Monday, June 14, 2021

WAVUVI, SIRI YA MAFANIKIO NI KUFANYA KAZI KWA VIKUNDI

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila wakati wa Ziara yake Wilayani Busega, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na Wavuvi wa Nyashimo.

Akifungua  Kikao hicho  Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe.Tano Mwera aliwafahamisha wakazi wa Nyashimo kuwa ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa Mpya wa Simiyu, imelenga kusikiliza kero zao na hatimae kupata ufumbuzi wa kero hizo.

Mhe.Tano aliwataka wawakilishi wa wavuvi hao kuwasilisha kero wanazokabiliana nazo katika shughuli za uvuvi, nao walikuwa na haya ya kusema;

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamikoma- Bw.Kurwa Bula; Changamoto, kubwa ni upumzikaji wa siku 10 hii ni changamoto kwani sisi tukipumzisha ziwa watu kutoka maeneo mengine wanakuja kuvua kwetu kwani wao huwa hawapumzishi Ziwa, ni bora,basi hiyo sheria iwekwe kwa mikoa yote mitatu.Kama kufungwa kufungwe Wilaya zote za mikoa jirani.

Akizungumza Diwani wa Kata ya Kabita- Silas Soshola, alisema changamoto kubwa tunazokabilina nazo ni pamoja na Sheria za uvuvi, nyingi ya sheria hizo ni za zamani na si rafiki, sasa hivi tunalipa Tsh. 400,000/- na bado kuna kodi nyingi Sana,Wavuvi wetu tuna Walipia leseni, tunaomba hiyo leseni ifutwe kwani mbona wakulima hawalipi leseni hizo,tunahitaji Masoko, tunaomba tupate masoko angalau mawili. Tuna Shule moja tu ya Sekondari, ambayo ina Wanafunzi 1250 na waalimu 2 wa somo la Biology, Waalimu 2 somo la Kiswahili ,waalimu 2-basic math, hatuna mwalimu wa fizikia. Wengi wa Waalimu wanaokuja hawakai. Wakazi wa Nyashimo walioamua kujenga Shule ya SekondariVenance Mabesho, ambapo tupo katika hatua za mwisho,tunaomba tupate angalau Mifuko 200 ya sementi kwani itasaidia sana katika ujenzi wa Uzio ili watoto wetu wasiliwe na wanyama. Tunaomba tuwekewe alama ya Pundamilia kwani Barabara yetu inakaosa alama hiyo na kwa kipindi cha kwa miaka watu wengi wamepoteza maisha.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji-Paulo Makongoro, alisema moja ya changamoto kubwa inayowakabili wakazi wa Nyashimo ni Changamoto ya viboko ambao wana angamiza watu. Mkazi mwingine wa Nyashimo Bw. Marko Shonokwa alisema ''Tunahitaji kituo cha Polisi, Kwani na kituo cha Polisi kilichojengwa na wananchi kukamilika bado wananchi wanaenda Nyamikoma''. 

Kero nyingine  zilizoelezwa na wakazi hao ni  pamoja na  watu kuchukua mamlaka  mkononi na kumtoa madarakani kiongozi aliyeschaguliwa na wananchi. Leseni  ilitajwa kuwa ni changamoto  kwani wakienda kwingine wanakamwatwa kwanini wao wakija huku hawakamatwi.Vilevile ilielezwa kwamba  shamba la Kijiji  limechukuliwa na kumilikiwa na watu binafsi.

Akijibu hoja hizo Mhe. Mkuu wa Mkoa alisema  Eneo la Nyashimo wilaya ya Busega lina ukanda wenye ukubwa wa kilometa za mraba 200 ambazo zinafaa kutumika kwa shughuli ya uvuvi. Uvuvi wa kutumia vizimba ndio wenye tija zaidi mnavyo Vizimba 12, na nimesikia kuwa mnavuna tani 54.

Eneo la kilometa za mraba 200 linaweza  kutumika kutengeneza Vizimba zaidi ya 55,000 na hivyo kupata Samaki kiasi cha tani 250,000, hatimae kuwa vinara katika eneo la uvuvi nchini. Njia nyepesi ya kupata msaada ni kukaa katika vikundi na hivyo kuirahisishia Serikali kutoa msaada mkiwa katika vikundi.

Kuhusu suala la kodi na ushuru, Mkurugenzi na watu wako andaeni taarifa kamili ya aina mbalimbali za ushuru/tozo. Pongezi kwa ujenzi wa Shule, mahitaji yenu ni shule nne namnayo moja, hatua madhubuti zitachukuliwa ili kuona ni kwa jinsi gani tutatatua changamoto hiyo.

MWISHO












0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!