Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini
Jenerali Venance Mabeyo ametoa wito kwa Viongozi wa Dini nchini kuendelea
kuhubiri amani ili kujenga jamii iliyo bora yenye kudumisha upendo na
mshikamano.
Jenerali Mabeyo ametoa wito huo wakati
wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha
Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega ambayo ilihudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa Kitaifa akiwepo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro,
Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese na viongozi wengine wa Chama na
Serikali, ambapo alisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo kwa Taifa lolote
duniani.
"Suala la amani na utulivu ni la
msingi sana katika nchi yetu, kwa vile kila mwananchi ana dini yake tunaamini
kuwa viongozi wa dini zote kwa kuwa wanasikilizwa sana na waumini
wakiweka msisitizo katika suala la amani, amani itatawala na kutakuwa na
utulivu"
“Utulivu huu tunauhitaji sana ili tupate
maendeleo, kama viongozi wetu wa kisiasa wanavyosisitiza kuwa tudumishe
amani na utulivu tupate maendeleo, bila utulivu watu wakiwa wanahaingaika
hakuna maendeleo kwa sababu hakuna shughuli mtu anaweza kufanya kama hana amani
na utulivu, hivyo hataweza pia kuleta maendeleo yake, familia, jamii na Taifa
kwa ujumla" alisema Jenerali Mabeyo
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini Inspekta Jenerali Simon Sirro amesema vitendo vingi vya uvunjifu wa
amani na uhalifu ikiwemo ukataji wa mapanga na mauaji ya vikongwe na
yanachangiwa na watu kukosa hofu ya Mungu; hivyo nyumba za ibada(makanisa na
misikiti) zinapojengwa kwa wingi zitakuwa msaada mkubwa sana kwa watu kuwa na
hofu ya Mungu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amesema jamii inayoamini uwepo wa Mungu haiwezi kuwa na vitendo
vya kisasi, kukatana mapanga na mauaji ya vikongwe huku akiwaasa Watanzania kukaa
kwa amani na upendo bila kufanya mambo yanayoweza kuhatarisha amani.
Akibariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu
Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega, Askofu wa Jimbo
Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu amewataka Watanzania kupendana na
kuacha roho ya ubinafsi na visasi.
Aidha, Askofu Sangu ametoa wito kwa
viongozi na waumini kufanya nyumba za ibada zibaki nyumba za sala kama yanenavyo
maandiko matakatifu na kamwe zisitumike kama majukwaa la wanasiasa.
" Palipo na msamaha pana umoja,
uelewano na usawa lakini palipo na kisasi hapana maendeleo; nyumba ya
ibada isitumike kama jukwaa la Wanasiasa alisisitiza Muhashamu Askofu Sangu.
MWISHO
Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi nchini Jeneral Venance Mabeyo akipokea mkono wa Heri ya Krismasi kutoka
kwa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, katika ibada
ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli
Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki
Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu akimshuhudia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
nchini Jenerali Venance Mabeyo wakati akitia saini kama shahidi katika Hati ya
kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli
Parokia ya Ilumya, katika ibada ya kubariki na kutabaruku kanisa hilo, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Kutoka kushoto Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard
Kibese, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP
Simon Sirro na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakiwa katika ibada
ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli
Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Wanakwaya
ya Mtakatifu Maxmillian kutoka Parokia ya Segerea jijini Dar es salaam wakiimba
katika katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango
cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika
Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki
Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na viongozi wengine
wakiwa na katika picha ya pamoja na watoto wenye ualbino wanaoishi katika kituo
cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum Lamadi, mara baada ya kumalizika kwa ibada
ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli
Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki
Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu( wa pili kushoto mbele) akiwaongoza
waumini katika sala ya kuombea Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli
Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu katika ibada ya kubariki na
kutabaruku kanisa hilo, iliyofanyika
Desemba 26, 2018.
Baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Simiyu na wa Kitaifa wakiimba wimbo wa mimina Neema wa Kwaya ya
Mwenyeheri Anuarite Makuburi jijini Dar es salaam, wakati wa ibada ya kubariki
na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya
wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akipokea sakramenti ya mwili na damu ya Yesu Kristo wakati
wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha
Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba
26, 2018.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini Inspekta wa Polisi Simon Sirro akipokea sakramenti ya mwili na
damu ya Yesu Kristo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu
Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu,
iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo akipokea sakramenti ya mwili na damu ya
Yesu Kristo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro
Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu,
iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Sehemu ya Kanisa la
Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya Busega, lililobarikiwa
na kutabarukiwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus
Sangu Desemba 26, 2018.
Baadhi ya viongozi wa
Serikali , vyombo vya ulinzi na usalama na waumini wakifuatilia ibada ya kubariki
na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya
wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Askofu wa
Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu( wa pili kushoto) na baadhi
ya viongozi wa Serikali , vyombo vya ulinzi na usalama na waumini, baada
ya ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha
Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba
26, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiteta jambo na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga,
Muhashamu Liberatus Sangu, baada ya ibada
ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli
Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki
Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
mapadri walioshiriki katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu
Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu,
iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki
Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu akitoa mahubiri katika ibada ya kubariki
na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya
wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki
Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu(kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa pili kulia) na baadhi ya wanakwaya ya
Mwenyeheri Anuarite Makuburi jijini Dar es salaam, baada
ya ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha
Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba
26, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kulia)akiteta jambo na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu
Liberatus Sangu(kushoto) na baadhi ya wanakwaya ya Mwenyeheri Anuarite Makuburi
jijini Dar es salaam, baada ya ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu
Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu,
iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu
Liberatus Sangu(kushoto) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenrali Venance
Mabeyo(kulia) baada ya ibada ya kubariki
na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya
wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
kutoka kushoto Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Benard Kibese, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta wa Polisi
Simon Sirro wakifurahia jambo na kulia na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini
Jenrali Venance Mabeyo akikabidhiwa mshumaa, katika ibada ya kubariki na
kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya
wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akipokea mkono wa Heri ya Krismasi kutoka kwa Askofu wa
Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, katika ibada ya kubariki
na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya
wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mwimbaji wa Nyimbo za
Injili, Christina Shusho akiimba pamoja na wanakwaya ya Mtakatifu Maxmillian Parokia
ya Segerea jijini Dar es salaam, baada ya ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa
la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega
mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Paroko wa Parokia ya
Ilumya, Michael Kumalija akitia saini Hati ya kubariki na kutabaruku Kanisa la
Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya, katika ibada ya
kubariki na kutabaruku kanisa hilo,