Tuesday, November 13, 2018

RAS SIMIYU: USHIRIKI WA MICHEZO KWA WATUMISHI UNAONGEZA ARI YA UTENDAJI KAZI

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema ushiriki katika michezo kwa watumishi ni moja ya njia za kuongeza ari ya utendaji kazi katika maeneo yao.

Sagini ameyasema hayo mwishoni mwa wiki Novemba 10, 2018 jioni wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu na Walimu wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya watumishi hao iliyochezwa katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo wenyeji Timu ya Walimu walikubali kichapo cha goli nne kwa tatu kutoka kwa Timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.\

“Mtu aliye na mwili wenye afya, akili yenye afya, aliye na uwezo wa kuruka na kuwepa ngwala kama nilivyokuwa nawaona hapa ni lazima hata katika kazi zake atafanya vizuri” alisema Sagini.

Aidha, Sagini ametoa wito kwa Maafisa Masuuli katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuwaunga mkono watumishi wao katika masuala ya michezo kwa kuwezesha wanapohitaji msaada kwao hususani katika suala la kuwawezesha kifedha, ili waweze kushiriki michezo mbambali ambayo pia inawasaidia kuimarisha afya zao na kuwaepusha na magonjwa yasiyoambukiza.

Akitoa shukrani kwa Timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Timu ya Walimu Manispaa ya Musoma kucheza mchezo huo  kwa nidhamu ya hali juu, Afisa Michezo wa Mkoa wa Mara, Bw. Evance Sangawe amesema nidhamu iliyooneshwa ni ishara kwamba watumishi hao wa Umma wanaweza kufanya kazi kwa kujituma bila kusimamiwa.

Kwa upande wake Kocha Msaidizi wa Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma, Mwl. Yisambi Mwazembe amesema mechi za kirafiki zina umuhimu mkubwa kwa watumishi wa umma kwani zina nafasi kubwa ya kuwakutanisha watumishi ambao walioachana muda mrefu shuleni, vyuoni na hata katika maeneo mengine ya kazi zao.

Naye Nahodha wa Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Elias Sebastian amesema mechi hiyo ya kirafiki imewakutanisha na  watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu na watumishi wa Manispaa ya Musoma ambao hawajawahi kuonana hapo awali, hivyo imechangia watumishi hao  kufahamiana na wenzao.
MWISHO

Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wenye jezi za bluu na nyeupe) na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma (wenye jezi nyekundu) wakiwa katika mnyukano mkali wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea kwa goli nne kwa tatu dhidi ya wapinzani wao.
Kikosi cha Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Kocha wao Bw. Justine Mnyandwa (kulia) kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma ,iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo Timu hiyo iliibuka kidedea kwakuichapa timu pinzani  goli nne kwa tatu.
Kikosi cha Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wenye jezi za bluu na nyeupe) na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma (wenye jezi nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki,iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea kwa kuichapa timu pinzani  goli nne kwa tatu.

Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mwenye trakisuti ya bluu aliyeinua mkono wa kulia juu) akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na mashabiki wa timu hiyo mara baada ya mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma,  iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea kwa goli nne kwa tatu dhidi ya wapinzani wao.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mara(kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakifurahia jambo, mara baada ya mechi ya kirafiki kati ya Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma,  iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma kumalizika , ambapo Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea kwa goli nne kwa tatu dhidi ya wapinzani wao.
Afisa Michezo wa Mkoa wa Mara, Bw.  Evance Sangawe akizungumza na wachezaji wa timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma, mara baada ya mechi ya kirafiki iliyochezwa Musoma kati ya timu hizo mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini kumalizika.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na wachezaji wa Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi  kabla ya safari ya kuelekea Musoma kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma,  iliyochezwa mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini  Musoma.
 Baadhi ya Mashabiki na Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakiishangilia ushindi wa goli nne kwa tatu ambao Timu ya Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliupata dhidi ya wapinzani wao Timu  ya Walimu Manispaa ya Musoma katika Mechi ya kirafiki ilichezwa katika Uwanja wa Posta Mjini  Musoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya Mashabiki na Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakiishangilia ushindi wa goli nne kwa tatu ambao Timu ya Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliupata dhidi ya wapinzani wao Timu  ya Walimu Manispaa ya Musoma katika Mechi ya kirafiki ilichezwa katika Uwanja wa Posta Mjini  Musoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya Mashabiki na Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakiishangilia ushindi wa goli nne kwa tatu ambao Timu ya Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliupata dhidi ya wapinzani wao Timu  ya Walimu Manispaa ya Musoma katika Mechi ya kirafiki ilichezwa katika Uwanja wa Posta Mjini  Musoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wenye jezi za bluu na nyeupe) na Timu ya Walimu wa Manispaa ya Musoma (wenye jezi nyekundu) wakiwa katika mnyukano mkali wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa mwisho mwa wiki katika Uwanja wa Posta Mjini Musoma, ambapo Timu ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliibuka kidedea kwa goli nne kwa tatu dhidi ya wapinzani wao.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!