Sunday, October 22, 2017

MABARAZA YA MADIWANI SIMIYU YARIDHIA HALMASHAURI ZIKOPE BILIONI 17.1 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Mabaraza ya Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Meatu Mkoani Simiyu yameridhia Halmashauri hizo kukopa shilingi bilioni 17.1 kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), kwa ajili ya kutekeleza Miradi mikubwa miwili  ya Maendeleo.

Maridhiano hayo yamefikiwa katika Vikao vya dharura vya mabaraza ya madiwani vilivyofanyika kwa nyakati tofauti, ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Busega imepanga kukopa shilingi bilioni 10.7 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili (eneo la ekari 2050)  na Meatu shilingi bilioni 6.4 kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha maziwa(MEATU MILK).

 Akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya Mpango wa Kilimo cha Umwagiliaji Wilayani Busega, Afisa Mipango wa Wilaya hiyo Josephat Joseph, amesema hadi sasa kazi za upimaji wa mashamba na njia ya kupita bomba la maji, kupima udongo, kusanifu mfereji mkuu kwenye chanzo, sehemu ya kuchukulia maji, nyumba za pampu, mifereji ya kuingiza na kutolea maji,kuandaa michoro na gharama za mradi zimeshakamilika.

Aidha, amesema katika utekelezaji wa mradi huu Halmashauri ndiyo msimamizi mkuu wa mradi na itajenga miundombinu yote ya umwagiliaji, hivyo itaingia makubaliano na wakulima wa Mwamanyili kupitia umoja wao watakaounda katika kutekeleza shughuli za mradi.

Nao wakulima wa Bonde la Mwamanyili wamesema wameupokea mradi huo kwa mikono miwili na kwa sasa wamesitisha shughuli zote za Kilimo katika bonde hilo, ili kupisha shughuli nyingine za maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya mradi huo.

“ Tunawashukuru viongozi wetu kwa kutusaidia kupata mkopo wa kutekeleza mradi huu naupokea kwa mikono miwili tena natamani uanze haraka, sasa hivi hatutalima maeneo yetu tunapisha wataalam waendelee na shughuli za maandalizi ya mradi ili wakikamilisha tu tuanze ” alisema Joseph Mayala.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema kutekelezwa kwa mradi huo, kutaiandikia historia wilaya ya BUSEGA  kwa kuwainua wananchi kiuchumi na kuondokana na aibu ya kuomba chakula cha msaada Serikalini, ambapo amesisitiza kuwa utakuwa mradi wa pekee ambao mnyororo wake wa thamani utaonekana kupitia mazao yatakayolimwa hususani mpunga.

Kwa upande wa Mradi wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza amesema kuelekea upanuzi wa kiwanda hicho, Halmashauri imekusudia kuongeza idadi ya wafugaji wanaopeleka maziwa kiwandani kutoka 45 wa sasa na kufikia wafugaji 400 wakubwa ambao wanafuga ng’ombe wa kisasa.

Mikakati mingine ni kununua mtambo mpya wa kuchakata maziwa wenye uwezo wa kuchakata lita elfu 15,000 kwa siku, kununua Mitamba 1000 na kuandaa shamba la malisho lenye miundombinu muhimu pamoja na kuongeza soko la MEATU MILK kwa kuingia mikataba na mawakala na kuweka maduka katika baadhi ya miji mikubwa.

Wafugaji wa Wilaya ya Meatu wamesema wameupokea mradi wa upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo kwa furaha, kwani utawasaidia kuongeza upatikanaji wa soko la uhakika la maziwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe.Pius Machungwa ametoa wito kwa wafugaji kukubali kubadilika na kuanza kufuga kisasa kulingana na jinsi wanavyoshauriwa na wataalam ili kuongeza tija.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imejipanga kutafuta  majawabu ya changamoto za wafugaji kwa kuwasaidia kufuga kisasa, ikiwa ni pamoja na kuwashauri kupima maeneo yao na kuyawekea miundombinu muhimu kama mabwawa, visima, majosho na mashamba ya malisho.

 “Kiwanda mnachokihitaji hapa kitatumia lita 15,000 kwa siku, mnapaswa kuweka mikakati mizuri ya ng’ombe wenu ili muwe na uhakika wa maziwa, nayazungumza haya ili kila mmoja aone umuhimu wa kiwanda; tuwasaidie wafugaji wafuge kisasa na kwa tija” alisema Mtaka.

Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Meatu zinatarajia kupata Mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ambayo imekubali kutoa mikopo hiyo ili kuunga mkono juhudi za Viongozi na wananchi wa mkoa wa Simiyu katika kuleta maendeleo. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (katikati) akizungumza na Madiwani na baadhi ya wafugaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu(hawapo pichani)   katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kujadili maombi ya mkopo kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe.Pius Machungwa akifungua kikao dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kujadili maombi ya mkopo kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe.Vumi Magoti(wa pili kulia)akizungumza na Madiwani na baadhi ya wakulima wa Busega(hawapo pichani) katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Nyashimo kwa lengo la kujadili maombi ya mkopo kwa ajili kutekeleza Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili Wilayani humo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndg.Fabian Manoza akizungumza na Madiwani na baadhi ya wafugaji wa Halmashauri hiyo (hawapo pichani)  katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kujadili maombi ya mkopo kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt.Joseph Chilongani akizungumza na Madiwani na baadhi ya wafugaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu (hawapo pichani)  katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kujadili suala la maombi ya mkopo kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (katikati) akizungumza na Madiwani na baadhi ya wakulima Bonde la Mwamanyili wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega (hawapo pichani) katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika Nyashimo kwa lengo la kujadili suala la maombi ya mkopo kwa ajili kutekeleza Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili Wilayani humo.
Afisa Mipango kutoa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndg.Josephat Joseph akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya Mpango wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili kwa viongozi, madiwani na baadhi ya wakulima (hawapo pichani) katika kikao cha dharura cha baraza la madiwani kilichofanyika kwa lengo la kujadili maombi ya mkopo kwa ajili ya kutekeleza mradi huo wilayani Busega.
Madiwani  na baadhi ya Wafugaji  wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakifuatilia mjadala kuhusu suala la maombi ya Mkopo kwa ajili ya Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Wilayani Meatu katika kikao cha dharura cha Baraza kilichofanyika Mjini Mwanhuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Meatu (baadhi hawapo pichani) alipotembelea eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuanzisha shamba la malisho ya mifugo wanaotarajiwa kununuliwa na Halmashauri hiyo kwa ajili ya kuwezesha  upatikanaji wa maziwa katika kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Diwani wa Kata ya Mwamishali katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mhe.Christopher Ndamo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika kwa lengo la kujadili suala la maombi ya mkopo kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Diwani wa Kata ya Mwamanyili, Mhe.Charles Luyenze akichangia hoja katika kikao cha cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwa lengo la kujadili suala la maombi ya mkopo kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili wilayani Busega.
Mmoja wa Wafugaji kutoka Wilaya ya Meatu, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika kwa lengo la kujadili suala la maombi ya mkopo kwa ajili upanuzi wa kiwanda cha maziwa wilayani humo.
Baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia mjadala kuhusu suala la maombi ya Mkopo kwa ajili ya Utekelezaji wa Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili wilayani humo, katika cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni katika makao makuu ya wilaya hiyo Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Busega  (meza kuu)  na watendaji mbalimbali wa Wilaya hiyo baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwa lengo la kujadili suala la maombi ya mkopo kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Busega  (meza kuu)  na madiwani wa Halmashauri hiyo baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwa lengo la kujadili suala la maombi ya mkopo kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Busega  (meza kuu)  na baadhi ya wakulima baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwa lengo la kujadili suala la maombi ya mkopo kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Bonde la Mwamanyili wilayani humo.

Saturday, October 14, 2017

TIZEBA:GINNER ATAKAYEGOMA KUPELEKA PAMBA MBEGU KWENYE KIWANDA CHA QUTON HATANUNUA PAMBA MWAKANI

Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt. Charles Tizeba amewataka wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba(ginners) kupeleka pamba mbegu kwenye kiwanda cha kuchakata(kutoa manyoya) mbegu za pamba cha Quton na akasema watakaogoma kupeleka hawatanunua pamba msimu ujao.

Waziri Tizeba ameyasema hayo jana alipotembelea kiwanda hicho katika Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kwa lengo la kujionea hali ya uzalishaji wa mbegu ya pamba inavyoendelea.

Amesema suala la wenye viwanda vya kuchambua pamba(ginners) kupeleka pamba mbegu katika kiwanda cha kuchakata mbegu za pamba(kuondoa manyoya) siyo la hiari na walishapewa maelekezo, hivyo wanapaswa kupeleka pamba mbegu katika kiwanda cha Quton ili zitolewe manyoya na baadaye zipelekwe kwa wananchi.

“ Nimeambiwa watu wa Quton wanashindwa kufanya kazi kwa shift tatu kwa siku kwa sababu walio na mbegu kwenye viwanda vyao vya kuchambua pamba hawataki kuleta pamba hapa, wakati wanayo maelekezo na hii siyo hiari mbegu ikishatengwa na Bodi ya Pamba si yao” alisema Tizeba.

“Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nakuagiza wapelekee ujumbe huu kwamba ginner atakayegoma kuleta pamba mbegu hapa Quton hanunui pamba mwaka kesho, wanapaswa walete mbegu zitolewe manyoya ziende kwa wananchi ili wapate mbegu bora, katika hili sitabembelezana na mtu” alisisitiza Tizeba.

Aidha, Mhe.Waziri amesema mahitaji ya mbegu ya pamba iliyotolewa manyoya kwa nchi nzima ni takribani tani 8000, hivyo ili kufikia kiwango hicho katika siku zilizobaki kuelekea msimu wa kilimo cha pamba, kiwanda cha Quton kinapaswa kufanya kazi saa 24 kwa kuwa uzalishaji wa sasa wa tani 60 hadi 65 kwa saa 16 kwa siku hautaweza kufikia lengo hilo.

Wakati huo huo Waziri Tizeba ametoa wito kwa wananchi Mkoani Simiyu kutopanda pamba sasa kwa kuhofia mvua kukatika mapema, badala yake wasubiri taarifa rasmi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa juu ya hali ya mvua katika ukanda huo itakayotolewa muda mfupi ujao,ambayo baadaye itatumika kuwashauri wakati muafaka wa kupanda, japo alieleza kuwa taarifa ya jumla ya utabiri wa hali ya hewa inaonesha mvua itanyesha juu ya wastani.

Pia Mhe.Waziri amewahakikishia wananchi kuwa bei ya mbolea imeshuka, hivyo akawataka wataalam wa Kilimo kuwaelimisha wananchi juu ya bei elekezi ya mbolea kwa kila wilaya, ili wasiuziwe kwa bei kubwa na akasisitiza kuwa bei ya mbolea na mbegu mwaka 2018 itapungua zaidi kwa kuwa Serikali imefuta takribani kodi 80 katika kilimo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga amesema Mkoa wa Simiyu unazalisha pamba kwa wingi, ambapo katika msimu wa mwaka 2016/2017 umezalisha takribani asilimia  65 ya pamba ya nchi nzima, hivyo akaomba wananchi wa mkoa huo wasaidiwe kupewa mikopo ya zana bora za kilimo na pembejeo nyingine kupitia mfuko wa pembejeo ili kuongeza uzalishaji zaidi.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Quton Tanzania Limited Ndg. Pradyumansinh Chauhan amemuomba Waziri wa Kilimo kuhamasisha wananchi kutumia mbegu za pamba zilizotolewa manyoya ili kuongeza uzalishaji kwa kuwa hazishambuliwi kwa urahisi na magonjwa na zinapunguza kiasi cha mbegu kinachotumika shambani ambapo kilogramu sita tu hutumika kwa hekali wakati zenye manyoya hutumika hadi kilogramu 15.


Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba (wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo kutoka wa Meneja Uzalishaji wa Mbegu,Pheneas Chikaura(kulia) katika Kiwanda cha Kuzalisha mbegu za pamba cha Quton wakati wa ziara yake kiwandani hapo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe Festo Kiswaga(kulia) akiwasilisha taarifa ya Wilaya yake kwa Waziri wa Kilimo, Dkt.Charles Tizeba (wa tatu kushoto) wakati alipofanya ziara katika Wilaya hiyo Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Charles Tizeba akikaribishwa na Mkurugenzi wa Quton Tanzania Limited Ndg.Pradyumansinh Chauhan, alipotembea Kiwanda cha kuzalisha Mbegu za Pamba cha Quton kilichopo kata ya kasoli Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba(kushoto) akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Donatus Weginah mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara ya siku moja Mkoani humo.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba(kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Mhe.Juliana Mahongo mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara ya siku moja Mkoani Simiyu.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Donatus Weginah akitoa taarifa ya Mkoa kwa Waziri wa Kilimo, Dkt.Charles Tizeba (kulia) wakati alipofanya ziara katika Wilaya ya Bariadi Mkoani humo.
Baadhi ya Viongozi na Wataalam wa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Dkt.Charles Tizeba(hayupo pichani) wakati alipozungumza nao kabla ya kutembelea Kiwanda cha Kuchakata mbegu za pamba(zilizotolewa manyoya) cha Quton katika Kata ya Kasoli Mkoani Simiyu kujionea uzalishaji wa mbegu za pamba.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance Ginnery, Ndg. Boazi Ogola(wa pili kushoto) akimuongoza Waziri wa Kilimo, Dkt.Charles Tizeba (aliyeweka mkono kifuani) na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu kuelekea kuona kiwanda hicho wakati wa ziara ya Waziri huyo Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt.Charles Tizeba akionesha moja ya mashine iliyopo katika Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery na akataka maelezo juu ya mashine hiyo wakati ziara yake Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba(wa pili kulia) na baadhi ya viongozi na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu wakielekea katika kiwanda cha kuzalisha mbegu za pamba zilizotolewa manyoya cha Quton wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt. Charles Tizeba(kulia) akizungumza na baadhi ya Viongozi na Wataalam wa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Mkoa wa Simiyu (hawapo pichani) kabla ya kutembelea Kampuni ya Quton katika Kata ya Kasoli Mkoani Simiyu kujionea uzalishaji wa mbegu za pamba.
Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt. Charles Tizeba(kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji wa Mbegu,Pheneas Chikaura(kulia) juu ya mbegu zilizozalishwa katika Kiwanda cha Kuzalisha mbegu za pamba cha Qutoni wakati wa ziara yake kiwandani hapo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya Viongozi, wataalam wa Mkoa wa Simiyu, Wataalam wa Kampuni ya Quton na Alliance Ginnery wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt. Charles Tizeba(wa pili kushoto) mara baada ya kutembelea moja ya kitalu kilichopandwa mbegu za pamba zilizotolewa manyoya wakati wa ziara yake Mkoani humo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Quton Tanzania Limited, Ndg.Pradyumansinh Chauhan akitoa taarifa ya uzalishaji wa mbegu za pamba zilizotolewa manyoya katika kiwanda cha kampuni hiyo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Quton Tanzania Limited, Ndg.Pradyumansinh Chauhan akitoa taarifa ya uzalishaji wa mbegu za pamba zilizotolewa manyoya katika kiwanda cha kampuni hiyo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya Kasoli (hawapo pichani)wakati wa Ziara ya Waziri wa Kilimo, Mhe.Charles Tizeba, ambapo alitembelea kiwanda cha kuzalisha mbegu za pamba zilizoondolewa manyoya cha Quton Mkoani Simiyu ili kujionea uzalishaji wa mbegu hizo.

Sunday, October 8, 2017

RC MTAKA: SIMIYU SASA TUNAJADILI MAENDELEO YA WANANCHI SIYO MAUAJI YA VIKONGWE NA ALBINO

Mkoa wa Simiyu kwa sasa haujadili tena masuala ya mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi(albino) badala yake unajidili maendeleo ya wananchi wa mkoa huo.

Hayo yamesemwa  jana na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ufungaji wa Makambi ya Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA) yaliyoyofanyika katika Uwanja wa Kidinda mjini Bariadi.

“Miaka hii miwili tumejenga mkoa ambao hatujadili mauaji ya albino, mauaji ya vikongwe, watu kukatwa mapanga, tunajadili Wasukuma Wanyantuzu wanaoenda kwenye maendeleo, ndiyo maana leo mtaona kumejengwa magorofa na nyumba nyingine bora, siyo watu wanaoamini kuwa mtu akiua watu anakuwa tajiri” amesisitiza Mtaka.

Ameongeza kuwa waumini hao wanapaswa kuwa mabalozi katika kufanya mambo ya maendeleo  na wakati huo huo wapinge na kukemea mambo maovu katika jamii na kuwa mfano wa kuigwa kwa watu wengine.

Aidha, ametoa wito kwa waumini hao kuchangamkia fursa za miradi mbalimbali itakayotekelezwa mkoani humo ukiwemo mradi wa kilimo katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mwasubuya Wilayani Bariadi, ambapo panakusudiwa kulimwa mpunga kupitia kilimo cha kisasa chenye tija.

Wakati huo huo amewataka waumini hao kuyafanyia kazi na kuyatafsiri kwa vitendo mafundisho waliyopewa wakati wa makambi yakiwemo ya ujasiriamali, ili mwaka 2018 watu watakaoshiriki katika makambi kama hayo waone matokeo ya bidhaa zilizotengenezwa kutokana na ujuzi walioupata mwaka huu.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato na wananchi wote kwa ujumla kuwaombe viongozi wa Serikali hususani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, kwa kuwa anafanya kazi kubwa katika kudhibiti wizi na kutetea rasilimali za nchi hii ili ziwanufaishe Watanzania wote.

“Wapo watu wanauliza ni kwa nini Mhe.Rais aombewe, nawaomba tumuombee Mhe.Rais kwa sababu anafanya kazi kubwa kutetea rasilimali za Watanzania, anafanya maamuzi mazito ambayo yanawaumiza baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijinufaisha wao na kuwaumiza wenzao; yanagusa biashara za watu ambao wakati mwingine wangetamani Serikali hii ife hata kesho, ni lazima tumuombee Mhe.Rais” amesema Mtaka.  

Akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka,  Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato wa Southern Nyanza Conference inayojumuisha Mikoa ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Geita, Mch.Sadock Butoke  amesema, Makambi hayo yamekuwa ya mafanikio kwani pamoja na waumini hao kufundishwa Neno la Mungu, wamefundishwa masomo  ya Afya, Ujasiriamali na kaya na familia ambayo yatawaimarisha kimwili na kiroho.

Naye Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe.Leah Komanya amewashukuru viongozi wa dini kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuisaidia Serikali kwa kuwaelekeza waumini wao kufanya mambo mema na kuwa na hofu ya Mungu, hali inayopelekea wananchi wengi kutojihusisha na vitendo viovu.

Makambi ya Waumini wa Kanisa la Waadventisha Wasabato yaliyofungwa rasmi jana Jumamosi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka yamedumu kwa takribani wiki tatu na yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato(hawapo pichani) jana wakati wa kufunga Makambi yaliyofanyika katika Uwanja wa Kidinda Mjini Bariadi.
Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato wa Southern Nyanza Conference inayojumuisha Mikoa ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Geita, Mch.Sadock Butoke akizungumza na waumini wa Kanisa hilo (hawapo pichani) jana, wakati wa kufunga Makambi yaliyofanyika katika Uwanja wa Kidinda Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akiimba (mwenye koti)pamoja na waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la Waadventisa Wasabato Kurasini(Kurasini Choir) ya Jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga Makambi ya waumini wa Kanisa hilo yaliyofanyika katika Uwanja wa Kidinda Mjini Bariadi.
Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe.Leah Komanya akizungumza na Waumuni wa Kanisa la Waadventista Wasabato (hawapo pichani) jana wakati wa kufunga Makambi ya waumini hao yaliyofanyika katika Uwanja wa Kidinda Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akifurahia jambo wakati wa kufunga Makambi ya Waumuni wa Kanisa la Waadventista Wasabato(hawapo pichani) jana,  yaliyofanyika katika Uwanja wa Kidinda Mjini Bariadi; anayefuata, Mwenyekiti wa UWT(CCM) Mkoa wa Simiyu, Katibu Tawala Wilaya ya Bariadi, Albert Rutaihwa na Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe.Leah Komanya.
Baadhi ya Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipozungumza nao jana wakati wa kufunga makambi yao yaliyofanyika katika Uwanja wa Kidinda Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(mwenye koti na tai) akiwa katika picha ya pamoja na waimbaji wa Kwaya ya Kurasini SDA mara baada ya kufunga makambi ya Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato jana,  yaliyofanyika katika Uwanja wa Kidinda Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(mwenye  tai ya bluu bahari) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mkoa huo, waimbaji wa Kwaya ya Kurasini SDA(wenye sare) na baadhi ya Viongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Southern Nyanza Conference mara baada ya kufunga makambi ya Waumini wa Kanisa hilo jana yaliyofanyika katika Uwanja wa Kidinda Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(mwenye koti na tai) akiagana na waimbaji wa Kwaya ya Kurasini SDA mara baada ya kufunga makambi ya Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato yaliyofanyika katika Uwanja wa Kidinda Mjini Bariadi.
Vijana wa Pathfinder wakimvisha skafu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kwa ajili ya kufunga makambi ya Waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato jana yaliyofanyika katika Uwanja wa Kidinda Mjini Bariadi.

Wednesday, October 4, 2017

WAFUGAJI NYUKI WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO KUONGEZA THAMANI YA MAZAO YA NYUKI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani  amesema Wafugaji Nyuki wanayo fursa kubwa ya kujikita katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vya kuchakata, kufungasha na kuongeza thamani mazao ya nyuki na kutengeneza vipodozi kutokana na mazao ya nyuki.

Mhandisi Makani  ameyasema hayo jana wakati alipozungumza na wafugaji wa nyuki na wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, chini ya Kauli Mbiu “UFUGAJI NYUKI KIBIASHARA UNACHANGIA KATIKA UKUAJI WA VIWANDA”

Amesema Mazao ya Nyuki ni malighafi ya Viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya vyakula vinavyotumia asali, viwanda vya dawa na vipodozi na viwanda vya utengenezaji vinavyotumia nta katika kuzalisha maturubai, dawa za kung’arisha viatu na bidhaa nyingine, hivyo wafugaji  wanao wajibu wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki na ujuzi wa kuyaweka katika ubora na kuyaongezea thamani.

Aidha, ametoa wito kwa wafugaji wa nyuki kuungana katika vikundi vyenye usajili ili waweze kuzalisha asali kwa wingi na yenye kufanana, kwa kuwa ikiwa watazalisha kila mmoja kwa utaratibu wake, asali hiyo haiwezi kuchanganywa na itakuwa na ubora na sifa tofauti, lakini ikiwa wataungana na kuzalisha asali nyingi kwa pamoja wakaipima kwa viwango vya ubora unaotakiwa wataweza kupata soko.

Sanjali na hilo amesema Serikali itahakikisha inawaunganisha wafugaji nyuki na walaji wa ndani na nje na akabainisha kuwa kwa miaka zaidi ya 11 imekuwa na ushirikiano na soko la Ulaya ambapo sampuli za asali kutoka maeneo mbalimbali zimepelekwa Ulaya na taarifa za maabara zinathibitisha kuwa asali ya Tanzania ni salama kwa afya ya mlaji.

Aidha, amesema katika kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki Serikali pia inaendelea kutoa elimu kwa wafugaji wa nyuki  kuachana na matumizi ya mizinga ya asili ambayo ni duni na inachukua nafasi kubwa wakati uzalishaji wake ni mdogo na kuwahamasisha kuanza kutumia mizinga ya kisasa.

“ Nawaagiza Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki nchini na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kupitia jukwaa hili, kwamba mbuni njia rafiki ya kuweka msisitizo katika utoaji wa elimu, uhamasishaji na kupima mafanikio kila mwaka; taarifa ya utekelezaji wa maagizo haya itolewe mara kwa mara, taarifa ya kwanza baada ya agizo hili itolewe katika siku ya maadhimisho kama haya mwaka kesho 2018” aliagiza Naibu Waziri.

Katika hatua nyingine Mhe. Makani amepongeza juhudi zinazofanywa na Mradi wa LVEMP II katika kuboresha mazingira na kubainisha kuwa pamoja na kuhifadhi rasilimali za asili za Bonde la Ziwa Victoria ambayo husaidia kutunza vyanzo vya maji  na mazingira hayo yanafanywa kuwa mazingira bora kwa ufugaji nyuki, ambapo katika wilaya ya Itilima kuna vikundi 22 vyenye mizinga 2080 ya nyuki vinavyofadhiliwa na LVEMP.

Akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Chele Ndaki amesema idadi ya wafugaji na mizinga ya nyuki imekuwa ikiongezeka kila mwaka ambapo kwa sasa kuna jumla ya vikundi 91 vyenye jumla ya mizinga 5824 na akaahidi kuwa mkoa utaendelea kusimamia uboreshaji wa mazingira ya ufugaji nyuki na kusimamia vikundi vinavyoanzishwa katika Halmashauri., ili wafugaji wanufaike na kujiimarisha kiuchumi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Ndg.Herberth Haule amesema shughuli ya ufugaji wa nyuki  inasaidia katika uhifadhi wa mazingira na  kujenga uchumi kwa wananchi hususani vikundi vinavyojishughulisha na kazi hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Ezekiel Mwakalukwa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi Tano za Afrika zinazoruhusiwa kuuza asali yake katika soko la Ulaya na nchi ya China.

Nao wafugaji wa nyuki na wajasiriamali wa mazao ya nyuki wameiomba Serikali pamoja na wadau wengine kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza vifungashio kwa kuwa suala hilo ni changamoto kwao ambayo  inawalazimu kuagiza vifungashio nje ya nchi kwa kutumia gharama kubwa.


Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa kwa mwaka 2017 yameadhimishwa kwa mara kwanza Mkoani Simiyu yakiwa ni maadhimisho ya tano kufanyika hapa nchini, ambapo kwa mara ya kwanza  yalifanyika mwaka 2013 Mkoani Singida.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani (Mb)(kulia)akitundika Mzinga katika Banda la Nyuki la Kikundi cha Wafugaji Nyuki cha Malela wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani (Mb)(kulia)akitundika Mzinga katika Banda la Nyuki la Kikundi cha Wafugaji Nyuki cha Malela wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani (Mb)akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Itilima(hawapo pichani ) wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika  Mkoa Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb)(kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ofisini kwake kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya Siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki yaliyofanyika Mkoani humo katika kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi akizungumza na wananchi wa wilayani hiyo (hawapo pichani ) wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika  Mkoa Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb) akizindua Manzuki (Shamba la Miti lenye Mizinga ya Nyuki) ya Kikundi cha Wafugaji nyuki cha Malela Wilayani Itilima wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika  Mkoa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng.Ramo Makani(Mb) (kulia) kabla ya kuanza safari kuelekea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani (Mb)(wa pili kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu wakielekea eneo la ktundika Mizinga wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizingaya Nyuki  Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima katika  Mkoa Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng.Ramo Makani(Mb) akivishwa skafu na Vijana wa Skauti ya Wilaya ya Itilima ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima katika  Mkoa Simiyu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng.Ramo Makani(Mb) (mwenye skafu) akiangalia mazao ya Nyuki alipotembelea Banda la maonesho la Kikundi cha Wafugaji Nyuki cha Malela wilayani Itilima, wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika  Mkoa Simiyu.
Baadhi ya wanachama wa Kikundi cha Wafugaji Nyuki cha Malela wakimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng.Ramo Makani(Mb) moja ya tuzo waliyopata kutokana na uzalishaji wa asali bora, wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima katika  Mkoa Simiyu.
Kutoka kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Dkt. Titus Kamani, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng.Ramo Makani(Mb) na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi wakizungumza jambo,   wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima katika  Mkoa Simiyu.
Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe.Njalu Silanga akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima katika  Mkoa Simiyu.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Chele Ndaki(kushoto) akiwasilisha taarifa ya Mkoa ya ufugaji Nyuki wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima katika  Mkoa Simiyu.
Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akitoa taarifa ya ufugaji nyuki, wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima katika  Mkoa Simiyu.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb) (mwenye skafu) akizungumza na wajasiriamali wa mazao ya nyuki kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, alipotembelea banda lao wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana,  katika Kijiji cha Isengwa Wilayani Itilima katika  Mkoa Simiyu.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb) (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani humo.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb) (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo  Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb) (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo  Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Itilima, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima na Halmashauri jirani, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wanachama wa Kikundi cha Wafugaji Nyuki cha Malela Wilaya ya Itilima, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya wajasiriamali walioleta bidhaa zao za mazao ya nyuki, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!