Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametekeleza agizo la Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kutoa vitambulisho
kwa wajasiriamali wadogo, ambapo amewakabidhi Wakuu wa Wilaya na Maafisa
Biashara wa Halmashauri mkoani hapa jumla ya vitambulisho 25,000, vitakavyotolewa kwa wajasiriamali
wadogo wenye mauzo pungufu ya milioni nne kwa mwaka.
Akikabidhi vitambulisho hivyo Mtaka amesema vitawasaidia
wajasiriamali wadogo kutambuliwa,kuwajengea ujasiri na uthubutu na kuwafanya kunufaika na fursa mbalimbali huku akibainisha kuwa
vitachangia pia kuwaibua wajasiriamali wapya mkoani Simiyu.
Ameongeza kuwa Simiyu imejipanga kuwafikia
wajasiriamali wote wadogo kama ilivyokusudiwa na Mhe. Rais, huku akiwaonya na
kuwatahadharisha wafanyabiashara wakubwa wanaotambuliwa na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kutojaribu kujipatia vitambulisho vya wajasiriamali wadogo kwa
njia ya udanganyifu.
“Niwatahadharishe wafanyabiashara wasije wakatumia
nafasi ya vitambulisho hivi vya wajasirimali wadogo, kufanya udanganyifu wowote
wa wao kuvitumia vitambulisho hivyo kujitambulisha kama wafanyabiashara wadogo;
huu udanganyifu hatutaupa nafasi na sisi kama Serikali tumejiandaa kuainisha
kila mtu anachofanya, mahali anapokaa, historia yake ya biashara”
“Ofisi za Wakurugenzi zitatoa magari yatakayowawezesha
maafisa Biashara kwenda vijijini kuwafikia wajasiamali wadogo,tunaamini
walengwa wa vitambulisho hivi ni wale ambao nauli ya kule aliko na Makao Makuu
ya Wilaya inaweza kuwa ndiyo fedha inayohitajika achangie kupata kitambulisho
hicho,kwa hiyo kuna kadi zitabaki wilayani lakini nyingine zitapelekwa mahali
walipo walengwa” alifafanua Mtaka.
Baadhi ya wakuu wa wilaya wakizungumza mara baada ya kupokea vitambulisho
hivyo wamesema watahakikisha vinawafikia walengwa waliokusudiwa na hakutakuwepo
na udanganyifu wowote katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo.
“Niwahakikishie wajasiriamali wadogo wote kuwa watapata vitambulisho kama
Mhe Rais alivyoelekeza na nitoe wito kwao kuja kuchukua vitambulisho hivi ili
asiwepo mtu yeyote wa kuwabugudhi na wafanye kazi zao kwa uhuru” Mkuu wa Wilaya
ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga.
“ Niwatoe hofu wajasiriamali wote wadogo kuwa kila aliye na sifa ya kupata
kitambulisho hiki atapata na kwa wale wanaodhani watatumia vitambulisho hivi
kukwepa kodi nichukue nafasi hii kutoa onyo kuwa hatutavumilia udanganyifu wa
aina yoyote” Mkuu wa Wilaya ya Busega,Mhe. Tano Mwera.
Baadhi ya wajasiriamali Wadogo Mkoa Simiyu wameshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutoa vitambulisho hivyo ambavyo vitawaondolea adha mbalimbali
walizokuwa wakizipata ikiwepo ya kuogopa kufanya biashar zao kutokana na kutotambuliwa
rasmi.
“ Tanamshukuru sana Rais ametupa ujasiri wa kufanya biashara zetu kwa uhuru
maana kuna watu walikuwa wanaogopa kufanya biashara kwa sababu ya kuogopa kodi,
kupitia vitambulisho hivi tutafanya biashara kwa uaminifu, uhuru na ujasiri na
katika wilaya yetu ya Bariadi, Tanzania
ya Viwanda hasa vile vidogo itawezekana” alisema Bahati Kaitila mjasiriamali mdogo kutoka Bariadi.
“ Nimelipokea vizuri suala la kupewa vitambulisho kwa sababu vitatusaidia sisi wajasiriamali
wadogo kupata ujasiri zaidi wa kufanya kazi zetu, tunaweza kuanza na kitu
kidogo lakini baadaye tukafanya makubwa” alisema Grace Mukali
mjasiriamali mdogo kutoka wilaya ya Bariadi.
MWISHO.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano
Mwera boksi lenye vitambulisho vya
wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa
Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo
yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka, ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia
wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga boksi lenye vitambulisho vya
wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa
Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo
yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia
wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt.
Joseph Chilongani boksi lenye
vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa
Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo
ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka ili vitambulisho hivyo viweze
kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment