Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka ameliomba Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT) kuendelea
kuwekeza katika miradi ya maendeleo na huduma mbalimbali za jamii mkoani hapa.
Mtaka ameyasema hayo Novemba 25, wakati
alipozungumza na waumini wa Kanisa hilo katika Usharika wa Tumain Bariadi
Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, ambapo alikuwa mgeni rasmi
katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10'ya vyoo
katika Shule Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School)
inayomilikiwa na kanisa hilo.
Amesema kanisa hilo limekuwa na mchango
mkubwa katika miradi mingi ya maendeleo hususani katika sekta ya elimu, afya,
maji na maeneo mengine muhimu ikiwemo sekta ya fedha ambapo Kanisa hilo
linamiliki Benki ya Maendeleo.
"Pamoja na mradi huu wa shule ya
msingi, tunaendelea kuliomba Kanisa kuona umuhimu wa kuwekeza katika miradi
mingine ya maendeleo kwenye mkoa wetu; Kanisa lina hospitali, benki na vyuo
vikuu; huu ni mkoa ambao bado haujawa na vyuo vikuu vingi kwa hiyo ipo nafasi
kwa kanisa kuona kama linaweza kuwa na chuo cha ufundi, chuo cha kati au Tawi
la Chuo Kikuu au kuwekeza katika eneo jingine ."alisema Mtaka.
Aidha, amesema Serikali inatambua na
kuthamini mchango wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa kuwa limekuwa
sehemu ya mafanikio ya nchi yetu tangu imepata uhuru, kwani wapo Viongozi na
Watanzania wengi katika maeneo tofauti nchini ambao wamepata elimu katika Vyuo
na shule za kanisa, huku akisisitiza kanisa kuendelea kuombea amani na mshikamo
wa nchi.
Naye Askofu wa KKKT, Dayosis ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala amesema Kanisa litaendelea kushirikiana
Serikali katika kuwafanya watu.wamjue Mungu na kuwaletea wananchi maendeleo,
ambapo amebainisha kuwa ujenzi wa shule ni moja ya njia za kushirikiana na
Serikali katika kuondoa ujinga na kujenga Taifa lenye watu walioelimika jambo
ambalo litairahisisha Serikali katika kuwaongoza wananchi wake.
"Kanisa litaendelea kushirikiana na
Serikali kuhakikisha watu wa Simiyu katika wilaya zote wanamjua Mungu;
tunajenga shule ili tuondoe ujinga watu waelimike, ujinga ukiondoka hata
Serikali inapata nafuu kuwaongoza watu wake" alisema Askofu Makala.
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi,
Katibu wa Kamati ya Ujenzi, Mwl. Oberlin Kileo amesema ujenzi wa Shule ya
Tumaini ulianza mwaka 2012, ambapo jumla ya vyumba vya madarasa tisa, matundu
ya vyoo 10, jiko, stoo na viwanja vya michezo vilijengwa na kugharimu shilingi
milioni 200 zikijumuisha na gharama za uwekaji wa miundombinu ya maji na umeme.
Ameongeza kuwa ili kujenga vyumba vya
madarasa vitano na matundu 10 ya vyoo vivyokusudiwa kujengwa kwa awamu ya pili
jumla ya shilingi milioni 120 zinahitajika.
Katika harambee hiyo jumla ya shilingi
41,526,500/= zilipatikana, kati ya hizo fedha taslimu zikiwa ni shilingi 7,466,
500 na ahadi shilingi 34, 060,000/= pamoja na vifaa mbalimbali vya ujenzi
ikiwemo mifuko 60 ya saruji, nondo tani moja, mchanga lori kubwa nne na
kokoto tripu mbili.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimsikiliza Askofu wa KKKT, Dayosisi ya
Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala katika harambee ya
ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre &
Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018
Mjini Bariadi.
. Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tumaini Bariadi Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya
madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini
(Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika
Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga wakifurahia jambo katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya
madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini
(Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika
Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa pili kushoto) akiimba pamoja na Kwaya ya
Uinjilisti kutoka KKKT Kijitonyama jijini Dar es Salaam katika harambee ya
ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya
Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre
& Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25,
2018 Mjini Bariadi, mstari pili ni Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Mashariki
ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto walioketi kwenye viti) na Askofu wa KKKT, Dayosisi ya
Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala wakiwa katika picha ya
pamoja na Kwaya ya Uinjilisti kutoka KKKT Kijitonyama jijini Dar es Salaam,
mara baada ya harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya
vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya
Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo,
iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Waimbaji wa Kwaya ya
Uinjilisti kutoka KKKT Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakiimba pamoja na Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga na Mchungaji wa KKKT Bariadi, Greyson Kinyaha, mara baada ya
harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika
Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School)
inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi..
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Maswa , Mhandisi. Paul Jidayi akizungumza na waumini wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tumaini Bariadi Dayosisi ya
Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano
vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini
(Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika
Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Waumini wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tumaini Bariadi Dayosisi ya
Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, wakifuatilia masuala mbalimbali katika
harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika
Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School)
inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Askofu wa KKKT,
Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akizungumza
na waumini wa kanisa hilo katika Usharika wa Tumaini Bariadi Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya
madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini
(Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika
Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi
wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Usharika wa Tumaini
Bariadi na Kamati ya Ujenzi ya Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre
& Primary School), baada ya harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya
madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule hiyo inayomilikiwa na kanisa hilo,
iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Kwaya ya
Uinjilisti KKKT Kijitonyama, viongozi wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya
Ziwa Victoria, Usharika wa Tumaini Bariadi Mjini Bariadi, baada ya harambee ya
ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya
Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika
Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Kwaya ya
Uinjilisti KKKT Bariadi, Timu ya Kusifu na kuabudu Bariadi, viongozi wa KKKT
Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Usharika wa Tumaini Bariadi, baada
ya harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo
katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary
School) inayomilikiwa na kanisa hilo,
iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Waimbaji wa Kwaya ya
Uinjilisti kutoka KKKT Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakiimba pamoja na Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala, , mara baada ya harambee ya ujenzi
wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na
Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa
hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Waumini wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tumaini Bariadi Dayosisi ya
Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, wakifuatilia masuala mbalimbali katika
harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika
Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School)
inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi
Waimbaji wa Kwaya ya
Uinjilisti kutoka KKKT Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakiimba pamoja na Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga na Mchungaji wa KKKT Bariadi, Greyson Kinyaha, mara baada ya
harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika
Shule ya Msingi na Awali ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School)
inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment