya viongozi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,
kilichofanyika Mjini Bariadi, lengo likiwa ni kukumbusha juu ya uadilifu katika
ununuzi wa pamba, ikiwa ni maandalizi wa
ununuzi baada ya msimu kufunguliwa
.Baadhi ya viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
(AMCOS) Mkoani Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa
katika kikao kati ya viongozi hao na Viongozi na watendaji wa Serikali mkoani
humo, wanunuzi wa Pamba na baadhi ya viongozi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,
kilichofanyika Mjini Bariadi, lengo likiwa ni kukumbusha juu ya uadilifu katika
ununuzi wa pamba, ikiwa ni maandalizi wa
ununuzi baada ya msimu kufunguliwa.
wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa
yakijadiliwa katika kikao kati ya viongozi hao na Viongozi na watendaji wa Serikali
mkoani humo, wanunuzi wa Pamba na baadhi ya viongozi wa Tume ya Maendeleo ya
Ushirika, kilichofanyika Mjini Bariadi, lengo likiwa ni kukumbusha juu ya
uadilifu katika ununuzi wa pamba, ikiwa
ni maandalizi wa ununuzi baada ya msimu kufunguliwa.
0 comments:
Post a Comment