Mhe. Kafulia amekutana na wadau wa ufugaji wa nyuki Mkoa wa Simiyu ambapo pamoja na mambo mengine alitaka kusikia changamoto zao na namna gani Mkoa unaweza kutatua changamoto hizo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa asali
Akizungumza Afisa Nyuki Mkoa, Bw.Maganga Juakali Ongala katika taarifa yake kwa Mhe. Kafulila alieleza kuwa Mkoa wa Simiyu una vikundi 91 vya ufugaji wa Nyuki.Katika mwaka wa fedha 2019/2020 uzalishaji wa asali kwa Mkoa ulikuwa lita 31,788. Asali hiyo iliyovunwa kutoka Halmashauri zote Sita za Mkoa wa Simiyu, huku Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ikiongoza kwa uzalishaji wa lita 8200.
Pamoja na mafanikio hayo wadau wa ufugaji wa Nyuki mkoani hapa wamekuwa wakikabiliana na Changamoto mbalimbali kama vile, upatikanaji wa soko la asali hii ni ndani na nje ya nchi.Ukosekanaji wa mashine za kuchakata na kupaki asali na hivyo kuomba kukopeshwa vifaa hivyo. Changamoto katika kurina asali na utambuzi wa ukomavu wa Asali hivyo elimu inatakiwa kuwa endelevu kwa wazalishaji.
Aidha Wadau hao waliomba Wafugaji binafsi wa Nyuki wakopeshwe mizinga au vifaa vingine muhimu vya Ufugaji nyuki. Changamoto nyingine ni pamoja na Maeneo ya kufugia nyuki, baadhi ya wafugaji nyuki kuchoma mizinga kwa mfano Meatu eneo la Mwasengela kwa kuhofia kunyang'anywa maeneo yao.
Akijibu hoja hizo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila alisema kuwa ni vyema wafugaji kujiunga kwenye vikundi vya uzalishaji wa asali ili waweze kukopesheka.Ufugaji wa nyuki ni muhimu sana katika uchumi wa Taifa Letu.Vikundi 91 vilivyopo ni vichache sana hivyo basi, vikundi viongezwe ili watu wengi zaidi waweze kufikiwa.
Hivyo ninaelekeza uandaliwe, mkakati utakaoonesha ni vikundi vingapi vilivyopo na vitakavyoongezeka na hitaji la nyongeza ya mizinga au vifaa vingine muhimu ili kuwawezesha wanachama katika vikundi hivyo kutengeneza kipato cha Tshs.270,000/= kwa mwezi kwa kila mwanachama.Maafisa Nyuki wa Wilaya kwa kushirikiana na Afisa Nyuki Mkoa waandae mkakati wa angalau watu 10,000 waweze kutengeneza kipato cha Tshs.270,000/= kwa mwezi. Mkakati huo uandaliwe kabla au ifikapo tarehe 18/6/2021.
Changamoto ya upatikanaji wa mizinga itafutiwe namna,Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wengine wahusishwe katika upatikanaji wa mizinga hata kwa mkopo, vilevile kwa vifaa vyote vinavyohusiana na ufugaji na uvunaji wa mazao ya nyuki.WMA Makao waandae mkakati kwa ajili ya ufugaji wa nyuki kwa utekelezaji.
0 comments:
Post a Comment