Thursday, November 29, 2018

RC MTAKA ATOA WITO KWA WALIMU KUEPUKA VITENDO VINAVYOHARIBU HAIBA NA HESHIMA YA UALIMU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa walimu kuendelea kuwa walezi wa wanafunzi wao na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoharibu haiba na heshima ya ualimu, ili waweze kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili kwao na kwa wanafunzi wanaowafundisha.


Mtaka ameyasema hayo Novemba 28, 2018 katika mahafali ya 26 ya kidato cha nne shule ya sekondari Mwembeni (ambayo alisoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 1997-mwaka 2000),  iliyopo Mjini Musoma ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Amesema katika baadhi ya maeneo baadhi ya walimu wamekuwa wakifanya mambo ambayo yanaharibu heshima na haiba ya ualimu jambo ambalo linapelekea wazazi kutowaamini walimu na kuogopa kuwapeleka watoto wao katika shule hizo.

" Naishukuru sana bodi ya shule na walimu wa Mwembeni kwa kuendelea kuhakikisha walimu wetu wanalinda heshima na haiba ya ualimu na wazazi wameendelea kuiamini shule kwa kuleta watoto wao, kwa sababu hakuna matukio yanayohatarisha uwepo wa watoto wao shuleni na masuala la elimu, maadili na nidhamu kwenye shule hii kama Taasisi yameendelea kuimarishwa" alisema.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wazazi, walezi na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wanafunzi waliosoma katika shule ya Mwembeni miaka ya nyuma kuchangia katika ujenzi wa shule(vyumba vya madarasa) ili kupanua wigo kwa wanafunzi kuanza kusoma masomo ya sayansi, ikizingatiwa kuwa katika dunia ya sasa ni ya ushindani wa sayansi na teknolojia.

"Dunia tunayoiendea sasa ni ya ushindani wa sayansi na teknolojia na kama shule imejielekeza kwenye masomo ya sayansi ni jambo la kuungwa mkono; niwaalike wenzangu wote tuliosoma katika shule ya sekondari Mwembeni kuona haja ya kurejesha kwenye shule katika kile tulichopata katika shughuli zetu za kimaisha, tukirejeshe tujenge shule yetu ili iendelee kuwa kwenye ushindani mkubwa na kuwa miongoni mwa shule bora mkoani Mara" alisisitiza Mtaka.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwembeni, Bro.Erasmus Marando amewaomba wadau wasaidie kujenga vyumba zaidi vya madarasa, shule hiyo ianze kutoa masomo ya mchepuo wa sayansi, ili kuwaanda wataalam watakaoenda sambamba na sera ya Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda.

Naye Mwalimu Anselm Mnibhi ambaye amemfundisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Shule ya Sekondari ya Mwembeni mwaka 1997 hadi mwaka 2000, amemshukuru kwa kukumbuka shule aliyosoma na kuonesha nia ya kusaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na kubainisha kuwa hakuna mwanafunzi yeyote aliyesoma hapo zamani aliyeonesha nia na dhamira hiyo na akawaomba wote waliosoma shuleni hapo kujitoa kujenga shule yao.

Kwa upande wake mhitimu wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni, Sharon Buganda ametoa wito kwa wanafunzi waliobaki kuondokana na dhana ya kuogopa kusoma masomo ya sayansi wakiamini kuwa ni magumu, badala yake wasome masomo hayo ili waweze kuwa wataalam wajao katika maeneo mbalimbali ikiwemo  viwanda ambavyo ni sera ya Serikali ya Awamu ya tano.

Katika mahafali hayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka aliahidi kuchangia shilingi milioni tano na kuhamasisha wenzake aliosoma nao shuleni hapo Mwembeni kuchangia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa vitakavyotumika na wanafunzi wa mchepuo wa sayansi, kutoa zawadi ya shilingi milioni moja (kwa mwanafunzi wa kiume) na shilingi milioni moja na laki tano(kwa mwanafunzi wa kike) atakayekuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa  katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2018.
MWISHO


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni Mjini Musoma, ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hiyo iliyofanyika shuleni hapoNovemba 28, 2018.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na Mwl.Anselm Mnibhi wa Shule ya Sekondari Mwembeni ambaye pia alimfundisha yeye akiwa mwanafunzi wa shule hiyo mwaka 1997-2000, wakati wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo,  iliyofanyika shuleni hapoNovemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye kipaza sauti) akiwa na wenzake aliosoma nao katika shule ya sekondari Mwembeni mwaka 1997- mwaka 2000 na baadhi ya walimu waliwafundisha, katika  mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa  shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwembeni mjini Musoma wakitoa burudani ya ngoma ya asili ya kabila la Wakurya, katika  mahafali ya 26 ya ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  alikuwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wenzake aliosoma nao katika shule ya sekondari Mwembeni mwaka 1997- mwaka 2000 na baadhi ya walimu waliowafundisha, katika  mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.

Baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwembeni  wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018. 


Loveness Leonidas mhitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwembeni Mjini Musoma akisoma risala kwa niaba ya wenzake, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mhitimu wa Kidato cha nne katika shule ya Sekondari Mwembeni Mini Musoma Pius Mwita akipokea cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri katika masomo yake kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,  katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo alikuwa Mgeni rasmi.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mwembeni ya Mjini Musoma Bro. Erasmus Marando(kulia) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa mgeni rasmi  , katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mwembeni ya Mjini Musoma Bro. Erasmus Marando(kushoto ) na Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Dkt. Mniko wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018. 
Mkuu wa shule ya Sekondari Mwembeni ya Mjini Musoma Bro. Erasmus Marando(kushoto) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka , katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo alikuwa Mgeni rasmi.


Vijana wa Skauti wa Shule ya Sekondari Mwembeni ya mjini Musoma wakimvisha skafu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka , kama ishara ya upendo kwake na kumkaribisha katika  mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo alikuwa Mgeni rasmi.
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwemeni ya Mjini Musoma, wakifuatilia masuala mbalimbali, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wazazi, walimu, walezi , wanafunzi na wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwembeni ya mjini Musoma, ambapo alikuwa mgeni rasmi, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akiwatambulisha wenzake alisoma nao katika Shule ya Sekondari ya Mwembeni ya Mjini Musoma, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo alikuwa Mgeni rasmi .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye kipaza sauti) akiwa na wenzake aliosoma nao katika shule ya sekondari Mwembeni mwaka 1997-2000 na baadhi ya walimu waliwafundisha, katika  mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa  shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwembeni mjini Musoma wakitoa burudani, katika  mahafali ya 26 ya ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  alikuwa mgeni rasmi.
Mhitimu wa Kidato cha nne katika shule ya Sekondari Mwembeni Mini Musoma Jesca Gozbert  akipokea cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri katika masomo yake kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,  katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo alikuwa Mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni Mjini Musoma, ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akisaini kitabu cha wageni katika Shule ya Sekondari Mwembeni ya Mjini Musoma ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.
Baadhi ya walimu na watumishi wasio walimu wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwembeni mjini Musoma wakitoa burudani, katika  mahafali ya 26 ya ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  alikuwa mgeni rasmi.
Afisa Elimu (Sekondari) wa Manispaa ya Musoma akizungumza na wazazi, walimu, walezi , wanafunzi na wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwembeni ya mjini Musoma, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alikuwa mgeni rasmi, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!