Thursday, December 27, 2018

JENERALI MABEYO ATOA WITO KWA VIONGOZI WA DINI KUHUBIRI AMANI

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo ametoa wito kwa Viongozi wa Dini nchini kuendelea kuhubiri amani ili kujenga jamii iliyo bora yenye kudumisha upendo na mshikamano.

Jenerali Mabeyo ametoa wito huo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwepo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese na viongozi wengine wa Chama na Serikali, ambapo alisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo kwa Taifa lolote duniani.

"Suala la amani na utulivu ni la msingi sana katika nchi yetu, kwa vile kila mwananchi ana dini yake tunaamini kuwa viongozi wa dini zote kwa kuwa wanasikilizwa sana  na waumini  wakiweka msisitizo katika suala la amani, amani itatawala na kutakuwa na utulivu"

“Utulivu huu tunauhitaji sana ili tupate maendeleo,  kama  viongozi wetu wa kisiasa wanavyosisitiza kuwa tudumishe amani na utulivu  tupate maendeleo, bila utulivu watu wakiwa wanahaingaika hakuna maendeleo kwa sababu hakuna shughuli mtu anaweza kufanya kama hana amani na utulivu, hivyo hataweza pia kuleta maendeleo yake, familia, jamii na Taifa kwa ujumla" alisema Jenerali Mabeyo

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Simon Sirro amesema vitendo vingi vya uvunjifu wa amani na uhalifu ikiwemo ukataji wa mapanga na mauaji ya vikongwe na yanachangiwa na watu kukosa hofu ya Mungu; hivyo nyumba za ibada(makanisa na misikiti) zinapojengwa kwa wingi zitakuwa msaada mkubwa sana kwa watu kuwa na hofu ya Mungu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema jamii inayoamini uwepo wa Mungu haiwezi kuwa na vitendo vya kisasi, kukatana mapanga na mauaji ya vikongwe huku akiwaasa Watanzania kukaa kwa amani na upendo bila kufanya mambo yanayoweza kuhatarisha amani.

Akibariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega, Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu amewataka Watanzania kupendana na kuacha roho ya ubinafsi na visasi.

Aidha, Askofu Sangu ametoa wito kwa viongozi na waumini kufanya nyumba za ibada zibaki nyumba za sala kama yanenavyo maandiko matakatifu na kamwe zisitumike kama majukwaa la wanasiasa.

" Palipo na msamaha pana umoja, uelewano na usawa lakini palipo na  kisasi hapana maendeleo; nyumba ya ibada isitumike kama jukwaa la Wanasiasa alisisitiza Muhashamu Askofu Sangu.

MWISHO

 Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu(kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo(kulia) wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.



Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jeneral Venance Mabeyo akipokea mkono wa Heri ya Krismasi kutoka kwa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.

Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu akimshuhudia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo wakati akitia saini kama shahidi katika Hati ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya, katika ibada ya kubariki na kutabaruku  kanisa hilo, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakiwa katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Wanakwaya ya Mtakatifu Maxmillian kutoka Parokia ya Segerea jijini Dar es salaam wakiimba katika katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na viongozi wengine wakiwa na katika picha ya pamoja na watoto wenye ualbino wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum Lamadi, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu( wa pili kushoto mbele) akiwaongoza waumini katika sala ya kuombea Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu katika ibada ya kubariki na kutabaruku  kanisa hilo, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wa Kitaifa wakiimba wimbo wa mimina Neema wa Kwaya ya Mwenyeheri Anuarite Makuburi jijini Dar es salaam, wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akipokea sakramenti ya mwili na damu ya Yesu Kristo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta wa  Polisi Simon Sirro akipokea sakramenti ya mwili na damu ya Yesu Kristo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo akipokea sakramenti ya mwili na damu ya Yesu Kristo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.

Sehemu ya Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya Busega, lililobarikiwa na kutabarukiwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu Desemba 26, 2018.
Baadhi ya viongozi wa Serikali , vyombo vya ulinzi na usalama na waumini wakifuatilia ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu( wa pili kushoto) na baadhi ya viongozi wa Serikali , vyombo vya ulinzi na usalama na waumini,  baada  ya ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiteta jambo na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, baada  ya ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mapadri walioshiriki katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu akitoa mahubiri katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu(kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa pili kulia) na baadhi ya wanakwaya ya Mwenyeheri Anuarite Makuburi jijini Dar es salaam,  baada  ya ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia)akiteta jambo na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu(kushoto) na baadhi ya wanakwaya ya Mwenyeheri Anuarite Makuburi jijini Dar es salaam,  baada  ya ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu(kushoto) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenrali Venance Mabeyo(kulia) baada  ya ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
kutoka kushoto Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Benard Kibese, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta wa  Polisi Simon Sirro wakifurahia jambo na kulia na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenrali Venance Mabeyo akikabidhiwa mshumaa, katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akipokea mkono wa Heri ya Krismasi kutoka kwa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, katika ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Christina Shusho akiimba pamoja na wanakwaya ya Mtakatifu Maxmillian Parokia ya Segerea jijini Dar es salaam, baada ya ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.
Paroko wa Parokia ya Ilumya, Michael Kumalija akitia saini Hati ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya, katika ibada ya kubariki na kutabaruku  kanisa hilo, iliyofanyika Desemba 26, 2018.

Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na viongozi wengine wakiwa na katika picha ya pamoja na watoto wenye ualbino wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum Lamadi, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayan Busega mkoani Simiyu, iliyofanyika Desemba 26, 2018.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!