Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini amezindua rasmi mfumo wa ununuzi
wa dawa na vifaa tiba kupitia kwa mshitiri mmoja wa mkoa ujulikanao kama JAZIA,
uliobuniwa kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi
katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali ngazi ya Mkoa na Halmashauri.
Akizindua mfumo huo Novemba 05, 2018 Mjini Bariadi Sagini amesema mfumo wa JAZIA si
mbadala wa Bohari ya Dawa (MSD) bali unalenga kuziba upungufu wa dawa, vifaa
tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika Bohari ya Dawa (MSD).
“JAZIA ni mfumo uliobuniwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI
kwa kushirikiana na wataalam washauri ili kuweza kuboresha upatikanaji wa dawa,
vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika vituo vya kutolea huduma za
afya vya Serikali ngazi ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, JAZIA si
mbadala wa MSD bali ni msaidizi wa MSD inapokuwa haina bidhaa husika.” alisema.
Aidha, Sagini alibainisha kuwa mfumo huu utasaidia
kupunguza gharama na bei ya upatikanaji wa dawa kwani bei za dawa na vifaa tiba
zitalingana na bei ya soko na sio matakwa binafsi ya wazabuni.
Aliongeza kuwa mfumo huo utapunguza urasimu
uliokuwepo wa namna ya kununua dawa nje ya MSD na hivyo kusaidia dawa kupatikana
kwa muda mfupi huku akiwataka Waganga wafawidhi wa vituo vyote vya kutolea
huduma za afya kuagiza dawa na vifaa tiba mapema wanapoona vinapungua kabla ya
kusubiri vifaa hivyo na dawa kuisha kabisa.
Kwa upande wake Mratibu wa Mfumo wa JAZIA Mkoa wa
Simiyu, Mfamasia Oscar Tenganamba amesema mfumo huu ulifanyiwa majaribio katika
mikoa ya Dodoma, Shinyanga na Morogoro na kuonesha mafanikio makubwa na sasa
hivi unatumika katika mikoa yote Tanzania Bara.
Naye mmoja wa wazabuni walioungana na kuwa mshitiri
mmoja wa Mkoa katika dawa na Vifaa Tiba (JAZIA) ambaye ni Mkurugenzi wa Operesheni
kutoka Kampuni ya Total Health Lab ya jijini Dar es salaam , Crispin Mtete amesema kampuni yake na Kampuni
ya Mufuruki Traders Company Ltd ya jijini Mwanza zitatoa huduma bora kwa
kuzingatia bei elekezi kama mkataba unavyoelekeza.
Mfumo wa JAZIA utatumia mzabuni mmoja aliyechaguliwa
kwa ushindani kujazia dawa na vifaa tiba vinavyokosekana katika Bohari ya Dawa
(MSD).
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (katikati) akisaini mkataba wa mshitiri mmoja wa
Mkoa katika dawa na Vifaa Tiba(JAZIA), Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Simiyu Mjini Bariadi, waliosimama kushuhudia ni Baadhi ya Wenyeviti wa
Halmashauri za Mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi wa
Operesheni kutoka Kampuni ya Total Health Lab ya jijini Dar es salaam , Crispin Mtete(kulia) na Mkurugenzi wa Mufuruki
Traders Company Ltd ya jijini Mwanza, Khalifa Mufuruki wakisaini mkataba Novemba 05, 2018 kama
wazabuni walioungana kama mshitiri mmoja wa mkoa wa Simiyu katika kutoa huduma
za dawa na vifaa tiba , katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini
Bariadi.
Mkurugenzi wa Mufuruki
Traders Company Ltd ya jijini Mwanza, Khalifa Mufuruki akizungumza jambo katika
uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, ASF. James John akichangia hoja katika
uzinduzi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa tiba “ JAZIA” uliofanyika katika Ukumbi wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
Viongozi mbalimbali wa
Halmashauri za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja
wa mkoa katika dawa na vifaa tiba “
JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Simiyu Mjini Bariadi.
Kutoka kulia,
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Kabuko, Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, ASF.
James John, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Mariano Mwanyigu, Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Melkizedeck Humbe na Katibu Tawala wa Mkoa,
Jumanne Sagini wakisaini mkataba wa mshitiri
mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa tiba “
JAZIA”, Novemba 05, 2018 mjini Bariadi.
Mganga Mkuu wa Halmashauri
ya Wilaya ya Bariadi, Dkt. Mike Mabimbi akichangia hoja katika uzinduzi rasmi
wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa
tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mfumo wa mshitiri
mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa tiba “
JAZIA”, Oscar Tenganamba (kulia) akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa, Bw.
Jumanne Sagini katika uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na
vifaa tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba
05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mfumo wa mshitiri
mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa tiba “
JAZIA”, Oscar Tenganamba (wa tatu kushoto) akimuonesha kitu Katibu Tawala wa
Mkoa, Bw. Jumanne Sagini katika mkataba wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa
na vifaa tiba “ JAZIA” katika uzinduzi
rasmi wa mfumo huo uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment