Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo, tarehe 11/06/2021 alifungua rasmi,michezo ya UMISSETA Mkoa, michezo ambayo ilikuwa ikifanyika katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Akizungumza Kaimu Afisa Elimu Mkoa Bwn.Charles Maganga alisema mashindano ngazi ya Mkoa yameanza leo 11/6/21 na yatakamilika 13/6/21 kwa kuunda timu ya Mkoa. Kauli mbiu ya Mashindano haya ya mwaka 2021 ni : “Michezo,Sanaa na Taaluma Kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda”.
Mashindano haya yana jumla ya washiriki 679, kati yao wanafunzi 600,waalimu 61, madaktari 2 na viongozi 16.Washiriki hawa ni kutoka Halmashauri zote za Mkoa.Idadi ya Michezo inayoshindaniwa ni saba na michezo 4 kati ya hiyo inahusisha wavulana na wasichana.Michezo hiyo ni pamoja na Riadha, Mpira wa Miguu, Mpira wa Wavu, Mpira wa Mikono,Mpira wa kikapu, Mpira wa Netiboli na fani za ngoma na kwaya.
Ili kuendesha mashindano kwa ufanisi tumeunda kamati ya ndhamu, afya, usafi na mazingira. Pia tumeunda kamati za michezo.Kamati hizi zina jukumu la kusimamia uendeshaji wa michezo kwa kuzingatia sheria na kanuni za michezo husika.Na wajumbe wa kamati hizi ni waalimu wa michezo husika.Hali ya kambi ni nzuri, hatujakumbanana changamoto
yeyote, wanamichezo wana ari kubwa ya kishindana katika hali ya utulivu, upendo
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa Dkt. Fredrick Sagamiko, alimkaribisha Mgeni rasmi Bi. Kayombo na kumhakikishia kuwa hali ya Maswa ni shwari hivyo wanamichezo wasiwe na wasiwasi kabisa.
Katibu Tawala, Bi. Kayombo ambaye alikuwa mgeni rasmi alikuwa na haya ya kusema;
napenda kuwashukuru Wazazi/ walezi kwa kuwaruhusu wanafunzi kushiriki michezo.Pia niwashukuru wadau mbalimbali kwa kuwezesha maandalizi mazuri.Niwapongeze wanamichezo wote kwa kuunda timu za halmashauri, ni matumaini yangu kuwa vipaji mlivyo vionyesha vitaendelea kuonekana katika mashindano haya yatakayofanyika katika ngazi ya Taifa, Mkoani Mtwara kuanzia 20/6/2021 - 03/7/2021.
Kama ilivyo kauli mbiu ya mwaka. huu Michezo na Sanaa ni sehemu ya Taaluma na maendeleo ya Elimu. Michezo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu na imekuwa chimbuko kubwa la kuzalisha na kukuza wanamichezo mbalimbali wanaounda timu za Taifa. Lengo la michezo hii ni kujenga na kuimarisha umoja, udugu, upendo, mshikamano, hali ya kujiamini, kukuza taaluma na utimamu wa akili kwa wanafunzi.
Tafiti mbalimbali zimebainisha kuwa michezo huchangia katika kuimarisha ushiriki wa wanafunzi kitaaluma kwa kupunguza utoro na kuimarisha afya za wanafunzi.Michezo imesaidia kujenga mshikamano kimkoa kwa kuwaleta pamoja wadau wa elimu na michezo.
Nitoe wito kwa wanafunzi wote watakaochaguliwa kuunda timu ya Mkoa, mzingatie kanuni za michezo, tumieni vipaji vyenu kuhakikisha kuwa tunapata ushindi. Tumieni fursa hiyo kuutangaza mkoa wa simiyu.Waalimu chagueni wanafunzi na sio mamluki kwani itakuwa aibu kwa mkoa.Ikiwa mtawela Mamluki.
Changamoto ya viwanja vya michezo, natoa maelekezo maafisa michezo, kuendelea kupima viwanja vyote vinavyohitajika kwenye maeneo ya shule ili wakuu wa shule waweze kusimamia utengenezaji wa viwanda hivyo kwa kushirikiana na wanafunzi na vitumike wakati wote,tusisubiri tu kipindi cha michezo hii ya UMISSETA.
Akitoa neno la shukrani Bi.Line Chanafi, alisema mgeni rasmi kwa niaba ya wenzangu nikuahidi ushirikiano. Sisi tupo vizuri na tumeanza vizuri na hatuna mamluki, tuna wanafunzi/ wanamichezo halali, tutafanya yote uliyotuagiza na hasa nidhamu.
MWISHO